Fursa ya kupata mapenzi ya kweli kwa wanawake wenye umri wa Miaka 38 - 55 ipo. Kwanini mnadanganyana otherwise?

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,821
Toxic batchelor: Money Penny it's high time uwaambie hao madogo unaowaandikia ukweli kuhusu real love

Tunasoma nyuzi zako tunacheka sana at the same time tunawahurumia Sana wanao comment

Yani NI kama age 20 mpaka 35 wako chocked when it comes to start a family na ndoa, wanapata presha za Marafiki, ndugu, jamaa, jamii kwamba usipoolewa UMRI huo hautaolewa tena 😱

Embu kawaambie hao watoto, wafanye KAZI, watafute hela zao, wafanye maisha Yao, waachane na kuweka mapenzi mbele na maendeleo nyuma

Sasahivi divorce ziko nyingi Tanzania sababu kuu ukiangalia NI kwamba wanawake wengi waliolewa mapema Kwa presha za society walikuwa hawajajiandaa

Ivi mshauri WA hawa watoto NI Nani?
Nani aliwadanganya ukifika Miaka 40-50 huwezi kuanza familia?
Biology clock ipi wanaongelea?
Kuna watu wameolewa Miaka 18 - 30 waka divorce in their 38 na wame remarry in their 45 happily married

Kwa karne ya sasa Mwanaume wa maana hawezi na hapendi oa mwanamke ambae hajielewi, hana malengo, hana maisha yake yaliyojaa kabla ya ndoa, kifupi wanaume wengi wanataka mwanamke aliejaa na anaejielewa.

Watoto waache kudanganyana kwenye social medias, kuwa wanaume huku juu hamna, wapo, wapo weeengi tena wa maana na hawajaoa na wanatafuta, na wanatafuta WA maana wenzao, watu wanazaa hata kwenye Miaka 50 tatizo NI kuwa na mipango na hela.

Vijana wanataka Ku rush maisha in the name of biological clock sasa ukiwa divorce hao watoto unaleaje ukiwa ulikuwa tegemezi Kwa mwanaume Kwa Kila kitu?

Waache kuisumbua serikali, wafanye KAZI, watafute maisha Yao, lakini ukweli utabaki pale pale, fursa ya mapenzi Kwa UMRI WA Miaka 38- 50 IPO nyingi Sana as you age tena ina rahaaa kuliko ukiwa naive and moneyless.

Tusaidie kushea hii Kwa hao watoto wako wa JamiiForums
 
Unahamasisha mabinti waendelee kudanga halafu waje kuolewa uzeeni kuanza familia at 40 years old ni kujichimbia kaburi la wazi ufikapo huo umri bora usioe au kuolewa kama unataka kuishi muda mrefu duniani nje hapo yatakukuta makubwa na umri utakaokuwa nao hautaweza kuhimili mikiki mikiki.
 
Unahamasisha mabinti waendelee kudanga halafu waje kuolewa uzeeni kuanza familia at 40 years old ni kujichimbia kaburi la wazi ufikapo huo umri bora usioe au kuolewa kama unataka kuishi muda mrefu duniani nje hapo yatakukuta makubwa na umri utakaokuwa nao hautaweza kuhimili mikiki mikiki.
Hakuna sehemu nimeandika wakadange
We vipi?!
Au kusoma hujui?!
 
Aposte nitaandaa uzi nishauri wana ndoa, Tangu nimempata mke wangu wa maisha nimekua na knowledge kubwa sana kuhusu mahusiano.

Nitakuja na bandiko, wanandoa na wanaotaka kuingia kwenye ndoa jiandaeni.

Kocha sasa nacheza na mm, coz nina mke.
Usitupake blue band Tu tukaanze kuumwa pumu in the name of get married
Pumu zenyewe sasa ndio haya makasiriko ya talaka
Kama hujajaaa subiri ujazwe🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom