Fungu la Kumi: Ni lazima?

Fungu la Kumi: Ni lazima?

Key point kwenye haya maagizo ni neno "MAONGEO" wengi wanayaruka Haya but yamebeba maana nzima
 
Ukishapata hyo 15000 kabla ya kufanya bajeti zako hakikisha fungu la Kumi umeiweka pembeni kinyume na hapo utapiga bajeti zako za home ukija stuka huna kitu hata hilo fungu la kumi utakosa,fanya hesabu zako vizuri kama utoe fungu la kumi kwa kila wiki au kwa kilamwez
Fungu la kumi tafsiri yake ni asilimia kumi ya kile unacho earn

Dini imefanya ku neutralize hilo neno kuligeuza kua fungu la kumi ili watu wasijue kua dini ni biashara
 
Kwenye buku kumi na tano yako daily tenga Buku jero kwa ajili ya fungu la kumi.Kwa maana hiyo pesa halali iliyokwenye mamlaka yako kuitumia ni shilingi 13500.Matumizi yako jitahidi yatoshe humo.

Kila kitu unachopata kama ujira wako kwenye kazi zako ni cha kwake(Mungu) anachotaka utoe Asilimia kumi tu ya hicho umrudishie kingine utumie.Na kwa kumrudishia hicho kidogo anakubariki wewe na familia yako.Kipato kinaongezeka a majanga yanapita mbali na familia yako.
Expecting something in return is what we call business

Hapo kuna win win situation naiona kati ya Mungu na binadamu
 
Unaposema 15 haitoshi unamzungumziaje mtu ambaye kipato chake ni elfu tano kwa siku? Habari ya fungu la kumi si ya kanisa ni agizo straight and very plain kutoka kwa Mungu.Hapo awali kabla Yesu hajafa msalabani palikuwa na laana endapo mtu atakwepa kutoa fungu la kumi lakini baada ya Yesu kufa laana hiyo imeondolewa.

Kwa maana hiyo basi asiyetoa hana dhambi wala laana juu yake ila hana pia baraka zilizoahidiwa kwa mtoaji. Ukilinganisha kiwango cha baraka kwa atakayetoa na kiwango cha pesa unachotoa watu wenye hekima huwiwa kutoa zaidi ya asilimia kumi ya pato lao.

10% ya kipato chako haiwezi kumaliza matatizo yako lakini kiwango hicho hicho kidogo ukimtolea Mungu kama zaka basi atakubariki na kama ungekuwa ni mkulima ningesema ungekosa hata maghala ya kuhifadhi chakula chako chote kwa namna ambavyo kingekuwa kingi.
Kwa hiyo hilo fungu la kumi nawewe unaamini anachukua Mungu na sio mchungaji?
 
Nilivoanzaga kutoa fungus la kumi hata kwenye hicho kidogo ninachopata aisee mambo yalianza kunyooka na majanga mengi yakanitoka aisee, so na wewe uwe unatenga kidogo utaona mafanikio, sio fungu la kumi tu watoaji wengi ndio wamefanikiwa
Kama ulitoa fungu la kumi na mambo yakakunyookea fikiria kama ukitoa percent 10 ya mshahara wako ukanipa mimi ni kiasi gani mambo yako yatanyooka

Fikiria vizuri hapo maana Mungu ana njia nyingi za kukuinua na kuyafanya mambo yako yanyooke
 
Kwa mawazo haya utaendelea kuwa maskini, wewe ni mchoyo Wala na mimi nilikuwaga ka wewe naona kidogo siku nilivoanza kutoa nimeona mafanikio
Achana na huyo mchoyo unalionaje wazo langu?
 
Na vp km najitolea kwenye huduma km fidia ya kias ambacho napaswa kutoa
Hiyo moja kwa moja ni kikumi bila ubishi tena siyo kikumi bali kimia kwasababu unafanya huduma hiyo hadi ikamilike kwa asilimia mia. Maana asiye na kazi atatoaje kikumi?
 
Bila shaka hapew mungu,anayepewa ni mtumish wa mungu kupitia kanisa
Wanapewa Makuhani (Priests na Wasaidizi wa Hekaluni) hapewi Mungu Lawi.27:30.

Swali gumu:
Kwanini Kanisa leo halimpi Kuhani fungu la kumi badala yake linapelekwa Dayosisi na ambako pia linafanya kazi za ofisi badala ya kumtunza Kuhani.

More worse, sheria ya kikumi inasema Kuhani akiishapewa naye atoe humo kikumi awape Wajane hasa (siyo Wajane wenye uwezo), je, hili linafanyika leo? Tunatakiwa kutengeneza TAKUKURU wa Kanisa kuchunguza hili.

Kwahiyo watoaji wa kikumi wanakosea, wapokeaji wa kikumi wanakosea, watumiaji wa kikumi wanakosea, wooooote kabisa madegenyanga.
 
Kama ulitoa fungu la kumi na mambo yakakunyookea fikiria kama ukitoa percent 10 ya mshahara wako ukanipa mimi ni kiasi gani mambo yako yatanyooka

Fikiria vizuri hapo maana Mungu ana njia nyingi za kukuinua na kuyafanya mambo yako yanyooke
Agano la kale Mungu alizingatia kiwango.

Agano Jipya (ambalo ndilo tunaloliishi leo) Mungu haangalii kiwango bali MOYO ulio tayari kumtolea kiwango chochote.

Waraka wa Pili wa Paulo Mtume kwa Wakorintho 2Kor.9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu" Yaani Mungu humpenda yeye atoaye kwa MOYO mkunjufu siyo yeye atoaye kiwango kamili (kikumi)

Mafundisho mengi yaliyojaza Madhabahu nyingi yanatutia woga kuliishi Agano la Kale (kutoa kwa kanuni ya Agano la Kale yaani kiwango) badala ya Agano Jipya. Maana leo wapo wengi wenye moyo wa kutoa japo siyo kiwango halisi (kikumi) badala yake wanaacha kutoa kwa kuwa hazijatimia 10% wanarudi nazo nyumbani, umewahi kufikiri ni kiasi gani kinarudi nyumbani? Labda ni kiasi kingi kuliko 10% zilizotolewa na wale waliotimiza matakwa ya Agano la Kale. Adui anapenda sana Injili ya Fedha ili aweke mtego humo anase wengi waumini na Makuhani. Kanisa lijisahihishe katika hili kabla ya Dahari.

Mwenye masikio na asikie maneno haya Roho ayaambia Makanisa.

Walawi wasaidizi Hekaluni wakipeleka Madhabahuni kikumi.

1640332250476.png

Taswira kwa hisani ya google.
 
View attachment 2055453
Taswira kwa hisani ya google.
Na kuongezea hapo kWa levites Mungu amesema wazi Dhaka yote ni yao Sababu wao si kuwapa Urithi wa fungu lolote.
Sasa hawa wa sababu walioamua kujivika huu ukuhani ni kweli hawana urithi?? Now kama ukuhani ndo wameufanya kuwa ni uchungaji basi uchungaji ni ajira kama ajira nyingine. Wana mishahara kama watu wengine kwneye ajira. So why wajivike makabila ambayo sio yao.
 
Kama ulitoa fungu la kumi na mambo yakakunyookea fikiria kama ukitoa percent 10 ya mshahara wako ukanipa mimi ni kiasi gani mambo yako yatanyooka

Fikiria vizuri hapo maana Mungu ana njia nyingi za kukuinua na kuyafanya mambo yako yanyooke
Natoa fungu la kumi, nasaidia yoyote mwenye uhitaji urgently na sio wale wavivu wapenda kitonga aisee
 
Natoa fungu la kumi, nasaidia yoyote mwenye uhitaji urgently na sio wale wavivu wapenda kitonga aisee
Daaah unanikatisha tamaa naona kama nabaguliwa vile

Kwani unapotoa hilo fungu la kumi, huyo unayemtolea anakua hajiwezi?
 
Kutokutoa zaka sio dhambi na wala sio kigezo cha kukuzuia kwenda mbinguni.Kama unaona miyeyusho usitoe, buku jero yako kunywa maji.Lakini mambo yako yatakapokwama usiende mbele za Mungu na kuanza kulia WHY LORD?WHY? jibu tayari unalo.
Na hata yakikwama inawezekana mungu ananijaribu km alivyomjaribu Ayubu na wengineo sidhan km kutoa hilo fungu ndio dhamana ya kutopatwa na majaribu
 
Sasa wapi Paul alikwambia umpe fungu la 10 mchungaji???? Paul Alisema toa kwa moyo na si kwa sheria/shuruti. 10% ilikuwa chini ya sheria. Kama watoa kwa moyo then Moyo hauna asilimia basi una kile UNACHOWEZA KUTOA.
Hili nalo nilikuwa silijui kuwa kanun ya fungu ilianzia kwa paulo
 
Sasa wapi Paul alikwambia umpe fungu la 10 mchungaji???? Paul Alisema toa kwa moyo na si kwa sheria/shuruti. 10% ilikuwa chini ya sheria. Kama watoa kwa moyo then Moyo hauna asilimia basi una kile UNACHOWEZA KUTOA.
Hili nalo nilikuwa silijui kuwa kanun ya fungu ilianzia kwa paulo
 
Daaah unanikatisha tamaa naona kama nabaguliwa vile

Kwani unapotoa hilo fungu la kumi, huyo unayemtolea anakua hajiwezi?
Wa kwetu hapa anatembelea vi8 anazo zaid ya kumi hilo jumba analoish balaa anawasaidiz binafs kibao na anatusisitiza ukitoa fungu dai risit kwa lugha nzuri jamaa anajiweza
 
Hili nalo nilikuwa silijui kuwa kanun ya fungu ilianzia kwa paulo
Ndiyo maana nilichangia hapa kuwa tunafundishwa na kuhimizwa kuishi Agano la Kale la TORATI ya matoleo badala ya Agano Jipya. TORATI imekamilishwa kwenye Agano Jipya kwa UPENDO, na UPENDO huo huo ndiyo Mungu anasisitiza kwa kinywa cha Mtume Paulo kwamba TOENI KWA MOYO MKUNJUFU (Neno moyo mkunjufu maana yake ni kwa upendo na siyo Torati ya Manabii).

Hivyo basi Manabii walitufundisha kutoa kwa sheria (TORATI) Mitume wanatufundisha kutoa kwa moyo mkunjufu (UPENDO). Ukiisha kuwa na upendo moyoni mwako kwa Mungu wako basi kumbe huwezi kumuibia stahili yake kama Malaki anavyotufundisha kwenye sura ya 3:7-12. Tafsiri yake ni kuwa kwenye Agano Jipya moyo mkunjufu (Upendo) tunaofundishwa unaweza kutuongoza kutoa hata zaidi ya kikumi (siyo lazima pungufu ya kikumi au kikumi kamili).
 
Back
Top Bottom