SoC02 Funguo za kupata fursa zaidi

Stories of Change - 2022 Competition

Stevenash classic

New Member
Jul 18, 2022
4
1
Kwa majina naitwa Steven J ni mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo cha Dodoma, Shahada ya utawala katika elimu. Naomba nikuletee makala fupi kuhusiana na Funguo za kupata Fursa zaidi, ambavyo ni vitu nilivyojifunza kupitia maisha niliyoyaona kwa watu lakini pia niliyoyaishi mimi mwenyewe.

Makala hii imejikita sana kuzungumzia watu ambao wamekwisha kupata Fursa mbalimbali ambao wanatamani kupata Fursa nyingine kubwa zaidi ya walizonazo na wengine wanatamani kupandishwa vyeo hivyo katika makala hii nitazungumzia kwa ufupi funguo mbili tu ambazo zikifuatwa na watu wa namna hiyo watafanikiwa;

1. Bidii na kujituma
Watu wengi wamepata fursa mbalimbali ambazo mwisho wao wameona hazina maslahi yoyote kwao wametamani wangepata nyingine zaidi Lakini pia wapo wanaotamani wangepandishwa vyeo makazini kwao. LAKINI chakushangaza haohao wanaotamani hivyo ni moja ya wategezi,wavivu na wanaofanya kazi au vitu kinyonge kama wamelazimishwa .

Makala hii itakusaidia wewe unayetamani kupata Fursa nyingine zaidi na kupandishwa cheo. Kwanza lazima utambue hakuna mwajiri anayependa mfanyakazi mvivu,hivyo ukitaka umvutie mwajiri wako hebu jitume katika hiyohiyo kazi aliyokupa kwakufanya yafuatayo;

(a)Jifunze kuwa na bidii wakati wote
Hii itakusaidia nakupelekea bidii kuwa tabia kwani "mazoea hujenga tabia" sio wakati ambao bosi au mwajiri yupo anakuona ndo unaanza kujituma au kufanya kazi kwa bidii lazima ujue kuwa nje ya bosi wako wapo watu wengine wanaokutazama ambao wangeweza kukupa fursa nyingine kubwa zaidi ya unaoyoifanya kama tu ungefanya kwa bidii kwahyo ule uvivu unakuwa kufuli la kupata Fursa nyingine zaidi Lakini pia hawa watu wanaokuona nje ya bosi au mwajiri wako wanaweza kutumika kama wajumbe wakupeleka taarifa kwa mwajiri wako ambazo zaweza kuwa nzuri au mbaya kwahiyo ukiwa mvivu tegemea wataenda kumwambia uvivu ulionao Ila kama watamwambia juhudi ulizonazo bosi anaweza kuamua kukupandisha cheo kwaajili ya maendeleo ya Taasisi yake. Kumbuka (uvivu unamatokeo yake na juhudi inamatokeo yake matokeo haya yote husema au hujieleza)

(b)Jitahidi angalau kutumia uwezo wako wa ziada na ubunifu ili kuongeza ubora wa kazi yako na kuonesha utofauti wa ufanyaji kazi Kati yako na wafanyakazi wengine na sio kufanya kazi kutimiza wajibu tu nakwambia utabaki palepale na ikiwezekana utashushwa zaidi kwa mfano unaweza kuamua kuwa unawahi kazini kabla ya wafanyakazi wenzako wote unaanza kufanya majukumu yako mapema na unaweza kuwa unafanya kazi hata kwa mda wa ziada nakwambia kazi yako haitakuwa sawa na wengine.

2. Uaminifu
Hii pia ni moja ya sehemu ambayo wafanyakazi wengi wamefeli ikawasababishia washindwe kupata Fursa nyingine zaidi na wengine kukosa kazi zao kwasababu wamekuwa wakitaka kujifaidisha wao kuliko wamiliki wa mali au taasisi fulani ambao ndio waajiri wao lakini moja ya sababu inayowafanya wafanyakazi wengi kukosa uaminifu nakujiingiza kwenye wizi au kuiba mali za waajiri wao ni;

-Tamaa yakutaka wafanikiwe mapema, mtu anatamani angenunua gari nzuri na ajenge nyumba lakini akilinganisha na mshara anaolipwa anakuta bado hautoshelezi kufanya yote hayo kwahyo kwakutaka kuharakisha kuyafanya hayo yote anaona Bora aibe fedha za kampuni au taasisi fulani anayofanyia kazi matokeo yake unakuta anapoteza kazi yake na wakati mwingine anapokonywa hata nyumba na gari alivyokuwa amenunua.

-Lakini pia shida,umasikini au dhiki, hii pia inaweza mfanya mtu ajikoseshe uaminifu kwakuona anakabiliwa na shida na mshahara alionao ni mdogo hautoshelezi mahitaji yake yote kwahiyo anaona Bora akafanye ubadhilifu tu wapesa za kazini anakofanyia ambazo si zake ni za mmiliki wa taasisi hiyo.

Hapa wengi huwa wanasahau kuwa shida huwaga haziishi na huwezi tatua shida zako kwakutegemea pesa ya mtu maana unaweza kufanikiwa kwa mara kadhaa lakini ipo siku moja utaumbuka na ndio unakuwa mwisho wakazi yako na kile kiwango cha mshahara ulichokuwa unakiona kidogo nacho kinapotea pia Ila matatizo yanakuwa palepale na yanakuwa yameongezeka kwani kukosa kazi nalo ni tatizo pia.

Kwahiyo ni vyema unapopewa fursa fulani au kazi fulani ukaifanya kwa uaminifu kwasabu mwajiri anakuwa kakuamini kwahiyo nawewe Jifunze kuamininika kwa maana fursa moja inaweza kuwa mlango wa fursa jingi kuja na kukupandisha pia ulipokuwa kwenda nafasi ya juu zaidi. Ni kweli kwamba matatizo huwa hayaishi na hayanaga hodi wala taarifa kwahiyo ili kuendelea kujijengea uaminifu hata ukiwa na shida kwa kufanya lifuatalo;

-Kuwa muwazi kwa mwajiri wako
Wakati ambao umepatwa na shida fulani na huna fedha usichukue hatua ya kwenda kujichukulia tu pesa za taasisi hata Kama wewe ni muhasibu muelekeze tu mwajiri wako(bosi) kwamba ninashida fulani inayohitaji pesa Ila mimi sina kwahyo kutokana na uzito wa tatizo ulilonalo bosi atakusaidia kwakukupa tu pesa au kukuazima kuliko unabeba tu mwishowe anagundua unakuta anatoa kauli zifuatazo ambazo huwa zinaumiza Sana;

Bosi; John sikutegemea kama wewe unaweza kufanya hivi nilikuamini sana na nilikuwa nina mpango nikupandishe cheo uwe meneja na Kama ulikuwa na shida kwanini usingenambia mimi ningekusaidia.

Sasa wakati huo bosi anasema hivo wewe ushapoteza kazi na uaminifu nakurudisha matukio nyuma haiwezekani.

Kwa hiyo ni Bora kuwa mwaminifu kwamaana mchawi wa kutopandishwa cheo na kupata Fursa nyingine zaidi ni wewe mwenyewe.

ASANTEEE.
 
Makala nzuri. Lakini tunawachukuliaje watu ambao wanaizo funguo zote na hawafanikiwi zaidi ya walipofikia? Shida ni nini unadhani? Kwasababu kuna makosa jinsi tunavyowafikilia watu. Wengi was watu sio wavivu kama watu wengi wanavyosema au kudhani..tunawaonea na kuzidi kiwagandamiza..wewe unasemaje kuhusu hili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom