Funza hutokea wapi?

Funza hutokea wapi?

mathematics

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
3,324
Reaction score
1,116
Umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji.

Siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?

Nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza?

Hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawahi pata majibu!!
 
Hata mimi nasubiri jibu. Funza ni shida, wapo mpaka kwenye vumbi si kwa vitu vilivyooza tuu.
 
Tupo wengi tunaojiliuza hili mkuu.
 
umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji. siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?

nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza??!!

hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawah pata majibu!!

Kuna mamilioni ya bacteria wanaotuzunguka ambao hawaonekani kwa macho ndio huleta haya yote na si kwenye vyakula tuu bali hata mwili hasa sehemu zako za siri na mdomoni
 
Kuna mamilioni ya bacteria wanaotuzunguka ambao hawaonekani kwa macho ndio huleta haya yote na si kwenye vyakula tuu bali hata mwili hasa sehemu zako za siri na mdomoni

Du! Hatare
 
Funza si kiumbe kinachojitegemea. Funza ni hatua mojawapo ya viumbe fulanifulani, kama vile nzi. Hivyo basi, uonapo funza, ujue kuna mdudu ametagia mayai yake hapo na yameanguliwa. Jua kuwa funza ni hatua tu Mkuu

Mzee Tupatupa
 
Funza ni vimelea wadogo wa nzi, wakipevuka wanakuwa ni nzi.
Kifupi kabisa nzi huwa anataga mayai yake kwenye chakula.
 
Funza dune kuja hapa Mara moja ujiekeze asili yenu!!
 
Kuna mamilioni ya bacteria wanaotuzunguka ambao hawaonekani kwa macho ndio huleta haya yote na si kwenye vyakula tuu bali hata mwili hasa sehemu zako za siri na mdomoni

mkuu hao bakteria wasionekana kwa macho wanabadilikaje kuwa funza?
 
Watu wa kigoma wangejibu hili swali.

swissme
 
Funza si kiumbe kinachojitegemea. Funza ni hatua mojawapo ya viumbe fulanifulani, kama vile nzi. Hivyo basi, uonapo funza, ujue kuna mdudu ametagia mayai yake hapo na yameanguliwa. Jua kuwa funza ni hatua tu Mkuu

Mzee Tupatupa

mkuu chombo kinafunikwa hakuna nafasi ya kupita mdudu, hata hao nzi hawawez kupenya na kutaga mayai. lakini ukifunua chombo unakuta funza!
 
Baada ya kurutubishwa kwenye hicho chakula hubadilika na kuwa funza

Mkuu hapa natofautiana na wewe. Bacteria hawezi kubadilikA kuwa funza. bacteria atabaki kuwa bacteria. Funza ni hatua mojawapo ya ukuaji wa viumbe hasa wadudu ambao wanapitia hatua za metamorphosis (complete au incomplete).
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Mayai hutagwa hata kabla ya kufunikwa

Mzee Tupatupa

Zanzibar-ASP na mkuu vuta nikuvute, fanya jaribio chemsha nyama kwamba unaua wadudu wote, puliza dawa chumba kuua nzi na wadudu wote, weka nyama humo chumbani kwny chombo cha wazi au chombo funika vizuri. baada ya siku kadhaa nenda angalia hizo nyama, utakuta kibaoo.
 
Last edited by a moderator:
Umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji.

Siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?

Nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza?

Hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawahi pata majibu!!

Mkuu nenda kasome kwenye THEORIES OF EVOLUTION,hasa Spontaneous Generation theory,naamini utapata majibu ya swali lako.
 
nami nashangaa sana hawa wadudu hata ununue kama nyama safi uiweke hata ghorofa ya kumi tena uifunge vizuri baada ya siku kadhaaa lazima funza wataibuka tu,na hata kama nzi hakuna
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom