FT: AFL: TP Mazembe 1-0 Esperence De Tunis | Stadium: Benjamín Mkapa | 22.10.2023

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,375
105,200
Leo tena Tanzania inabahatika kushuhudia mechi bora yenye viwango vya juu inayopigwa katika dimba la Benjamín Mkapa huku Tp Mazembe akiwa mwenyeji.

Hii ni mechi ya tatu ya mashindano haya mapya tangu yazinduliwe Tanzania na Club kubwa Africa Mashariki na kati.

Ikumbukwe kuwa Tp Mazembe wameomba uwanja wa Benjamín Mkapa utumike kama uwanja wao wa nyumbani baada ya kutokea sintofahamu kati ya Club yao na serikali huko Congo.

Mechi inatazamiwa kuwa ya mvuto na ushindani dakika zote ambapo kwa statistics za matokeo kati ya Tp Mazembe na Esperence De Tunis inaonesha mbabe ni Esperence De Tunis.

Wamekutana mara mbili, mechi moja ambayo Tp Mazembe alikuwa nyumbani iliisha kwa sare.

Mechi ya mwisho ya marudiano Tp Mazembe alikufa goli moja.

Je leo Tp Mazembe atashinda ili asawazishe rekodi katika h2h?

Mechi ni saa 18:00

Na usisahau kuwa mechi hii pale kwa Mkapa hakuna kiingilio yani ni bureeeeee.
 
Vikosi vya timu zote mbili

Mwenyeji Tp Mazembe
Screenshot_20231022-173545.png



Mgeni Esperence De Tunis
Screenshot_20231022-173606.png
 
Back
Top Bottom