Fungu la Kumi: Ni lazima?

Kwa kweli ishu ya fungu la kumi huwa linanichanganya sana....huwa najiuliza kama kuna mtu unaona kabisa anahitaji msaada wa hali na mali...je unamuacha halafu unakwenda kumpa Gwajiboy hiyo hela ? matokea jamaa mhitaji anateseka na huku Gwajiboy anaongeza liHammer jingine!
 
Kwa cc watoto wa baba Paroko tuna matendo ya huruma
 
Nilivyoielewa michango ya wadau ni Walawi walipaswa kupewa kwa sabab wao hawafanyi shughul za uzalishaj isipokuwa wao wanahudumu ktk nyumba za ibada na ndio maana wanapaswa kupewa fungu ili waweze kujikimu.

Lkn kwa mazingira ya sasa taasis zetu za ibada zina miradi kibao inayoingiza mamilion ya shilingi na hata hao wanaohudumu ni waajiriwa na mishahara wanalipwa.

Na hapo ndipo unapokuja utofaut wa sabab zilizopelekea kuwekwa utaratibu wa kutoa fungu ili kuwezesha shughul ziendelee ktk nyumba za ibada na hali ya sasa ambayo imezifanya nyumba za ibada kuwa na ukwasi wa kutosha kuziwezesha kujihudumia zenyew kwa kuwalipa wanaohudumu.

Km ingewezekana kifungu hiki kinachoelezea kuhusu fungu kilipaswa kuangaliwa upya kutokana na mazingira ya sasa.
 
Kuna watu walikuwa wanafanya kazi tofauti na kilimo wala hawakutoa. Sababu haikuwahusu. Iliwahusu tu wale wenye ardhi. Na ilikuwa ni mwaka to mwaka sababu kilimo ndio kilivyo na sababu aliwapa ardhi then alitaka kinachotokana na ardhi tu. It was never money. And ilikuwa ni sheria.
 
Yes hapa ndo wanapokosea. Wameona ni easy money na waumini wao wanaamini kila wanachowaambia so it's easy to convince them. Huyu mlawi wa sana Ana mishahara Ana marupurupu Ana posho yaani Wako vzri kuliko waumini and still they want that LEVITE TITLE. [emoji849]. Zamani walikuwa wanatuhubiria kutoa kwa moyo but now wamepiga turn now ni 10% lazima lazima. Wanasahau ukifuata kibible ni zaidi hata ya huyo 10%. Yaani wameenda agano la kale wakakimbia na fungu la 10 tu. Maana now ndo mahubiri everywhere hata yale ya mahusiano binafsi na Mungu hayapo. Why 2005 kurudi nyuma hakukuwa na Haya mahubiri??
 
Mi nimeamua tu najisalia mwenyewe home, nasoma bible yangu naweka fungu la kumi kwenye kibubu.
Mwaka mzima si haba.simpi mtu yoyote huko kanisani au sijui pastor Masanja mkandamizaji, sijui pilipili wakafie mbere
 
Fungu la kumi kapanga Mungu mwenyewe. Inaitwa Zaka kwa Kiswahili na TITHE kwa kiingereza. Ukipitia Biblia yako ambayo cleary unaonekana huisomi bwana Joseph utaona haya yote yameandikwa kwa uwazi kabisa.
Kwanini Yesu hajazungumzia kabisa fungu la kumi??
 
Unajaribiwa kwa kidogo unachopewa ili uonyeshe uaminifu wako utakapopewa kikubwa imagine ukipewa 15,000,000 ukatakiwa utoe 1,500,000 hapo ndio ungeona maumivu hatari
 
Mi nimeamua tu najisalia mwenyewe home, nasoma bible yangu naweka fungu la kumi kwenye kibubu.
Mwaka mzima si haba.simpi mtu yoyote huko kanisani au sijui pastor Masanja mkandamizaji, sijui pilipili wakafie mbere
Duuuu!!!!inamaana hilo fungu mtoaji ndio mpokeaji???
 
Aliyefanya kazi ni nani ili ku justify hio kauli yako? Padri au mwamba?
 
Hakuna mahali kwenye Biblia pameonyesha ulazima wa ndoa kufungwa kanisani ila wachungaji wamelazimisha hilo.
Kitimoto kwenye agano la kale kimekstazwa, agano jipya kwakuwa hajazungumzwa nguruwe basi ni halali, ila fungu la kumi kwenye Malaki yaani agano la kale ndiko reference kuu ya patapeli makanisani huku agano jipya 10% imetupilia mbali.
Yesu zaka kataja mara 1 tu katika miaka yake yote 3 ya utumishi wake na hakuitaja kama msisitizo bali aligusia tu juu ya mada fulani.
Wengi wamepata laana kwa ujinga wao, wamemezeshwa kuwa usipotoa 10% unalaaniwa na kwakuwa mjinga hula ujinga wake ndipo anajilaani mwenyewe.
Ukweli ni kwamba hakuna laana unayoweza kuipata kwa kutokutoa fungu la 10 kanisani.
 
Mi nimeamua tu najisalia mwenyewe home, nasoma bible yangu naweka fungu la kumi kwenye kibubu.
Mwaka mzima si haba.simpi mtu yoyote huko kanisani au sijui pastor Masanja mkandamizaji, sijui pilipili wakafie mbere
Good hata Bible imesema itumie jinsi upendavyo hata kwa mvinyo
 
Dah!! Unakuta mtu anafanya kibarua cha 5k kwa siku na anapaswa kumpa fungu la kumi padri ambae kanisa linamhudumia kila kitu kanisa ambalo lina miradi ambayo inayoliingizia mamilion ya shiling kwa siku
Unyonyaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…