Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 1,997
- 7,551
Na Malisa GJ
Habari kaka.
Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.
Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.
Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.