FULL TEXT: HOTUBA ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Lissu, Katiba na Sheria, yaibua makubwa bungeni

Chadema sio chama makini. Kingekuwa chaam makini kisingengoja mama Migiro aje kuwakumbusha umuhimu wa kuhamasisha wanachama na viongozi wake kushiriki mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba.

Wao kutwa kuandamana mpaka mambo ya msingi yanawapita halafu wanalia lia tu.

Hawa watu HOVYO kabisa...

nahisi we ZeMarcopolo utakuwa Zombie
 
Last edited by a moderator:
Ninachoona kuhusu hayo mabilion ya wajumbe na HIV ni haya
1.) Wajumbe wameingia kwenye Tume wakiwa na ukimwi, hivyo wanatafuta njia ya Maisha bora, nasema wameingia na ukimwi kwa sababu hakuna aliyepimwa na kuthibitika hana UKIMWI kabla ya kuanza hiyo kazi ya tume ya katiba.
2.) Tume ya katiba mpya inaamasisha ngono zembe, hii ni kurudisha nyuma mapambano zidi ya ukimwi
3) double standard na ubaguzi, nchi tayari ina funds za Ukimwi kuna Bilions karibu 20 zinatumika kila mwaka, wajumbe waingizwe Huko Kama wanaona kuna umuhimu wa kutafuta ukimwi
4.) wajumbe wa tume ya katiba ni wazinzi na hiyo kazi wanaifanya kuliko kazi yenyewe ya katiba,
5.) huu ni upuuzi kwa kufikiria kitu Kama hicho
6.) tusitegemee katiba mpya maana wajumbe wake wamekosa uhalisia zidi ya jamii tunayohishi, watashindwa kutoa katiba inayotafutwa na watanzania, POSHO ni moja ya mambo yanayopigwa vita sana na watanzania wa sasa, hii tume imejilimbikizia posho.
7.) kuna wahuni ndani ya tume ya katiba
8.) wanajaribu kitajirika kwa kutumia hii tume
9.) wajumbe wote wapimwe UKIMWI sasa ili kujua Kama wako FIT FOR A JOB
 
Hii hotuba ni nzuri sana na ya kisomi.

Msigwa alipaswa kuomba msaada kwa Tundu Lissu ili na yeye aandae hotuba ya kisomi sio ule uchafu alioleta juzi Bungeni.

Hongera Tundu Lissu.

Hoja za Lissu zinahitaji kujibiwa kwa hoja...
Mkuu ZeMarcopolo kweli umekunwa. Hotuba ni nzuri sana na ya kutetea nchi isiyo na majungu. Mimi sijaisoma yote kwa kuwa nilipofika kwenye posho zinazoombwa nikazimia. Nilipozinduka sikurudia tena kusoma nikaogopa kujitafutia kiharusi kisicho cha lazima.
 
Last edited by a moderator:
Hotuba ni ya kisomi lakini hoja pekee ambayo ufafanuzi wake unahitajika ni moja tu ya milioni 18 kwa ajili ya wajumbe wataopata UKIMWI.

Milioni 18 ni pesa ndogo, lakini hiyo sababu iliyotolewa ni absurd. Hata kama ingekuwa laki tatu bado hoja hii inahitaji ufafanuzi.
 
Nimeshitushwana hotoba ya kampi rasmi ya Upinzani bungeni katiba na sheria kutamtaja Dr.AshaRose Migiro kushiriki Siasa Chafu za kuteka mchakato wa mabariko ya katiba.Sijaamini kwa sabababu nilikuwa naamini kuwa mtu aliyefikia level yake hawezikurudi kwenye siasa duni kama hizi za ulaghai na ujanjaunja.
Mtualiyeshaka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu waumoja wa Mataifa kshiriki na kuongozasiasa za kitoto kama alivyo dai Tundu Lisu ni aibu na siajabu ndio maanaalisitishiwa mkataba UN
Eti MigiroKafanya haya !!!!

Barua pepe ya Dr. Asha-Rose Migiroinasema: “Naandika kuhimiza kazi ya kuwatia hamasa Makatibu wa Mikoa wasimamiekikamilifu mchakato wa kuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba. Kamamnavyofahamu Tume ya Katiba imeshatoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari... kuhusu zoezi hili muhimu. Sambamba na hatua za awali tulizochukua baada yakupata rasimu ya mwanzo ya Mwongozo wa Tume, hivi sasa tunatakiwa tuongezejuhudi za ushiriki wetu na kutayarisha makundi husika kama tulivyokwishaongea.”

Baada ya kuagiza ‘mawasiliano kati ya SUKI na Makatibu wa Mikoa’ kuhusu mamboya kufanya, Dr. Asha-Rose Migiro alimalizia barua yake kwa maneno yafuatayo:“Tafadhali wanakaliwa msisite kutoa maoni, ushauri na mbinu bora zaidi zakutimiza azma yetu katika suala hili muhimu.” ‘Wanakiliwa’ wa barua pepe ya Dr.Asha-Rose Migiro ni pamoja na Mh. Mwigulu Nchemba, Mh. Zakhia Meghji, Mh.Muhamed Seif Khatib na Bw. Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa NEC ya CCM.


Dr. Migiro umejishusha sana MHESHIMIWA
 
Hatuna wabunge kama hoja zenyewe ndizo hizi.

Kibwete

Unastahili kupewa pole, kama huwezihata kusoma masuala ya muhimu kwa nchi kama hotuba hiyo inavyoonesha na kufafanua.

Ukisoma utakuwa mwelewa. Nikutafunie? Haya soma kipande hiki hapa chini;

Mheshimiwa Spika,

Endapo hadi kufikia mwisho wa kipindi hicho Serikali itakuwa haijaleta Muswada wa marekebisho yanayotakiwa; au endapo Muswada utakaoletwa hautakidhi matakwa ya kuboresha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, basi CHADEMA itawaalika wanachama, wafuasi na mashabiki wake Tanzania nzima, pamoja na taasisi za kiraia na za kidini, vyama vya siasa na Watanzania wote wenye nia njema na taifa hili kuhamasisha Watanzania kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya kwenye kura ya maoni itakayofanyika kwa ajili ya kuihalalisha Katiba hiyo.
 
Maswali ya msingi ya kujiuliza ni

1.je, kwanini chadema haijahamasisha viongozi na wanachama wake kuhakikisha mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba hauwapitii pembeni.

2. je, mamilioni anayolipwa Dr. Slaa ili aende vijijini kutoa elimu ya uraia kupitia M4C imezaa matunda gani kama haijawawezesha viongozi na wanachama wa chadema kushiriki kidete katika mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba?

3. je, kwanini vijana wa bavicha hapa JF kila ilipoanzishwa thread ya uundwaji wa mabaraza ya katiba walikuwa hawachangii mada na badala yake wanajikita kwenye kujadili UDAKU mbalimbali unaoandikwa na gazeti la Tanzania Daima?

Chadema wanategemea mama Migiro atalala kama jinsi wao walivyolala juu yamchakato wa uundwaji wa mabaraza. Huo ni UTOTO...

Mkubwa hadi hii thread inafika kesho utakua na post kama mia mbili hivi sasa zidisha kwa 7000TZS kila post, Mkubwa nipe ajira kwa huo mtindo naweza tajirika mapema sana aisee. Yani umetawala thread nzima na mawazo ambayo siyo objective kabisa,Nilitegemea nawe ungeshusha ile ya hotuba ya upande wa CCM ili sote tuchangie kwa kulinganisha nani kamjali mwananchi. Badala yake wewe ni CHADEMA tuu na kulisha watu maneno kibao yasiyo na tija. Issue za kugusa wananchi moja kwa moja jaribu kuwa objective bila kuzingatia ni nani kawasilisha.

Nakumbuka hata kwenye hotuba ya Msigwa ambayo umeikomalia kuna mawazo ambayo yalitolewa na tume ya Diallo lakini wapinzani wameyachukua kuonyesha kama yalikuwa yanatija kwa jamii ila yakapigwa chini.
 
Hii bajeti ni kwaajili ya kupata katiba nzuri au ni kwaajili ya kunufaisha wajumbe wa katiba?
 
user-online.png
Tumaini Makene.
Nasema katika hali kama hiyo sina hakika kama tutafika salama; na tukifika salama tukiwa na uongozi huu huu wa Chama na Serikali mbele kutakuwa ni giza tupu. Majuto ni mjukuu, huja baadaye.”

Mheshimiwa Spika,

Baada ya maelezo haya marefu, naomba kukushukuru na wewe binafsi na naomba kuwasilisha.





---------------------------------------------------------------
Tundu Antiphas Mughwai Lissu
MSEMAJI & WAZIRI KIVULI, SHERIA, KATIBA NA UTAWALA
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Asante sana Waziri wangu wa Katiba na Sheria.
Hao Jamaa wa Green T-Shirts sidhani kama wanaelewa wanachokifanya lakini baya zaidi wameshindwa hata kusoma maandishi ya ukutani.Refer. KANU DEATH-Kenya.
 
Kuhusu barua pepe ya mama Asha-Rose Migiro:

Hapa kuna mambo mawili.
1. Hakuna kosa lolote kwa CCM kuhamasishana kushiriki katika mchakato wa katiba kama jinsi ilivyo si kosa kwa makundi mbalimbali ya kijamii kama NGO, wanaharakati etc. Kwahiyo kama kiongozi wa CM mama Migiro anayo sababu ya kuhamasisha wana CCM kutokujiweka mbali na uundwaji wa mabaraza ya katiba.

2. Chadema wameibuka na mchezo mpya wa kuingilia mawasiliano binafsi ya watu na kutokuon aibu kusema hadharani kuwa wamefanya hivyo.

Chadema inapaswa kutambua kuwa kuingilia mawasiliano binafsi ya watu ni kuvunja sheria za nchi. Hii ni sawa na mtu kusema kuwa "nimeingia chumbani kwa mtu fulani nikafungua kabati lake nimekuta ana shilingi laki mbili, nadhani hizi hela kaziiba". Hapa inabidi uulizwe, wewe umefikaje chumbani kwa mtu na kufungua kabati lake wakati mweyewe hayupo?

Hii inanikumbusha maisha yetu uswahilini ya nyumba za kupanga. Wapangaji tunatumia jiko la pamoja huku uswahilini. Kuna mpangaji mwezangu chumba cha jirani aliniambia kaka mbona wali wako hujaweka chumvi. Nikashangaa jamaa kajuaje kama mimi sijaweka chumvi?!!!

Hii ndio tabia waliyoanzisha chadema hivi karibuni...

Zemaco.....mbona hutaki kujiaminisha kuwa makundi yenu ya Urais ndio chanzo cha kuvuja kwa taarifa zenu za ndani za kimawasiliano? Kwani hujui kuwa ndani ya Secretariat yenu kuna vikumbo vya urais? Hujui kuwa wanaweza kuwa chanzo muhimu cha taarifa kwa lengo la kukomoana ili wapya walioingizwa waonekane hawafai? Jaribu kujifikirisha then jiulize mtindo wa taarifa zenu kuvuja kwa wingi ulianza lini.......
 
Baada ya Spika wa Bunge kupokea nakala ya hotuba ya kambi ya upinzani iliyokuwa haijawasilishwa hapo awali, spika akatoa maelekezo kuwa kutokana na 'kifungu cha 99 (5)' kanuni za bunge zinawataka mawaziri wote kuwasilisha nakala mezani kwa kuzingatia mpangilio wa bunge kabla shughuli za uwasilishaji hazijaanza. Hotuba ya Serikali na Kambi ya Upinzani zilikuwa hivi...



 

Attachments

  • MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI_3.pdf
    273.5 KB · Views: 103
Last edited by a moderator:
Serikali ya namna hii inayoshiriki uvunjifu wa haki za binadamu kwa kiwango hiki, imepoteza uhalali wa kutawala kama anavyoonesha Lissu hapa;


Mheshimiwa Spika,

Sasa Taarifa ya Uchunguzi wa Kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Bw. Daudi Mwangosi, iliyoandaliwa na Kamati iliyoundwa na Mheshimiwa Nchimbi na kuchapishwa tarehe 9 Oktoba 2012 imethibitisha ukweli wa kauli hii na ukweli wa madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya matumizi ya nguvu ya Jeshi la Polisi. Baada ya kuzunguka huku na huko ikijaribu kulisafisha Jeshi la Polisi, Taarifa ya Kamati hiyo inasema: “Hapakuwepo na uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo la ulipuaji wake ni ili watu waogope na kukimbia.”

Aidha, Kamati hiyo iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema, inakiri kwamba “hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomu la Kishindo kwa sababu hata ingekuwa ukamataji tayari askari polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio.” Kwa misingi hiyo, “… Kamati imeona kwamba … tukio la kuuawa Bw. Daudi Mwangosi na kuumizwa baadhi ya askari polisi halikustahili kabisa.”

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli kama inakubaliana na matokeo ya taarifa hizi tatu zilizoandaliwa na taasisi za kiserikali kama vile Tume ya Haki za Binadamu, Kamati ya Jaji Ihema na MCT/TEF juu ya kuhusika kwa Jeshi la Polisi na mauaji ya marehemu Daudi Mwangosi. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iteo kauli mbele ya Bunge lako tukufu kama inakubaliana na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu kwamba kitendo cha Kamanda Kamuhanda kupiga marufuku mkutano halali wa CHADEMA kilikuwa ni kinyume cha Sheria ya Jeshi la Polisi, Sheria ya Vyama vya Siasa na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli kama – baada ya ushahidi wa taarifa hizi tatu - iko tayari kuiomba radhi CHADEMA kwa kuisingizia kuhusika na kifo cha marehemu Daudi Mwangosi. Na mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge lako tukufu kama iko tayari kuilipa familia ya marehemu Mwangosi fidia kwa mujibu wa sheria kwa kitendo cha Serikali kusababisha mauaji yake bila ‘uhalali.’

Mheshimiwa Spika,

Serikali na chama ambacho sera zake zinakiuka haki za binadamu na misingi ya utawala bora inapoteza uhalali (legitimacy) ya kuendelea kutawala. Hapa ndipo CCM na Serikali yake ilikoifikisha nchi yetu: waandishi wa habari wanauawa kwa sababu ya kufanya kazi yao halali ya kutafuta habari za mambo yanayohusu umma kama mikutano ya vyama vya siasa. Watanzania hawastahili Serikali ya aina hii. Kama alivyosema Baba wa Taifa katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania:

“Hatulazimiki kuendelea na uongozi mbovu wa Chama na Serikali. Wala tukiendelea na hali hii, bila kubadili uongozi wa Chama na Serikali, sina hakika kama tutafika huko salama. Masuala muhimu ya nchi yetu hayatashughulikiwa.... Na masuala mengine muhimu ... yataachwa yajitatue yenyewe. Nasema katika hali kama hiyo sina hakika kama tutafika salama; na tukifika salama tukiwa na uongozi huu huu wa Chama na Serikali mbele kutakuwa ni giza tupu. Majuto ni mjukuu, huja baadaye.”

Mheshimiwa Spika,

Baada ya maelezo haya marefu, naomba kukushukuru na wewe binafsi na naomba kuwasilisha.
 
Serikali ya namna hii inayoshiriki uvunjifu wa haki za binadamu kwa kiwango hiki, imepoteza uhalali wa kutawala kama anavyoonesha Lissu hapa;


Mheshimiwa Spika,

Sasa Taarifa ya Uchunguzi wa Kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Bw. Daudi Mwangosi, iliyoandaliwa na Kamati iliyoundwa na Mheshimiwa Nchimbi na kuchapishwa tarehe 9 Oktoba 2012 imethibitisha ukweli wa kauli hii na ukweli wa madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya matumizi ya nguvu ya Jeshi la Polisi. Baada ya kuzunguka huku na huko ikijaribu kulisafisha Jeshi la Polisi, Taarifa ya Kamati hiyo inasema: "Hapakuwepo na uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo la ulipuaji wake ni ili watu waogope na kukimbia."

Aidha, Kamati hiyo iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema, inakiri kwamba "hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomu la Kishindo kwa sababu hata ingekuwa ukamataji tayari askari polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio." Kwa misingi hiyo, "… Kamati imeona kwamba … tukio la kuuawa Bw. Daudi Mwangosi na kuumizwa baadhi ya askari polisi halikustahili kabisa."

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli kama inakubaliana na matokeo ya taarifa hizi tatu zilizoandaliwa na taasisi za kiserikali kama vile Tume ya Haki za Binadamu, Kamati ya Jaji Ihema na MCT/TEF juu ya kuhusika kwa Jeshi la Polisi na mauaji ya marehemu Daudi Mwangosi. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iteo kauli mbele ya Bunge lako tukufu kama inakubaliana na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu kwamba kitendo cha Kamanda Kamuhanda kupiga marufuku mkutano halali wa CHADEMA kilikuwa ni kinyume cha Sheria ya Jeshi la Polisi, Sheria ya Vyama vya Siasa na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli kama – baada ya ushahidi wa taarifa hizi tatu - iko tayari kuiomba radhi CHADEMA kwa kuisingizia kuhusika na kifo cha marehemu Daudi Mwangosi. Na mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge lako tukufu kama iko tayari kuilipa familia ya marehemu Mwangosi fidia kwa mujibu wa sheria kwa kitendo cha Serikali kusababisha mauaji yake bila ‘uhalali.'

Mheshimiwa Spika,

Serikali na chama ambacho sera zake zinakiuka haki za binadamu na misingi ya utawala bora inapoteza uhalali (legitimacy) ya kuendelea kutawala. Hapa ndipo CCM na Serikali yake ilikoifikisha nchi yetu: waandishi wa habari wanauawa kwa sababu ya kufanya kazi yao halali ya kutafuta habari za mambo yanayohusu umma kama mikutano ya vyama vya siasa. Watanzania hawastahili Serikali ya aina hii. Kama alivyosema Baba wa Taifa katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania:

"Hatulazimiki kuendelea na uongozi mbovu wa Chama na Serikali. Wala tukiendelea na hali hii, bila kubadili uongozi wa Chama na Serikali, sina hakika kama tutafika huko salama. Masuala muhimu ya nchi yetu hayatashughulikiwa.... Na masuala mengine muhimu ... yataachwa yajitatue yenyewe. Nasema katika hali kama hiyo sina hakika kama tutafika salama; na tukifika salama tukiwa na uongozi huu huu wa Chama na Serikali mbele kutakuwa ni giza tupu. Majuto ni mjukuu, huja baadaye."

Mheshimiwa Spika,

Baada ya maelezo haya marefu, naomba kukushukuru na wewe binafsi na naomba kuwasilisha.

Tumaini,

Umeshaweka hotuba yote hapo juu. Hii tabia ya kukata vipande vya hotuba hiyo hiyo na kuvipost ni kuwapotezea wasomaji appetite ya kufuatilia thread.

Kama una majibu ya hoja ziliyoibuliwa na wadau zilete lakini kurudia kutuma excepts toka kwenye hotuba sio sahihi...
 
Back
Top Bottom