lulu za uru
JF-Expert Member
- Aug 7, 2015
- 2,184
- 2,688
Sasa ilikuwa awasingizie ili nn mkuu?acheni ushabiki maandazi.
IliKila alichofanya Magufuli kinatokana na hisia zake mbovu. Kwenye ile clip maarufu ya kabla ya 2015 ambayo na Charles Kitwanga yupo, Jiwe alisikika akisema kuwa madini yanaibiwa kupitia mchanga unaosafirishwa nje ya nchi nakwamba akiwa Raisi watu watalimia meno.
Baada ya kuwa Rais akataka ku-prove kuwa hypothesis yake iko kweli ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.
Kwa vile Magufuli alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.