Funza ndani ya korosho

Kitrack

Member
Dec 11, 2011
50
16
Habari za Asubuhi wadau,naomba mnijuze kuhusu hili suala.

Juzi nimenunua pakti la korosho pale Kisutu sokoni zikiwa fresh zikinukia vizuri, nikaanza kula kidogo.

Kwa kuwa nilinunua kilo nzima nikaja nazo hadi nyumbani, usiku watu wakala.

Asubuhi siku ya pili nataka kupata kifungua kinywa,nikachukua kisosi nikaweka korosho kidogo..dah nikaona funza mmoja anatoka kwenye korosho.Ikanibidi nianze kuzikagua moja moja ndipo nilipogundua nyingi zinafunza wadogo(larvae sijui) na nyingine funza wakubwa.

Je, funza hawa ukiwala na korosho hawana madhara kiafya?

Na Je, funza hawa wanapatikanaje ndani ya korosho ambayo haina hata katobo?.

Natanguliza shukrani.
 
Ndiyo bidhaa zetu hizo; kwa kisutu pana wafanyabiashara wahuni sana;
hizo korosho zitakuwa zimekaa sana lakini wanafanya kuzipasha moto ili
harufu isipotee, au wanachanganya na mpya;

Kuhusu kula funza ngoja waje wataalam, vinginevyo mtafute rafiki yako
daktari uongee naye; kumbe ni heri kula majimbi kuliko korosho, bei kubwa ila
ni hatari;
 
Kuna Korosho Zimeandikwa Munawari.

Zinahifadhiwa Kwenye Mifuko Pia Zinawekwa Chumvi Kwa Mbali Nimekuwa Mtumiaji Ila Sijaona Funza.

Kuhusu Kula Funza Hiyo Haina Shida Ni Kama Kumbikumbi,Senene,
Huwezi Kupata Madhara
 
Mkuu kwanza pole sana kwa hasaraa uliyoipata, tena yaani ulitakiwa kurudi kwenye hiyo supermarket ukawaelezee wakulipe na fidiaa.

Kuhusu kula funza hilo hata usijari hakuna athari mbaya itakayokutokea hivi karibuni na hata baadae. Ninakwambia hivi hata mimi imenitokea hivi karibuni niliwabugia wakiwa kwenye tikiti maji pasipokujua, tena nilianzisha na uzi humu so unaweza kuperuzi ukaona ushauri na mawazo ya wataalamu.

lakini kwa kifupi tu kwamba hakuna madhara yoyote utakayoyapata kwa kumeza funza.
 
Funza ule uji uji mweupe wa ndani in full mavitamini mkuu, wala usiogope. Tena kama bado zipo zibugie zote ujenge mwili
 
Asanteni kwa kunitoa wasiwasi,maana ilinibidi nizitupe zilizobakia
 
Nakushauri uwe unafungua kichwa kwa kutumia vyakula vya asili kama magimbi, mihogo, viazi and the like. Kuhusu kula funza hakuna shida umeongeza vitamin mwilini wala usijisikie vibaya, korosho zilizobakia usizitupe wewe kula tu na hao funza na wazuri sana mwilini
 
Baba yangu alinifundisha hili, nikinunua korosho kabla sijaanza kula au kuwapa watu, niweke frying pan kwenye moto mdogo, nizipashe moto taratibu. Baba yangu hana uzoefu wa science bali aliniambia zimepita kwenye mikono ya watu wengi. Ninamshukuru kwa mafundisho yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom