Huyu jamaa ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu ndani ya chama chake.Wee kigoli mbona hueleweki? watu wanaongelea hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu wewe umeng'ang'ania Dr Slaaa tu basi kaanzishe thread yako na watu watakufuata huko, pls waache watu wadiscuss ki mature na peleka ujinga wako Lumumba
ZeMarcopolo, acha ujuha wewe. Soma hapa.
Nimekuwa mfuatiliaji wa Bunge lakini kila msemaji wa Chadema anapoinuka ni lawama kwa serikali bila mapendekezo ya suluhu na kutupa vijembe hata kama jambo analozungumzia lina maslahi ya umma. Acheni kuwawapinzani wa nchi yenu
Ndo kama jibu lako lilivyo kila kitu ni mitusi bila kujadili hoja.Nonsense!
cjaona mahali ikizungumzia mahakama, kesi kurundikana, mazingira mabovu ya utendaji kazi wa waandaaji wa haki ya mtu kupatikana na mengine. au yapo kwenye page zilizosalia?
Kwa sisi tulioshiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi wa mabaraza ya katiba ya Wilaya, tungewashangaa sana kama Chadema wasingejitoa, lakini mtu kama wewe mramba viatu vya ccm huwezi kuliona hilo.
Hii hotuba ni nzuri sana na ya kisomi.
Msigwa alipaswa kuomba msaada kwa Tundu Lissu ili na yeye aandae hotuba ya kisomi sio ule uchafu alioleta juzi Bungeni.
Hongera Tundu Lissu.
Hoja za Lissu zinahitaji kujibiwa kwa hoja...
Yaani nusu ya hotuba inazungumza habari za mkoa mmoja tu Arusha tena kata ya Sombetini tu, hiki chama kina kazi kuba sana kujivua tuhuma za ukabila na ukanda
Halo umeniacha na maswali kadhaa, Hivi Kama ametoa hoja nzuri zinahitaji kujibiwa kwa hoja au kwa vitendo?, Na kama kwa hoja ambayo ni maneno, je hoja hizo zitakuwa zimesaidia kurekebisha tatizo lililoongelewa katika hoja ya mwasilishaji?. Mi nadhani serikali ingeweza kuchambua kipi cha kufanyia kazi ili kiwekwe katika utendaji na kile kisichofaa kiwekwe katika kabati kama tulivyozoea.
Kuhusu barua pepe ya mama Asha-Rose Migiro:
2CHADEMA inapaswa kutambua kuwa kuingilia mawasiliano binafsi ya watu ni kuvunja sheria za nchi. Hii ni sawa na mtu kusema kuwa "nimeingia chumbani kwa mtu fulani nikafungua kabati lake nimekuta ana shilingi laki mbili, ?
Hii ndio tabia waliyoanzisha CHADEMA hivi karibuni...
Maswali ya msingi ya kujiuliza ni
1.je, kwanini CHADEMA haijahamasisha viongozi na wanachama wake kuhakikisha mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba hauwapitii pembeni.
2. je, mamilioni anayolipwa Dr. Slaa ili aende vijijini kutoa elimu ya uraia kupitia M4C imezaa matunda gani kama haijawawezesha viongozi na wanachama wa CHADEMA kushiriki kidete katika mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba?
3. je, kwanini vijana wa BAVICHA hapa JF kila ilipoanzishwa thread ya uundwaji wa mabaraza ya katiba walikuwa hawachangii mada na badala yake wanajikita kwenye kujadili UDAKU mbalimbali unaoandikwa na gazeti la Tanzania Daima?
CHADEMA wanategemea mama Migiro atalala kama jinsi wao walivyolala juu yamchakato wa uundwaji wa mabaraza. Huo ni UTOTO...
Yaani nusu ya hotuba inazungumza habari za mkoa mmoja tu Arusha tena kata ya Sombetini tu, hiki chama kina kazi kuba sana kujivua tuhuma za ukabila na ukanda