(Fungu la 10) mchungaji agoma kufungisha ndoa

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,024
2,000
Ilikuwa ni kama filamu ya kusisimua pale maharusi, Paul Lugendo na Ester Kapilimka, wakazi wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam walipobaki vinywa wazi kufuatia mchungaji wao, Alphonce Lubalate kugoma kuwafungisha ndoa kwa madai kuwa bwanaharusi hakutoa fungu la kumi.

Tukio hilo ambalo linaweza kuingizwa kwenye kumbukumbu mbaya za wanandoa, lilijiri Julai 16, mwaka huu ndani ya Kanisa la Kilokole la Haven of Christian, Ubungo ya Kibangu, Dar.

MWANZO WA UTUNGU
Awali ilidaiwa kuwa, maharusi hao walifika nje ya kanisa hilo wakiwa wamechelewa kwa saa tatu nje ya muda waliowekewa na Mchungaji Lubalate.

Inadaiwa kuwa, ndoa hiyo tukufu ilikuwa ifungwe saa tisa alasiri, lakini kujiremba kwa maharusi hao, ukijumlisha na usafiri wa Dar pamoja na foleni, walijikuta wakiwasili kanisani hapo saa 11:30, nusu saa kabla ya muda wa kufungisha ndoa wa serikali kumalizika.

Ndipo Mchungaji Lubalate akaweka ngumu akidai eti anaheshimu mamlaka na kama maharusi hao watataka warudi kesho yake, Julai 17, mwaka huu saa sita alasiri waunganishwe huku akiwa amesahau kuwa, matarumbeta na pilau vilikuwa vikiwasubiri waalikwa.

BWANA HARUSI AFUNGUKA
Akiweka wazi mkasa mzima, Bwanaharusi Lugendo alisema:
"Nimesikitika sana, inaonekana kama mchungaji hakupenda nifunge ndoa hii kwani toka mwanzo alikuwa akiweka vikwazo mbalimbali visivyo na msingi. Kuna wakati alisisitiza kuwa, eti hatanifungisha ndoa kwa sababu sitoi fungu la kumi."

KUHUSU SIKU YA TUKIO
"Siku ya harusi, nilimtuma mtu akachukue gari la kutubeba maharusi mjini kwa dada mmoja. Alipofika, akaambiwa hawezi kupewa mpaka niwepo mimi mwenyewe.

"Ilibidi nitoke saluni niende mjini kufuata gari. Wakati tunarudi, kufika Ubungo tulikuta foleni kubwa sana na baadhi ya watu waliokuwa kanisani, akiwemo mchungaji tuliwaambia kuhusu foleni hiyo.

"Mwisho wa yote, nilimwambia msimamizi wangu, tushuke tuchukue Bajaj mpaka Riverside, pale tuchukue taksi, halafu gari na dereva tukawaambia wamfuate bibiharusi saluni, Mwenge.

"Tulifika kanisani saa kumi na moja, sambamba na bibi harusi, tukamkuta mchungaji yupo ofisini kwake, akatuuliza mmefika siyo, tukamjibu ndiyo, akasema twendeni kanisani.

"Tulipofika kanisani, akaanza kuhubiri sisi maharusi tukiwa mbele. Lakini mahubiri yake yalinipa wasiwasi, kwani si yale ya ndoa kama nilivyozea.

"Alianza kusema watu tunatakiwa kutii mamlaka iliyopo, hata Yesu mwenyewe alitii. Akasema sisi tumechelewa kufika kanisani, kwa hiyo yeye hawezi kufungisha ndoa maana anatii mamlaka zilizopo.

"Baada ya hapo, akaomba kwa ajili ya kumshukuru Mungu ili amalize na kutoka, watu hawakumuitikia, akarudia mara mbili, mwisho akajiitikia mwenyewe," alisema bwanaharusi huyo.

Aliendelea kuweka bayana kwamba, baada ya hapo, baadhi ya watu waliwataka maharusi kubaki kanisani ili wao wakamuombe mchungaji arudi kufungisha ndoa hiyo kwa sababu tayari gharama za ukumbi na mambo mengine vilishafanyika.
Bwanaharusi anasema pamoja na kuombwa, hakubadili msimamo.

KILICHOTOKEA SASA
Bwanaharusi huyo akasema kuwa, ilibidi yeye, mkewe mtarajiwa, ndugu na waalikwa waende ukumbini kusherehekea lakini hakukuwa na kushikana mikono kwa maharusi kwa sababu hawakuwa wameunganishwa kisheria.

Akasema: "Achilia mbali kushikana mikono, hata keki sikutakiwa kumlisha mke wangu maana hatujafunga ndoa."
Lakini akasema kuwa, toka mchungaji alipogoma kufungisha ndoa hiyo, kukawa na mawasiliano na mchungaji mwingine wa kanisa moja la kiroho lililopo Kimara ambaye alikubali kuwafungisha pingu wawili hao.

Bwanaharusi akasema: "Tulifanya mawasiliano na mchungaji mwingine, yupo Kimara, akakubali kutufungisha ndoa, hivyo tulitoka ukumbini saa saba na nusu, saa nane usiku akatufungisha ndoa kisha tukarudi nyumbani."

MASIKITIKO MAKUBWA
Bwanaharusi alisema kuwa, ana masikitiko makubwa, hajui ni kwa nini Mtumishi huyo wa Mungu alimtendea vile, kwani alichobaini, visingizio vilikuwa vingi, fungu la kumi likiwemo ndani.

KAULI YA MCHUNGAJI
Kwa upande wake, Mchungaji Lubalate alisema alishindwa kuwafungisha pingu za maisha wawili hao kwa sababu muda ulikuwa umekwenda.

"Nisingeweza kufungisha ndoa, muda ulikwenda. Mimi kama Mtumishi wa Mungu natakiwa kutii mamlaka. Saa kumi na mbili ndiyo mwisho wa kufungisha ndoa kiserikali."kutokana na maelezo ya bwana harusi nadhani huyu mchungaji kapokonywa tonge mdomoni alimpenda bibie
 
Babuu blessed

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
1,371
1,250
Hapa kuna utata katika maandalz ya ihi ndoa kwa sababu na inawezekana kuna bifu la chini chini kati ya bwana harus na pasta wake,kwa sababu bwana harus akuwa amemwalika pasta wake katka tafrija yaani akumpa invtation card,na aliyefungsha ndoa usiku wa manane ni mchungaj wa upande wa bi harusi kwa sababu bi harusi alitoka kanisa lingne.kuhusu mchungaj kupokonywa tonge siwez kubal au kukataa kwa sababu uyu pastor alishatimua mke wake kwa sababu alimpeleka mtoto wao kuchezwa ngoma uko uzaramoni alipo balehe.
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,541
2,000
Ilikuwa ni kama filamu ya kusisimua pale maharusi, Paul Lugendo na Ester Kapilimka, wakazi wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam walipobaki vinywa wazi kufuatia mchungaji wao, Alphonce Lubalate kugoma kuwafungisha ndoa kwa madai kuwa bwanaharusi hakutoa fungu la kumi.

Tukio hilo ambalo linaweza kuingizwa kwenye kumbukumbu mbaya za wanandoa, lilijiri Julai 16, mwaka huu ndani ya Kanisa la Kilokole la Haven of Christian, Ubungo ya Kibangu, Dar.

MWANZO WA UTUNGU
Awali ilidaiwa kuwa, maharusi hao walifika nje ya kanisa hilo wakiwa wamechelewa kwa saa tatu nje ya muda waliowekewa na Mchungaji Lubalate.

Inadaiwa kuwa, ndoa hiyo tukufu ilikuwa ifungwe saa tisa alasiri, lakini kujiremba kwa maharusi hao, ukijumlisha na usafiri wa Dar pamoja na foleni, walijikuta wakiwasili kanisani hapo saa 11:30, nusu saa kabla ya muda wa kufungisha ndoa wa serikali kumalizika.

Ndipo Mchungaji Lubalate akaweka ngumu akidai eti anaheshimu mamlaka na kama maharusi hao watataka warudi kesho yake, Julai 17, mwaka huu saa sita alasiri waunganishwe huku akiwa amesahau kuwa, matarumbeta na pilau vilikuwa vikiwasubiri waalikwa.

BWANA HARUSI AFUNGUKA
Akiweka wazi mkasa mzima, Bwanaharusi Lugendo alisema:
"Nimesikitika sana, inaonekana kama mchungaji hakupenda nifunge ndoa hii kwani toka mwanzo alikuwa akiweka vikwazo mbalimbali visivyo na msingi. Kuna wakati alisisitiza kuwa, eti hatanifungisha ndoa kwa sababu sitoi fungu la kumi."

KUHUSU SIKU YA TUKIO
"Siku ya harusi, nilimtuma mtu akachukue gari la kutubeba maharusi mjini kwa dada mmoja. Alipofika, akaambiwa hawezi kupewa mpaka niwepo mimi mwenyewe.

"Ilibidi nitoke saluni niende mjini kufuata gari. Wakati tunarudi, kufika Ubungo tulikuta foleni kubwa sana na baadhi ya watu waliokuwa kanisani, akiwemo mchungaji tuliwaambia kuhusu foleni hiyo.

"Mwisho wa yote, nilimwambia msimamizi wangu, tushuke tuchukue Bajaj mpaka Riverside, pale tuchukue taksi, halafu gari na dereva tukawaambia wamfuate bibiharusi saluni, Mwenge.

"Tulifika kanisani saa kumi na moja, sambamba na bibi harusi, tukamkuta mchungaji yupo ofisini kwake, akatuuliza mmefika siyo, tukamjibu ndiyo, akasema twendeni kanisani.

"Tulipofika kanisani, akaanza kuhubiri sisi maharusi tukiwa mbele. Lakini mahubiri yake yalinipa wasiwasi, kwani si yale ya ndoa kama nilivyozea.

"Alianza kusema watu tunatakiwa kutii mamlaka iliyopo, hata Yesu mwenyewe alitii. Akasema sisi tumechelewa kufika kanisani, kwa hiyo yeye hawezi kufungisha ndoa maana anatii mamlaka zilizopo.

"Baada ya hapo, akaomba kwa ajili ya kumshukuru Mungu ili amalize na kutoka, watu hawakumuitikia, akarudia mara mbili, mwisho akajiitikia mwenyewe," alisema bwanaharusi huyo.

Aliendelea kuweka bayana kwamba, baada ya hapo, baadhi ya watu waliwataka maharusi kubaki kanisani ili wao wakamuombe mchungaji arudi kufungisha ndoa hiyo kwa sababu tayari gharama za ukumbi na mambo mengine vilishafanyika.
Bwanaharusi anasema pamoja na kuombwa, hakubadili msimamo.

KILICHOTOKEA SASA
Bwanaharusi huyo akasema kuwa, ilibidi yeye, mkewe mtarajiwa, ndugu na waalikwa waende ukumbini kusherehekea lakini hakukuwa na kushikana mikono kwa maharusi kwa sababu hawakuwa wameunganishwa kisheria.

Akasema: "Achilia mbali kushikana mikono, hata keki sikutakiwa kumlisha mke wangu maana hatujafunga ndoa."
Lakini akasema kuwa, toka mchungaji alipogoma kufungisha ndoa hiyo, kukawa na mawasiliano na mchungaji mwingine wa kanisa moja la kiroho lililopo Kimara ambaye alikubali kuwafungisha pingu wawili hao.

Bwanaharusi akasema: "Tulifanya mawasiliano na mchungaji mwingine, yupo Kimara, akakubali kutufungisha ndoa, hivyo tulitoka ukumbini saa saba na nusu, saa nane usiku akatufungisha ndoa kisha tukarudi nyumbani."

MASIKITIKO MAKUBWA
Bwanaharusi alisema kuwa, ana masikitiko makubwa, hajui ni kwa nini Mtumishi huyo wa Mungu alimtendea vile, kwani alichobaini, visingizio vilikuwa vingi, fungu la kumi likiwemo ndani.

KAULI YA MCHUNGAJI
Kwa upande wake, Mchungaji Lubalate alisema alishindwa kuwafungisha pingu za maisha wawili hao kwa sababu muda ulikuwa umekwenda.

"Nisingeweza kufungisha ndoa, muda ulikwenda. Mimi kama Mtumishi wa Mungu natakiwa kutii mamlaka. Saa kumi na mbili ndiyo mwisho wa kufungisha ndoa kiserikali."kutokana na maelezo ya bwana harusi nadhani huyu mchungaji kapokonywa tonge mdomoni alimpenda bibie

binafsi namauunga mkono asilimia 100 mchunghaji lazima ifike uheshimu mamlaka mtu huyu anaekuja harusini saa kuminamoja
ofisini anaingia saa mojananusu wakati waemandikiwa saa mbili sasa kama anaheshimu kazi kwanini asimheshimu MUNGU zaidi aliempa hiyo kazi na mke tena ningekuwa mimi ningemwambia apeleke ujinga wake swala la fungu la kumi si ombi lazima akasome maandiko na nina uhakika ameongelea sababu amekataliwa kufungishwa kwa ujinga wake ..naeleza hili nikimaanisha nimeona harusi nyingi sana wachungaji wanaogopa kuacha kufungisha wakiogopa aibu ...hasa AZANIA KUNA WANANDOA KILA SIKU WANAINGIA SAA KUMINAMOJA NA NUSU NA MCHUNGAJI ASHAANZA MAANDIKO
BINAFSI NAmsaidia mkuu ukijitayarisha kuoa unakuwa umejiandaa sio umechukua kichujio pale tandale unataka kuchuja maziwa la hasha huyo ni mkeo wa ndoa na lazima unamwelekeza kabisa saa kadhaa umefika kama wewe ndio kioo unatia aibu mkeo atakutii kivipi ndan ya ndoa ifike wakati mjiulize wanandoa mnachokifanya nje hawa wanawake wanaa kili kinakuja kukugeuka ndna ya ndoa
Kila la k heri na ndoa yako
 
Big One

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
758
195
ndoa si imetanganzwa mara 3 kanisan sasa si angetoa pingamizi hyo alikuwa na lake jambo
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,334
2,000
Jamani sa fungu la kumi linahusiana na nini hapo?halafuuu makamisa mengi ya kiroho yapo kibiashara biashara tuu!aghhhhhhhhhh!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom