Hoja na maneno ya wanasiasa wetu kama haya ni kutafuta sifa na hongera za kitoto!.
Kwa hiyo Mhe. Zitto anataka kutuambia baada ya kusoma maazimio ya PAC, hata wasiwasi wa kuuwawa umeisha.
Kwani yeye kama angeuwawa, hata maazimio ya PAC yangeuwawa wakati Kamati ya PAC ilikuwa na wajumbe zaidi ya 18?
Nilishangaa sana kuwasikia eti wanasema hawakulala kwa sababu walikuwa wanalinda repoti isiibiwe. Really?
Hizi ndizo fikra na mitazamo ya kudhani bila mimi hakuna mwingine anayeweza!
Wao wameishatimiza wajibu wao kama PAC, haya mengine ni kutafuta sifa kwa nguvu.
Politics is perhaps the only profession for which no preparation is thought necessary-Robert Louis Stevenson