FULL TEXT: HOTUBA ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Lissu, Katiba na Sheria, yaibua makubwa bungeni

Chadema hawajui nini wanataka. Kutwa wako kwenye maandamano badala ya kuhamasishana kushiriki kwenye uundwaji wa mabaraza ya katiba...

Kudai katiba mpya ilikua kisingizio cha kushindwa uchaguzi wa 2010. Kwao njia nzuri ya kuelezea mashabiki wao kwa nini walishindwa haikua kuwaambia kuwa hawa kubaliki kama walivyo dhani bali kwamba katiba iliyopo ilikua inapendelea CCM. Huwezi kudai kitu kisha ukikubaliwa ukikatae. Wao hawakutegemea serikali ingekubali mchakato wa katiba mpya.
 
Chadema hawajui nini wanataka. Kutwa wako kwenye maandamano badala ya kuhamasishana kushiriki kwenye uundwaji wa mabaraza ya katiba...

Mi nadhani WEWE akili zako Ni mbovu !!!!!! Full stop. Maana hata vitu vizuri unatoa ushuhuda WA kijinga mpaka unakatisha tamaa kama zimekamilika kichwani
 
cjaona mahali ikizungumzia mahakama, kesi kurundikana, mazingira mabovu ya utendaji kazi wa waandaaji wa haki ya mtu kupatikana na mengine. au yapo kwenye page zilizosalia?
 
Wapi mahala ambapo hotuba ya lisu imeonesha kipao mbele cha kushughurikia changamoto ziliopo kwenye wizara ya katiba na sheria,zaid anlalamika kama mtoto mdogo.
Kwa nini tunaangalia mambo kwa wepesi kiasi hiki?
Hiki ni chama pinzani ambacho dhamira yake ni kuanika mapungufu ya chama tawala ili Wananchi wakichague uchaguzi ukifika na kazi hiyo wanaifanya vizuri.
Umesoma mawasiliano ya CCM kuhusu mchakato wa katiba,huoni kuwa hili ni jambo hatari?
Umesoma matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi,mpaka kupangiana vyakula kwa watakaokuwa na bahati mbaya ya kupta ukimwi.
Let us approach these things with an open mind.
Ni kweli kuna wakati wanakera lakini katika hizi hotuba za mawaziri vivuli kuna mambo amabao inabidi tuyapokee na tuyafanyie kazi.
 
Kuhusu Kujitoa Tume ya katiba Mpya:

It is very clear sasa kwamba CHADEMA wamezoea kupiga mikwara wasiyoweza kutekeleza. WAMESHINDWA kujitoa.

Mbaya zaidi CHADEMA wametoka kwenye hoja ya kujitoa kwenye mchakato, hotuba ya Lissu imekuja na mambo mengine mapya kuwa watahamasisha watanzania kuikataa rasimu.

Kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu ni tofauti na kujitoa kwenye mchakato.

Actually hata mimi, wewe na yule tunaweza kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu iwapo tutaona haina manufaa kwa taifa. Kwahiyo kitendo cha CHADEMA kusema watahamasisha watanzania kuikataa rasimu sio kitu cha ajabu, ila kina utoto ndani yake kwa sababu rasimu wenyewe hawajaiona. Utajiandaa vipi kupinga kitu ambacho hujakiona kama kina manufaa au hakina manufaa.

All in all chadema MKWARA waliopiga wa kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30.4.13 UMESHINDWA. CHADEMA imemsikiliza Prof. Baregu ambaye amewaambia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ni siasa za KITOTO...

Pamoja na kwamba nakubaliana na CDM katika mambo kadhaa, hawakuwa sahihi kujitoa! Maana yake ni kwamba wangekosa nafasi ya kuwaeleza wananchi uzuri au ubaya wa rasimu. Pili kujitoa kwao ni kufanya kosa ambalo wanalalamika ccm wamefanya! Kama kweli ccm wanaingilia mchakato, cdm hawaoni kama wangefanya walokosudia wangekuwa wanafanya avid same mistakes? Ilitosha sana kuonesha mapungufu ya tume, ili kwamba kama hatwatajirekebisha, iwe ni ground ya kuikataa rasimu!
 
Tumaini,

Umeshaweka hotuba yote hapo juu. Hii tabia ya kukata vipande vya hotuba hiyo hiyo na kuvipost ni kuwapotezea wasomaji appetite ya kufuatilia thread.

Kama una majibu ya hoja ziliyoibuliwa na wadau zilete lakini kurudia kutuma excepts toka kwenye hotuba sio sahihi...

kweli mkuu, huyu Tumaini Makene, amekata hotuba. Mambo kibao hayaonekani. sasa kuna sababu gani ya kusema FULL TEXT? Wacha uzandiki wewe Tumaini Makene. utadhani na wewe Mr. dhaifu? page zaidi ya 20 umemwachia nani azisome?
 
Swala la wajumbe kutengwa pesa za kutibia iwapo watapata UKIMWI linahitaji maelezo toka kwa waziri husika. Itakuwa kitu cha ajabu sana kama kuna pesa za namna hiyo!!!

Mkuu nami imenishangaza zaidi maana yake ni kwamba wanahalalisha wajumbe wa Tume kufanya ngono nzembe ama uzinzi wawapo katika kutekeleza majukumu yao ya tume na wakiathirika basi watagharamiwa? Na kama alivyouliza Mh. Sungura, waliwapima wajumbe wa Tume kabla ya kuteuliwa ili kufahamu kama walikuwa tayari ni waathirika ama majukumu ya tume yanapelekea kuathirika (in that sense je ofisi na wananchi wanaambukiza UKIMWI kama mionzi ama ni kama wanafanya kazi kwenye sources za radiation e.g nuclear poweplant etc)?
Kuhusu mafuta FULL TANK kama alivyosema Tundu Lissu napo kuna utata...posho ya laki 5 na zaidi kwa siku kwa muongozo upi wa utumishi? Mbona huku kwenye taasisi na idara zingine za serikali miongozo haisemi posho na ukarimu wa aina hii?
Tanzania, Tanzania, ooooooooooooh my country!!!
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa Bunge lakini kila msemaji wa Chadema anapoinuka ni lawama kwa serikali bila mapendekezo ya suluhu na kutupa vijembe hata kama jambo analozungumzia lina maslahi ya umma. Acheni kuwawapinzani wa nchi yenu
 
Kudai katiba mpya ilikua kisingizio cha kushindwa uchaguzi wa 2010. Kwao njia nzuri ya kuelezea mashabiki wao kwa nini walishindwa haikua kuwaambia kuwa hawa kubaliki kama walivyo dhani bali kwamba katiba iliyopo ilikua inapendelea CCM. Huwezi kudai kitu kisha ukikubaliwa ukikatae. Wao hawakutegemea serikali ingekubali mchakato wa katiba mpya.

Kwa sisi tulioshiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi wa mabaraza ya katiba ya Wilaya, tungewashangaa sana kama Chadema wasingejitoa, lakini mtu kama wewe mramba viatu vya ccm huwezi kuliona hilo.
 
Mheshimiwa Spika,

Yote ambayo tumeyasema hapa yanathibitishwa pia na Tume yenyewe. Tarehe 29 Aprili, 2013 Mwenyekiti wa Tume Jaji Warioba alikiri kwenye mkutano wa waandishi habari kwamba “... sehemu kubwa ya matatizo yaliyojitokeza yalisababishwa na misukumo na misimamo ya kisiasa na kidini.” Mwenyekiti Warioba amekiri kwamba kuna wajumbe wamejazwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya: “‘Hao waliojazana kwenye mabaraza wanadhani wanakuja kupiga kura, hapana.... Tume inazingatia uzito wa hoja zilizotolewa na wananchi na si idadi ya watu waliotoa maoni.’” Kwingineko, Mwenyekiti Warioba amekaririwa na vyombo vya habari akikiri kwamba kulikuwa na rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Hata hivyo, licha ya kukiri kuwepo kwa matatizo makubwa kama haya katika mchakato wa kuunda Mabaraza hayo, Mwenyekiti Warioba na Tume yake wamekataa madai ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Mabaraza kwa hoja kwamba kufanya hivyo kutachelewesha kupatikana kwa Katiba Mpya! Mheshimiwa Spika,

Kwenye red na bold ... sehemu kubwa ya matatizo yaliyojitokeza yalisababishwa na misukumo na misimamo ya kisiasa na kidini.” Hii lazima ni chama cha CCM na DINI yake ya Ponda & co

Na Mwenyekiti Warioba amekaririwa na vyombo vya habari akikiri kwamba kulikuwa na rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya NI lini CCM ikatenganishwa na rushwa?

Maneno ya matumaini “‘Hao waliojazana kwenye mabaraza wanadhani wanakuja kupiga kura, hapana.... Tume inazingatia uzito wa hoja zilizotolewa na wananchi na si idadi ya watu waliotoa maoni.’”
 
Katika swala la Mwangosi, Lissu alipaswa pia atoe ufafanuzi wa jinsi CHADEMA inavyotumia picha na video za tukio la kifo cha Mwangosi kujiingizia pesa. Ikumbukwe kuwa Mwangosi alikufa kwa sababu CHADEMA wakiongozwa na Dr. Slaa walikataa kuheshimu amri halali ya polisi na kwamba Dr. Slaa aliwachochea vijana wadharau amri ya polisi lakini yeye mwenyewe Dr. Slaa aliheshimu amri hiyo na kujifngia hotelini Iringa mjini huku akifuatilia matukio kwa njia ya simu kuulizia mambo yanaendeleaje.

Fujo zilizoongozwa na Dr. Slaa kwa simu zilisababisha Mwangosi kufa na sasa video na picha zake zinatumiwa na CHADEMA kujiingizia fedha ndani na nje ya nchi.

Mtu mzima akikaa kwenye internet akatunga uwongo live namna hii, tabu sana
 
Kwa sisi tulioshiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi wa mabaraza ya katiba ya Wilaya, tungewashangaa sana kama Chadema wasingejitoa, lakini mtu kama wewe mramba viatu vya ccm huwezi kuliona hilo.

Wewe kweli SIFURI kama Msigwa. Nani kakwambia chadema wamejitoa?
 
Katika swala la Mwangosi, Lissu alipaswa pia atoe ufafanuzi wa jinsi CHADEMA inavyotumia picha na video za tukio la kifo cha Mwangosi kujiingizia pesa. Ikumbukwe kuwa Mwangosi alikufa kwa sababu CHADEMA wakiongozwa na Dr. Slaa walikataa kuheshimu amri halali ya polisi na kwamba Dr. Slaa aliwachochea vijana wadharau amri ya polisi lakini yeye mwenyewe Dr. Slaa aliheshimu amri hiyo na kujifngia hotelini Iringa mjini huku akifuatilia matukio kwa njia ya simu kuulizia mambo yanaendeleaje.

Fujo zilizoongozwa na Dr. Slaa kwa simu zilisababisha Mwangosi kufa na sasa video na picha zake zinatumiwa na CHADEMA kujiingizia fedha ndani na nje ya nchi.

Wee kigoli mbona hueleweki? watu wanaongelea hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu wewe umeng'ang'ania Dr Slaaa tu basi kaanzishe thread yako na watu watakufuata huko, pls waache watu wadiscuss ki mature na peleka ujinga wako Lumumba
 
We kweli SIFURI kama Msigwa. Hujui kuwa hotuba imeelezea swala la Mwangosi, sasa sijui unajadili hotuba gani. AKili zako ni level ya bavicha, unawaza maandamano tu...
 
Kuhusu Kujitoa Tume ya katiba Mpya:

It is very clear sasa kwamba CHADEMA wamezoea kupiga mikwara wasiyoweza kutekeleza. WAMESHINDWA kujitoa.

Mbaya zaidi CHADEMA wametoka kwenye hoja ya kujitoa kwenye mchakato, hotuba ya Lissu imekuja na mambo mengine mapya kuwa watahamasisha watanzania kuikataa rasimu.

Kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu ni tofauti na kujitoa kwenye mchakato.

Actually hata mimi, wewe na yule tunaweza kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu iwapo tutaona haina manufaa kwa taifa. Kwahiyo kitendo cha CHADEMA kusema watahamasisha watanzania kuikataa rasimu sio kitu cha ajabu, ila kina utoto ndani yake kwa sababu rasimu wenyewe hawajaiona. Utajiandaa vipi kupinga kitu ambacho hujakiona kama kina manufaa au hakina manufaa.

All in all chadema MKWARA waliopiga wa kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30.4.13 UMESHINDWA. CHADEMA imemsikiliza Prof. Baregu ambaye amewaambia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ni siasa za KITOTO...
ZeMarcopolo, acha ujuha wewe. Soma hapa.

"Endapo hadi kufikia mwisho wa kipindi hicho Serikali itakuwa haijaleta Muswada wa marekebisho yanayotakiwa; au endapo Muswada utakaoletwa hautakidhi matakwa ya kuboresha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, basi CHADEMA itawaalika wanachama, wafuasi na mashabiki wake Tanzania nzima, pamoja na taasisi za kiraia na za kidini, vyama vya siasa na Watanzania wote wenye nia njema na taifa hili kuhamasisha Watanzania kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya kwenye kura ya maoni itakayofanyika kwa ajili ya kuihalalisha Katiba hiyo."- Tundu Lissu, Waziri Kivuli Katiba
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom