Fumanizi hili Guest house Iringa

Fumanizi hili Guest house Iringa

Namuunga mkono huyo jamaa kwa namna alivyoliona kosa
Lakini hakustahili kumpiga mkewe!

Amelijudge in a right way hata nilivosoma ile sababu ya kumuachia yule mwanaume...

niliona ni sawa....ila kumpiga hapana......
 
Mapenzi ni hiari, kama una mke mzinzi na huwezi vumilia mwache.

Kumbuka, katika sheria si kila halali ni haki. Hao walioua magoni wao na kuachiwa inawezekama walitumia kipnegele cha 'temporal Insanity', lakini je kuua mtu sababu ya K moja tu ni haki?


Malengo ya taasisi yeyote kama ni kutetea haki ya binadamu, basi ina wajibu wa kutetea haki ya binadamu huyo endapo itapokonywa hata kama ana tabia ya aina yeyote.

Kwa hiyo sababu tu mwanamke ni mzinzi apigwe hata akifa poa? Kisa? To feed men's ego?Absurdity of Weak Men!

Ndg yangu Kongosho, kwani hao TGNP na TAMWA walimutuma huyo dada akafanye uzinzi asb yote hii. Mbona mnazibambikia hizi taasisi majukumu mengine ambayo yako nje ama mbali na majukumu yao. Siiungi mkono sana mwanandoa yeyote kumpiga mwenzake lakini lipokuja swala mahususi kama hilo lolote linaweza kutokea ikiwemo kupigwa na hata kufikia kupoteza maisha/uhai wa mhusika.

Wapo watu waliwaua wagoni wao, kisheria ni kosa kujichukulia sheria mkononi, lakini mahakama ziliwaachia huru kutokana na aina ya tukio lilivyotokea na huyo mhusika alivyorespond kwalo, hebu mara nyingi tujaribu kuuvaa uhusika, imagine kama ungekuwa wewe ungefanya nini.

Eti TGNP, TAMWA, nk, kumbe basi watu wanaweza kuamua kufanya upuuzi ndani ya ndoa zao kwa kujua ama kutambua kuwa hizo taasisi zipo kwa ajili ya yao na kutetea upuuzi wao. Nitazishangaa hizo taasisi za namna hiyo ambazo zitaacha mambo ya msingi kama ya mirathi ya wajane, utumikishwaji wa watoto wadogo nk, na kwenda kushughulikia mambo ya kujitakia kama hayo.
 
Sasa kuna haja gani ya kumpiga kwa kumfumania mtu na unamwacha? Kwa nini asimwache tu?

Ego?

Kupiga ni kutoa adhabu...kutoa talaka nayo ni adhabu...wala sio ego.

Hapa kitu cha muhimu ni kwa wanaume na wanawake waliopo kwenye ndoa waache zinaa basi..

Ukiacha zinaa haya mengine yote yatukuayo baada hayawezi pata nafasi...
 
Uzinzi ni A, kuchukua sheria mkononi ni B
Havichangamani! Kama ameumia sana, angempa talaka tu maana hata kisheria inaruhusiwa kumwacha kwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa.

Mwanamme anayepiga mkewe kwa sababu yeyote ni 'WEAK', period!

Mimi ninachojua hakuna mwanaume ama mwanamke yeyote anayepanga kwenda kumpiga mwenzake, hili jambo mara nyingi hutokea automatically kutokana na sababu za jambo husika, ambazo mhusika kwa namna moja ama nyingine hushindwa kukontrol hasira zake. Wapo wanawake ambao katika ugoni huwapiga wanaume wao tena hadharani na jinsi ya kitendo chenyewe pindi unapokamatwa hugeuka kuwa aibu hivyo pamoja na ubabe wa wanaume wengi hakika hapo hujikuta wakinywea/ kuwa wapole.

Bado napingana na dhana yako ya mwanzo kuona kuwa ni haki kwa TGNP ama TAMWA kuingilia mambo kama hayo. Aidha pia ukisema kuwa kwa vile sheria inaruhusu kumwaacha mtu mzinzi, je utaachana na wangapi if it hapen for more than once in your marriage. Makosa mengine lazima tukubali kupeana adhabu za papo kwa papo na katika kufanya hivyo nadhani itasidia kusonga mbele kimaisha.

Katika kuanza kufanya legal procedures za kumpa talaka huyo mwanamke ambaye eti umenshika ugoni, inaweza kuchukuwa muda mrefu, na ujue pia huyo mtu bado ni mkeo ama mume bado maana mnasubiri sheria iwatenganishe, kumbe basi kihalali mnapaswa kuendelea kuishi pamoja na kutenda pamoja at the time mnasubiri kesi yenu kuweza kuamliwa na mahakama or whatever, mnaweza kujikuta kwa muda huo hadi mmerudiana na hadi kwenda kuomba kufuta kesi mahakani, kumbe ni bora kama mngeweza kuazibiana kama kuna kuendelea na maisha mtajua kama sivyo mtajua maana ukweli kosa liko wazi.
 
"Ukiona nimenyamaza ujue nimekubali wewe niangusage tu sambi sote sakwako" ndimgaya sida
 
Duh! Anaukika kama jamaa alikua hatambui huyo ke ni Mke wa watu?
Adabu na fundisho zuri lingepatikana kwa kuwahukumu wote!!

Usikute njemba ilikuwa na viazi a.k.a baunsa. Kwa hiyo mume akafyata na kusingizia hana hatia.
 
Sijui, but ikitokea nitajua la kufanya hapo hapo.

Sidhani kama utaweza

Juzi nilikuwa eneo moja hapa jijini Mwanza linaitwa Kayenze,ilitokea kadhia ya namna hii,yule jamaa aliogopa kupambana na mwanaume aliyemfumania akataka kuhamishia hasira zake kwa mkewe

Mkewe alijitahidi kumzidi nguvu lakini alishindwa alipewa kipigo hadi wasamaria wema waliingilia kati,hadi naondoka eneo hilo kurudi mjini yule mwanamke aliyefumaniwa alikuwa amezirai kwa kipigo

Hawa watu wa aina hii ni kujiepusha kuingia nao kwenye mahusiano hasa kwenu wanawake
Ni hatari!
 
TGNP na TAMWA ndio walimtolea mahari huyo bwana?...acha mtu apewe mkong'oto kidogo maana hakuna taasisi inayoshughulikia mafumanizi

mfumo dume, ampige ili iweje, unafikiri inasaidia?bora wakae chini waongee, je kama hamridhishi.
tena huyu lazima ashitakiwe,mbona wanaume wanafumaniwa na kusamehewa
 
Kupiga ni kutoa adhabu...wala sio ego.

Nina mashaka na hili
Kupiga kunatokana na udhaifu wa kijinga unaoitwa wivu,huu ni udhaifu hatari sana,watu wanawadhru binadamu wenzao kisa huu udhaifu wa hovyo!
kutoa talaka nayo ni adhabu...
Sawa!!!!
Hapa kitu cha muhimu ni kwa wanaume na wanawake waliopo kwenye ndoa waache zinaa basi..
Wasiache kwakuwa kuna kupigwa......
Waache kwakuwa zinaa ni kitendo kinachofanywa na wanyama na sio binadamu!!!

Ukiacha zinaa haya mengine yote yatukuayo baada hayawezi pata nafasi...
Inawezekana!!!!!!!!!!!!
 
mfumo dume, ampige ili iweje, unafikiri inasaidia?bora wakae chini waongee, je kama hamridhishi.
tena huyu lazima ashitakiwe,mbona wanaume wanafumaniwa na kusamehewa

Wewe unadhani huyo mwanaume alipanga kumpiga mkewe?

Hapo waongee nini sasa na kama ni maji ndio yashamwagika...

Huko kutoridhishwa ndio uamue kwenda kuzini? Kwa nini usingeliongea na mumeo?

Suala la wanaume wengine kufumaniwa na kusamehewa linahusiana vipi na hili tukio?
 
watu8@ kama akimuua je?angemuuliza taratibu kwanini umefanya hivi na tatizo liko wapi?kama hamtaki basi anamwacha< mbona wanaume wanafu,aniwa sana?
Wewe unadhani huyo mwanaume alipanga kumpiga mkewe?

Hapo waongee nini sasa na kama ni maji ndio yashamwagika...

Huko kutoridhishwa ndio uamue kwenda kuzini? Kwa nini usingeliongea na mumeo?

Suala la wanaume wengine kufumaniwa na kusamehewa linahusiana vipi na hili tukio?
 
Back
Top Bottom