watu kibao
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 466
- 1,645
Vijana wetu kuna muda mnajishusha tunawapa chance kuwaamini lakini mambo wanayofanya yanatukatisha tamaa ya kuendelea kuwaamini.
Gari ilikuwa na matatizo, nikaenda mtaani kutafuta fundi aje kuliangalia.
Gari iligoma kuwaka kwajili ya matengenezo tukaona mafuta hayatoshi kuliwasha.
Nikampa fundi elfu 10 aende kununua mafuta akate humo humo hela ya usafiri.
Kituo cha mafuta ukienda na bajaji unarudi ndani ya dakika 15, na nauli ya bajaji kwenda na kurudi ni kama buku jero,
Fundi kakaa huko zaidi ya karibia lisaa zima karudi na mafuta kwenye kigaloni cheupe, sikuweza kuona mafuta.
kaweka mafuta kwenye gari, muda wa kuwasha gari inapiga tu starter, ukiachia funguo inazima.
Fundi ametafuta tatizo kashindwa, akaondoka.
Nimeleta fundi mwengine kuangalia tatizo akatoa ule mpira wa kupeleka mafuta kwenye engine.
Mafuta ni meupe kama yamechanganyika na mapovu na maji.
Tamaa hizi ! nimeambiwa inabidi niende kusafisha tenki zima, dah !!
Napoteza muda na pesa kwenda garage kwajili ya tamaa za mtu aliebana elfu 10 kutafuta mafuta ya mchongo.