Funguka kuhusu abortion

Funguka kuhusu abortion

Third Eye

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2012
Posts
373
Reaction score
210
Umeshawahi kufanya abortion? (Kwa wanawake)

Umeshawahi kusuport/ kukataa mwenzi wako kufanya abortion? (Kwa wanaume)

Nini sababu za kufanya abortion?

Nini mtazamo wako juu ya abortion? Unadhani iwe legal Tanzania?
 
Kwakwli swala hili ni janga la kitaifa. Tukubali tukatae humu jamvini asilimia kubwa kama sio wote tushawahi kushiriki swala hili on either way.
Nakumbuka livokua chuo mwalimu wetu aliwahi kutuambia kua watu walokua kwenye ndoa ndio most aborter kuliko vijana ambao hawapo kny ndoa. darasa loote lilihamaki na kukataa. Lakini ukweli huu mekuja kuubaini these days baada ya kumuuliza rafiki angu dokta.
Sababu hasa za hii kitu ni unplanned pregnant. Utakuta mama anamtoto anamwaka mmoja tayari kashika momba nyingine.
Kuhusu iwe legal. hapana. ni dhambi kubwa kuabort.
 
Bahati mbaya mada hii itakosa wachangiaji wengivna sababu tunazijua. Mimi nadhani asilimia kubwa tumeshiriki directly or indirectly katika utoaji wa mimba, wanaume huwa wakubaliana na hali halisi alafu wanashiriki financially.
sababu zake
1. Mimba zisizotarajiwa, hasa kwa wanandoa
2. Kufanya mapenzi na wanafunzi ambao kiuhalisia hawako tayari kubeba mimba
3. Kukimbia majukumu,hasa kwa wanaume

Kuhalalisha utoaji wa mimba si sahihi ila kama ukilitizama swala hili kwa undani, ni kama vile limehalalishwa. Ila ni dhambi kutoa mimba.
 
Niko 101% against abortion for any reason other than saving maisha ya mama. Hata kama mtoto ana miezi sita nikipata mimba nyingine nitazaa wapishane mwaka, next time nitajua tahadhari gani ya kuchukua.

Abortion is a cardinal sin, its barbaric, its unfair to the mother and the baby too. Bahati yangu mama alikuwa anaongea sana kuhusu abortion (kuna video ilikuwa inaitwa 'tafadhali usiniue' alituonyesha nikiwa std 4 nadhani. Inaelezea kisayansi what actually happens wakati wa utoaji mimba kwa njia mbali mbali. Inatisha haswaa).

Ukikosea unapaswa kujifunza kutoka kosa lako na kuhakikisha halijirudii. Face your consequences, that is maturity
 
Abortion for medical reasons its okay 100% but abortion kwa sababu nyingine haifai kabisa....yaani kati ya vitu ambavyo kwenye practice nliapa kuofanya ni abortion ...
 
Abortion haikubaliki for any reason. Ni kweli nimeshuhudia wanandoa kadhaa wakiabort na wengi walilazimishwa na waume zao. Hii ni dhambi na tunamnyima kiumbe haki yake ya kuishi. Cha msingi ukipata ujauzito usioutarajia zaa tu na kamwe usitoe mimba. Binafsi hata nikibeba ujauzito baada ya miezi 2 toka kujifungua lazima nitaulea ujauzito huo. Rai yangu kwa wababa wajitahidi kuzuia hii kitu kwani wao ndio supporter wakubwa wa hili.
 
ukweli ni huu hakuna mtu yeyote atakaekubali humu kuwa ameshatoa mimba.wengi watasema,kuna dada fulani nilimshauri au hiki kitu napinga{kwa sababu maybe ulitoa}baadae kuna majuto fulani,ambayo unajutia kwa nini ulifanya hivyo.hii mara nyingi huwa ni siri,hata kama ni ndani ya ndoa huwa vile vile ni siri.mambo haya yapo mitaani,mashuleni,maofisini,na majumbani.ni issue sensitive
 
Abortion iruhusiwe kisheria watu waache kuzaliana kama kuku hasa vijijini
 
Kuna rafki yangu aliwah fanya wakati yupo kidato cha tatu now ameolewa mwaka wa pili sasa hajapata mtoto....ni kitendo ambacho now ndo anajua hasara zake na kumuumiza sana moyo...
 
Haikubaliki na ni uuaji kabisa. Labda for medical reasons can be debated lakini ni kitendo cha kupingwa kwakweli.
 
sifagilii hii kitu kabisa..........nashukru sijawahi kushiriki directly or indirectly either kwa kumsupport mtu ktk hili.
 
Kiukweli from the heart naogopa hiki kitu na binafsi namuomba Mungu kisikae kinitokee,kwa sasa nina changamoto moja nina mtoto anakaribia kutimiza mwaka,hospitalini tulishauriwa kuwa kina mama tuliojifungua kwa operation tujitahidi angalau miaka mitatuu bila kushika mimba,back home mimi na mume wangu baada ya kusoma hapahapa jamii forum madhara ya njia za uzazi wa mpango tumeogopa kbs na hivo tunatumia natural methods.so far naogopa sana bt nikifikiria ikitokea nikapata nitafanyaje?lakini Mungu atanisaidia nitafanikiwa,plz ladies lets share
nb,natumia natural mbili na condom
 
Mungu atusamehe tu kwa kweli.....
binafsi sijawahi kufanya huu unyama kwangu ila najikuta nimeshiriki kwa namna moja au nyingine kwa watu wanaonizunguka....
 
Tofauti kati ya ujauzito wa mwezi na mimi ni mwili na mi-containers na mi-lorries ya dhambi, ila NAFSI IPO HAI, kwa hiyo kwa namna yeyote ni uuaji. Je?, ni bora uue mtu ili uonekane bora kwa watu (tena wengine ni wadhambi kuliko wewe)? au uonekane unapanga familia vizuri?? au kijana uonekane umejiheshimu? kwanza ukishaonekana then WHAAAT?????????????

Nasupport wanaolea mimba hata kama zimekataliwa, ni aheri kama mtu umeshindwa kumlea umtelekeleze kwenye ophanange centre kuliko KUMUUA kwa kisingizio cha kudhani utakuja kushindwa kumlea. na sisi WANAUME ndio tunahusika kwa kiwango kikubwa either kwa uzembe wa kutochukua tahadhari, kukataa mimba, kutoa fedha kwa kushawishiwa au kushawishi itolewe, 'tusipobadilika, we have our reward' ''LAZIMA TUKUBALI KUWAJIBIKA KWA MATENDO YETU''

Kama umewahi kushiriki utoaji mimba kwa namna yeyote, ni kitu kibaya sana Mbele ya Muumbaji, please take time kufunga na kuomba TOBA, Mungu ni wa rehema ataturehemu na kutuachilia tena.

Tized.
 
Back
Top Bottom