Unaujua uchungu wa kuchukuliwa mume wewe............
Hizi ni mbinu za akina KASEJA mashambulizi yakizidi..unajivunja kiaina.... hapo kapunguza mashambulizi....mpaka wafike nyumbanihivi kuna watu wanaoweza kugawa kisago hadi mtu akapoteza fahamu? wapi wanatoa mafunzo haya?
Mimi siku zote huwa najitaidi sana kumfanya mtu wangu asitoke njee kwa kuhakikisha majukumu yangu kama mwanaume nayatimiza kila idara. Hata akitoka nikajua sitompiga, tachunguza madhaifu yangu kwanza. Nitaongea naye, tufike muhafaka yaishe siku hiyo hiyo. ile dhana ya mwanaume ndio mwenye haki ya kwenda nyumba ya kando, mwanamke ikitokea imepitwa na wakati. kabla ya kutoa hukumu, jiulize wewe upo vyema. Tutazungumza mara ya kwanza, ya pili ya tatu. Asipo nisikia, namwambia mama kwa heri ya kuonana. Si dhani kama ni vyema kumpiga alafu usiku kitandani unamwambia sogea huku.
Hata kama kamfumania, hakutakiwa kumpiga, TGNP na TAMWA waingilie kati, unyanyasaji wa kijinsia huu.
Anaweza kufa kwa kipigo hiki, nani anajua kama hapata madhara makubwa ya ndani?
Na watu humu wanachangia mada kwa ushabiki...huyu angekuwa, binti yako, dada yako au mama yako ungekubali apigwe hata kama ana kosa gani?????
Muwe mnajaribu kuvaa uhusika...kosa amefanya lakini hiyo adhabu si sahihi...hakuna binadamu anastahili kupigwa...siku hizi hata wanyama kwenye nchi za wenzetu wanalindwa. Na huku kwetu wanafunzi tu wameacha kupigwa...upori pori at work
Huyu angekuwa dada yangu huyo mwanaume ndio angejua kama kuoa si kununua...tungemfunza adabu nyumba nzima.Lol Kama wameshindwana amrudishe kwao
Amseme tu kisha amsamehe,na kama hawezi kufanya hivyo amuache!!Kwani angefanyweje? @ mimi49
Duh! Anaukika kama jamaa alikua hatambui huyo ke ni Mke wa watu?
Adabu na fundisho zuri lingepatikana kwa kuwahukumu wote!!
Mmoja tu, yule wa kwanza maana baada ya hapo huwezi kuendelea kukaa na kicheche.Kama mume/mke ni mzinzi mzoefu utagombana na wanaume/wanawake wangapi?!