Fuso lenye maiti za kufundishia

Dah, hii thread inatisha sana. We do need Physicians ila kwa mtindo huu wa kuexchange cadaver kati ya Dar na Dodoma unatisha.

Nawaheshimu sana mnaosomea udaktari wa binadamu..... Binafsi hata kuangalia kidonda naogopa itakuwa kumpasua pasua mfu?

Mungu awatie nguvu katika hili dah.

Hata mimi nimetumia kujifunza maiti za hapa Tanzania. Ni heri kuwa na madaktari wengi kuliko kusikia maiti nyingi zatelekezwa kwa kuzikwa kt kashimo kadogo na manispaa.

wapendwa,

kweli habari hii inashtua na kutisha kwa mtu anayeisikia kwa mara ya kwanza, ila ni vizuri tukajieleimisha vizuri kuhusu cadaver na umuhimu wake .

mi naungana na kamanda wa polisi kuwa suala hilo ni la kiutawala zaidi. ni uzembe wa utawala wa MNH kuweka taratibu zote sawa sio mlinzi aletewe lori lina maiti ambao utaratibu wa kuwasafirisha haujakamilika

poleni kwa mshtuko wapendwa. dunia hii ni zaidi ya tuijuavyo. wanasema elimu haina mwisho, hiyo hapo topic nyingine ya cadaver, elimu mpya kwa wengi wetu hapa JF!

Mungu mkubwa!

mbarikiwe sana

Tunahitaji madaktari banaaaaaaa.
Unalalamika nini? Kwani daktari atakayejifunza kwa maiti ya ndugu mmoja kwa ajili ya kuokoa maisha ya ndugu wengi inaleta shida gani. Acha watu wafanye kazi yao. Wengi wa watanzania wanapoteza maisha kwa kukosa madaktari bingwa wenye ujuzi na kile walichojifunza kutoka kwenye hizo maiti.
Iwapo Nyerere angeogopa kuuawa kwa wananchi wake katika vita ya Idd Amin na akaamua kutopeleka jeshi kupambana, madhara yake yangekuwa vipi kama si mauaji ya wengi zaidi na hata kutawaliwa na Amin. Jaribu kuwa na uelewa wa mambo. Kama utaratibu uliowekwa Muhimbili ungekuwa haufai suala hili lisingeibuka leo kutokana na kitendo cha walizi kuzuia gari bali kwa wafiwa.

Kwa hili nina:hungry: walakini ila ngoja tutayasikiaga yote siku moja yatendekayo :hungry: maana kila kona ni ufisadi umeganda fluuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!

duh hayo mambo ya cadaver yamenishtua,kuanzia sasa nitaheshimu madaktari duh......

duh hayo mambo ya cadaver yamenishtua,kuanzia sasa nitaheshimu madaktari duh......

pilikapilika za madaktari hazizuii mtu kufa!!! ni sanaa ya kiwango cha kuhofiwa ambayo ni state of the art that can postpone death we hate the most. kumbuka....mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, eventualy tunakufa hakika, hata wakuzunguke madaktari mabingwa wa dunia nzima waliosomea cadaver miaka ya kupindukia. haki ya maiti ni kuzikwa. kuitumia vinginevyo ni kukusanya specimen za sanaa.

Lakini bado ndugu yangu wanapunguza vifo ile mbaya.

Nijuavyo ni kuwa maiti za nchi moja hubadilishana na za nchi ingine not otherwise
Sasa kama mumefikia kubadilishana ya mkoa kwa mkoa inanifanya kukumbuka msemo wa Nyerere kuwa hata mambo ya msingi mnayatilia shaka!

Bado Suala lenyewe linatisha maiti ya Mtanzania kwenye Lorry bila shaka halina kiyoyozi, halafu safari ya Dodoma zinapigwa na jua, kwenda na kurudi kisha masaa kumi nje zimezuiwa na walinzi bila shaka zilishaoza huu ni uungwana kweli hivi nani anataka maiti yake idhalilishwe namna hiyo. Kukosa ndugu isiwe sababu ya kuwanyanyasa wanadamu na hasa pale wanapokuwa hawana uwezo wa kujitetea.

Duh!
Hii inasikitisha kweli.
Eti maiti ikikaa zaidi ya siku 14 ndio wanaigawa,
Je! Ikitokea maiti zote zinapata ndugu zao kabla ya hizo siku watatumia zipi kwa mafunzo?
wakikosa watasaka watu mtaani vijana wakasomee

Ahaaa,,, napata picha, cku moja nilitoka skuli ya elimu UDOM kwenda kutembea skuli ya tiba udom, km ilivyo ada kwangu, wakati wa kurudi, tukapark pembeni baada ya kuona lorry maabara kwa nje maana ilikuwa wkend, tulidoubt ni wezi, tukaenda, kufika lorry imejaa majeneza na maiti zake, tulivo hoji jamaa wakajibu maiti zimetoka Ivory cost. I was extremely terrified'

sasa, kama ndugu hawajaja uongozi ufanye nni? kama wakizikwa na manispaa ndio mnaona heri? sioni ajabu ya maiti hizo kutumiwa kwa manufaa ya wengi. kama kuna jingine hapo sawa

Bado Suala lenyewe linatisha maiti ya Mtanzania kwenye Lorry bila shaka halina kiyoyozi, halafu safari ya Dodoma zinapigwa na jua, kwenda na kurudi kisha masaa kumi nje zimezuiwa na walinzi bila shaka zilishaoza huu ni uungwana kweli hivi nani anataka maiti yake idhalilishwe namna hiyo. Kukosa ndugu isiwe sababu ya kuwanyanyasa wanadamu na hasa pale wanapokuwa hawana uwezo wa kujitetea.

usiwe na wasiwasi mpendwa,

hali haiko hovyo hivyo unavyofikiria. huwa wamehifadhiwa vizuri ili watumike kwa muda mrefu. huko kwenye chumba cha cadaver, maiti mmoja anaweza kutumika hata zaidi ya mwaka mzima (kumbuka wanasoma topic moja kwa wakati mmoja). mfano leo watachunguza misuli ya tumbo, kesho joint za nyonga, keshokutwa misuli ya kifua, nk na wanaendelea hivyo hadi sylabus yao imekamilika! kama wangekuwa wanarundikwa tu bila kuhifadhiwa vizuri, basi huo uvundo huko cadaver lab sijui kama kuna mtu angeingia!

haya mambo hayakuanza leo, yameanza kabla wewe na mimi hatujazaliwa. yana umri sawa na profession yenyewe ya tiba za binadamu, so kwa kuwa wewe mwenzetu umejua leo, basi isiwe tabu. tuliza moyo hii ndiyo dunia yetu!

ubarikiwe sana mpendwa!

nakuombea amani ya Bwana ipitayo akili zote!

Lakini bado ndugu yangu wanapunguza vifo ile mbaya.

vifo havipunguzwi mkuu, zamani ilikuwa nadra kijana kufa, achilia mbali watoto, those days hakukuwa na cadaver, mambo ikoje siku hizi with so many cadavers, take note: as soon as a man is born he starts to die, kula ni mojawapo ya njia za kuahirisha kufa, tusije tukakosea kuhitimisha kwenye hili!, tusijivishe hisia za umaiti, you can not die and still think, thinking dead suits religious leaders & belivers.

Nijuavyo ni kuwa maiti za nchi moja hubadilishana na za nchi ingine not otherwise
Sasa kama mumefikia kubadilishana ya mkoa kwa mkoa inanifanya kukumbuka msemo wa Nyerere kuwa hata mambo ya msingi mnayatilia shaka!
Heri umesema ujuavyo. Lakini hujaenda kupasua hizo maiti. Wasikia tu kutokana na hadithi. Mna pesa hata za kwenda kuchukua maiti jirani? Dodoma tu hapo wanatumia fuso, sasa huko nje mtapeleka ndege? Kuwapa pesa wanafunzi wakafanye field ni shida, sembuse kwenda kuchukua maiti nje wakati hapa zipo kibao? Cadaver nyingi zinatumiwa toka hapahapa.

Bado Suala lenyewe linatisha maiti ya Mtanzania kwenye Lorry bila shaka halina kiyoyozi, halafu safari ya Dodoma zinapigwa na jua, kwenda na kurudi kisha masaa kumi nje zimezuiwa na walinzi bila shaka zilishaoza huu ni uungwana kweli hivi nani anataka maiti yake idhalilishwe namna hiyo. Kukosa ndugu isiwe sababu ya kuwanyanyasa wanadamu na hasa pale wanapokuwa hawana uwezo wa kujitetea.
Hahahaa, yaani umeishi kwa taabu zote duniani (tena kwa bahati mbaya ukiwa Mtanzania) halafu unataka ukiwa maiti ufidiwe kwa kuwekewa kiyoyozi? Na kaburini itabidi sasa waweke Air conditioner. Tukubali tu, tukishakufa thamani zetu zinakuwa zimekwisha. Tusijidanganye kwa mwonekano wa sasa, tukifa hatuna deal tena. Hapo ndipo namkumbuka Mungu.

Umenichekesha mkuu!

Back
Top Bottom