Kuna kisa kimoja kilinifanya niamin haya mafungu ya 10 ni wizi mtupu
Kuna mama alifiwa na mume wake, yule mama alishiba sana imani na akawa anatoa fungu la 10 kila akipata hela, ilifika hatua Hadi hela za mikopo anatoa fungu la 10, baada ya maisha kuwa magumu aliamua kuuuza hiace yake kwa 10M kwakua alimuamin sana mchungaji alimuomba mchungaji amtafutie mteja kwahiyo hata hyo 10M ilipitia kwa mchungaji bila huruma wala kujua shida za yule mama , mchungaji alimpelekea mama 9M tu anamwambia kuwa 1M ni fungu la 10 ameikata juu kwa juu
Maisha yakaendelea lakin mambo yakazidi kuwa magumu biashara zikawa zimedorora sana ikafika hatua yule mama akaenda kuchukua mkopo wa 100M kupitia nyumba yake ili alipe madeni na kuboresha biashara yake siku ya kwenda kuchukua mkopo akaenda na bint yake pamoja na mchungaji baada ya hela kuingizwa kwenye accnt ya mama, yule mchungaji akamwambia mama "Nipe changu"

chako kipi? Jamaa fungu la 10 ambayo itakua ni 10M mama akajikaza sana kutokana na ujinga wake wa kulewa kiimani kweli akamuingizia mchungaji 10M kweny accnt yake binafsi kama fungu la 10, mchungaji alivyokua Hana aibu akamuomba yule maza amuongezee 5M ili iwe 15M kuulizwa sababu? Akajibu Kuna gari anaipenda sana na hiyo ndo bei yake kwahyo akamuomba mama amuongezee 5M maza akampa jamaa akaenda kununua gari.
Yule mama Leo hii amefilisika lakin waliochangia kumfilisi kwa asilimia 50% ni Hawa watu wa dini hawa, hizi habari za fungu la 10 kama kweli unataka kutoa basi wapelekee mayatima na watu wasio jiweza kwa kuwanunulia mahitaji muhimu la sivyo utajikuta sadaka yako inatengeneza maisha ya watu binafsi tu kitu ambacho kinatafsirika ni utapeli