FULL TIME: Simba Vs TP Mazembe(0-1) | Simba Day | Mkapa Stadium

Mimi ni nani nisikushukuru kwa Kuniona na Kunitaja (Kuniita) Kwako hivi Ndugu? Tupo wengi na huenda wako wanaonizidi ila yawezekana kuna Thamani Tukuka iliyopo ndani yangu na umeitambua na unaiheshimu pia. Niseme tu Asante Kwako na kwa wale Mashabiki zangu.

Kuhusu tukio zima la leo nadhani la Muhimu kwa Wana Simba SC wote ni hasa Kufurahi na Kusheherekea zaidi hata kama ikitokea tukafungwa na Wageni Tou Puisant ( TP ) Mazembe leo.

Na kizuri kingine ni kwamba tunacheza na Bingwa wa CL mara Tano, moja ya Klabu Tajiri Afrika lakini na Timu inayojua, inayojitambua na iliyotuacha mbali mno Simba SC kwa Maendeleo, Mfumo na Mikakati ya Kimchezo.

Nitashangaa mno leo nikiona au nikisikia mwana Simba SC ananuna na Kukasirika kama ikitokea tukafungwa kwani Jukumu letu ( Mama ) leo ni Kukiangalia Kikosi chetu, Maingizo mapya na Muunganiko wao ( their Chemistry ) kama imeshakubali au inaelekea Kukubali.

Wana Simba wote tufurahi na tutambe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…