Funza hutokea wapi?

Funza hutokea wapi?

Mi nadhani kuna story nyingine kabsaa kuhusu funza.

Kwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kukata magogo polini mtanielewa.

Ukishusha kitu ghafra utaona nzi wa kijani wanaopatikana vyooni wameripoti,mara wanatotoa funza wadogo weupe.nadhani maisha ya inzi yanaanzia mazingira kama yale.

Sasa vip ndani ya chupa iliyofungwa madhubuti kwa mfuniko,fridge ambayo hujaifunguliwa mlango mwezi mzima ikiwa haijawasha na samaki ndani yake???.labda mniambie huwa mayai yameishatagwa.ingawa jaribio langu litakataa majibu yenu tena.kwani hata uwashe oven pandisha joto mpaka mwisho kwa lengo la kuua mayai,kisha ikiwa ya moto hivyo hivyo chukua mshikaki wa mbuzi choma ukiwa unatoka jikoni na moto wake kisha fungia humo.zima oven usiiwashe siku 7 hakikisha hakuna hewa mpya itaingia humo.kisha rudi hapa uliwa na mshangao na maswali kama yangu.
 
Mkorinto, kwanza kabisa ukishasema hakuna hewa mpya itakayoingia ina maan kwamba bado kuna hewa ya zamani ndani ya chupa ambayo ina bacteria wa kutosha watakaofanya decay process ya meat.pili ili hao funza(maggots) waweze kutokea lazima nyama ama chochote kile kioze na purpose ya hao bacteria ni kuozesha hiyo nyama.Tatu lazima wawepo flies watakaodondosha mayai yao katika decayed meat hayo mayai ndio yata develop into maggots.prove ya hili ilifanywa na Italian biologist Francesco Redi in 1668 alionyesha kwamba decaying meat protected from flies does not spontaneously produce maggots.
 
Mkorinto, kwanza kabisa ukishasema hakuna hewa mpya itakayoingia ina maan kwamba bado kuna hewa ya zamani ndani ya chupa ambayo ina bacteria wa kutosha watakaofanya decay process ya meat.pili ili hao funza(maggots) waweze kutokea lazima nyama ama chochote kile kioze na purpose ya hao bacteria ni kuozesha hiyo nyama.Tatu lazima wawepo flies watakaodondosha mayai yao katika decayed meat hayo mayai ndio yata develop into maggots.prove ya hili ilifanywa na Italian biologist Francesco Redi in 1668 alionyesha kwamba decaying meat protected from flies does not spontaneously produce maggots.

Wakuu tusibishane na sayansi, ukweli ndio huo uliokwisha semwa, ya kwamba funza ni Hatua ya pili katika ukuaji wa wadudu kama inzi hatua ya kwanza ikiwa ni Yai. Nzi jike akishakuwa na mayai yaliyotayari kwa kutagwa hutafuta sehemu ambayo akitaga yai kitakachotokea kitakuwa na uhakika wa chakula. Mara nyingi nzi atakwenda kutaga kwenye vyakula n.k. Baaa ya siku kadhaa kutegemeana na aina ya mdudu, hatua hii hutokea (Larva), baadae hii larva inabadilika kuwa Pupa na Nzi atatokea kutoka kwenye pupa.

Pia ikumbukwe kuwa kuna aina ya Nzi ambao badala ya kutaga Mayai, wao hutaga Larva kabisa hawa kitaalamu huitwa Larviparous.

So Nzi anapotua kwenye chakula chako kabla hujakifunika vyema atafanya moja wapo ya mambo yafuatayo ama yote:
1. Kufyonza fluids zilizopo kwenye chakula (Kula) kutegemeana na aina ya chakula
2. Kutaga mayai (Kutegemeana na Jinsia ya nzi)
3. Kuacha vimelea vya magonjwa (e.g.Bacteria) hapa nzi huyu atakuwa ana act kama mechanical vector
 
Hivi na wale inzi ambao ukila embe mfano embe dodo hutokea hivi ile inakuaje?
 
Umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji.

Siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?

Nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza?

Hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawahi pata majibu!!

Haiwezekani... Funza anatokana mayai ya inzi au jamii ya nyingine ya nzi bila kutagwa mayai hakuna fuza labda wakati unafunika mayai yalishatangwa tayari..
 
bado sijaona majibu ya kitaalamu kuhusu utokeaji wa funza asee
 
Mliosema nzi anaweza kutaga mayai mapema hata kabla ya kufunika nyama, ningependa kufahamu je mayai ya inzi yanaweza kufa iwapo nyama itatokoteshwa kwa maji ya moto?
 
Analyst ulichoandika ni kweli wala sikipingi na maelezo yako yanawiana kwa kiasi kikubwa na yangu labda huwe hujaelewa tu.
 
kuhusu funza kusababishwa na nzi;
kuna watu wamechangia nyama iliyowekwa kwenye ovena ikapata moto, ovena ikazimwa lakin bahat mbaya nyama ikasahaulika humo, lakin funza wakatokea. mayai nzi alitaga muda gani??

kuhusu bakteria kusababisha funza;
baketria anasababishaje funza haijaeleweka, bakteria ndio anabadilika kuwa funza? bakteria ndio tunakubali anasababisha chakula au nyama iharibike, mbona isiharibike tu na kuoza bila kutokea funza?!
 
Mie huwaga nataka kujua wanapotokea senene tu,bhaaasi!
 
Navyojua mimi funza hutokana na viroboto
akikung'ata wewe binadamu au Nguruwe huendelea kuingia kwenye nyama na hatimaye hunenepeana huko ndani ya nyuma na kuwa mweupe

Ni kama mchwa wanavyotokana na kumbikumbi! Kumbikumbi akidondosha yale mabawa yake wanaanza kufuatana wawili huku dume akimfuata jike kwa nyuma na baadaye kutafuta au huchimba kashimo na kuanza maisha huku
Jike kale kanakuwa malkia wa mchwa
 
Kwanza tukubaliane kila kitu kina bacteria

Hao bacteria wanapokua kwenye nyama ndio wanasababisha funza na sio kila funza ni matokeo ya nzi

Na sio kwamba kuchemsha kitu ndio kuua bacteria.Na bacteria walio kwenye nyama inabidi uiunguze nyama yote sio kwamba ubakishe ili uangamize bacteria

Ndio maana moto wa kuchemshia maji hauyeyushi chuma

Njia pekee ya kuangamiza bacteria walio kwenye nyama ni kuipoteza hiyo nyama ili upoteze hao bacteria wasababishao funza
 
kuhusu funza kusababishwa na nzi;
kuna watu wamechangia nyama iliyowekwa kwenye ovena ikapata moto, ovena ikazimwa lakin bahat mbaya nyama ikasahaulika humo, lakin funza wakatokea. mayai nzi alitaga muda gani??

kuhusu bakteria kusababisha funza;
baketria anasababishaje funza haijaeleweka, bakteria ndio anabadilika kuwa funza? bakteria ndio tunakubali anasababisha chakula au nyama iharibike, mbona isiharibike tu na kuoza bila kutokea funza?!

Bacteria wala hawasababishi funza kazi ya bacteria ni kuozesha (decay process) hiyo nyama ili wakati wa kukua kwa mayai ya inzi(eggs) kuelekea kwenye hatua ya pili larva(maggots) ambao ni funza waweze kujipatia nutrients za kutosha kwa ajiri ya kukua kutoka kwenye nyama iliyooza na unatakiwa ujue ya kwamba nyama ambayo itawekwa mbali na flies kiasi kwamba hatukakuwa na mayai yaliyoanguliwa kwenye hiyo nyama basi hakutakuwa na funza watakaotokea.
 
mbona nyama iliyokaushwa au kubanikwa haitoi funza hata ikae muda mrefu?? je hakuna nzi anayetua na kutaga kwenye nyama iliyokaushwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom