FT: Yanga 1-0 Simba| Azam Sports Federation Cup| CCM Kirumba, Mwanza

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,128
Ahlan Wasahlan wana JF

Ni mtanange wa kukata na shoka baina ya Yanga Vs Simba katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho la Azam ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ni mchezo unaozikutanisha timu mbili zenye mafanikio zaidi katika soka la Tanzania. Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana katika michuano hii ni msimu uliopita katika fainali ambapo Simba ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa 1-0 pale mjini Kigoma.

Yanga itashuka dimbani ikihitaji kulipiza kisasi lakini pia kujaribu kutwaa ndoo hiyo pamoja na ndoo ya Ligi Kuu kwa pamoja huku Simba wakishuka dimbani kujaribu kushinda ili walau wapate taji la kufutia machozi msimu huu.

Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi wa mechi ya Azam Fc Vs Coastal Union katika mchezo wa Fainali utakaopigwa jijini Arusha baadae mwaka huu.

Huu ni mchezo ambao lazima mshindi apatikane. Hivyo hakutakuwa na droo.

Kutokana na uwanja wa CCM Kirumba kutokuwa na taa, mechi itapigwa saa 9:30 alasiri hivyo wapenzi na mashabiki mnakumbushwa kuwahi uwanjani na kwenye vibanda umiza.

Mchezo huu utakujia live kupitia Azam Sports 1HD na updates zote utazipata hapa usicheze mbali...

Vikosi

=========

BFFD7C09-4066-499A-B02A-B2B03D2E70D6.jpeg
72B1040D-7ED9-4AC5-B941-D6890FE5B83F.jpeg

Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, uwanja umejaa
2' Mchezo umeanza kwa timu zote kufungu10' Yanga wametawala mchezo licha ya kuwa Simba nao wanafunguka
15' Kuna ushindani mkali unaendelea, faulo za hapa na pale
20' Yanga wanafika langoni kwa Simba mara kadhaa
23' Ushindani wa Mayele na walinzi wa Simba ni mkali

25' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Feisal Salum anaipatia Yanga bao kwa shuti kali kutoka nje ya 18

33' Kibwana Shomari wa Yanga anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kibu Denis
34' Simba wanakosa bao, mpira wa kichwa cha Onyango unatoka nje
37' Sure Boy anamchezea faulo Sakho
38' Kasi ya mchezo imepungua kidogo tofauti na ilivyoanza
38' Mayele anashindwa kutumia nafasi nzuri aliyopata, anabaki na kipa lakini Kakolanya anauwahi mpira.
42' Simba wanafanya shambulizi kali, Mugalu anapiga shuti linazuiwa inakuwa kona
45' Zinaongezwa dakika 2 za nyongeza.
45+1' Lwanga yupo chini ameumia baada ya kugongwa jichoni na Makambo wakati wakiwania mpira

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
Simba wanamtoa Lwanga anaingia Bwalya
47' Mugalu anamchezea faulo Job.
48' Simba wanapata na, inapigwa inaokolewa
50' Inonga anacheza vizuri kwa kumdhibiti Makambo ndani ya boksi la Simba
52' Simba wametawala mchezo tangu kuanza kwa kipindi cha pili
60' Kibu ameumia na anatoka damu karibu na jicho, anatibiwa na kurejea uwanjani
63' Shomari Kibwana anatoka, anaingia Farid Musa
65' Onyango anamzungusha mtu ndani ya boksi lake na kuokoa
67' Simba wanafanya shambulizi lakini Kibu anakuwa ameunawa mpira
68' Makambo anatoka, anaingia Ngushi
73' Sure Boy anapiga shuti kali linatoka nje
76' Meddie Kagere kaingia ametoka Muzamiru Yassin
76' Kibu anatoka baada ya kuumia, anaingia Yusuph Mhilu
82' Kasi ya mchezo imepungua lakini ni Simba wanaoonekana kuwa na kasi ya kutafuta bao
83' Fei Toto anatoka anaingia Zawadi Mauya upande wa Yanga
90' Zinaongezwa dakika tatu

FULL TIME
 
Ahlan Wasahlan wana JF

Ni mtanange wa kukata na shoka baina ya Yanga Vs Simba katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho la Azam ndani ya dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ni mchezo unaozikutanisha timu mbili zenye mafanikio zaidi katika soka la Tanzania. Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana katika michuano hii ni msimu uliopita katika fainali ambapo Simba ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa 1-0 pale mjini Kigoma.

Yanga itashuka dimbani ikihitaji kulipiza kisasi lakini pia kujaribu kutwaa ndoo hiyo pamoja na ndoo ya Ligi Kuu kwa pamoja huku Simba wakishuka dimbani kujaribu kushinda ili walau wapate taji la kufutia machozi msimu huu.

Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi wa mechi ya Azam Fc Vs Coastal Union katika mchezo wa Fainali utakaopigwa jijini Arusha baadae mwaka huu.

Huu ni mchezo ambao lazima mshindi apatikane. Hivyo hakutakuwa na droo.

Kutokana na uwanja wa CCM Kirumba kutokuwa na taa, mechi itapigwa saa 9:30 alasiri hivyo wapenzi na mashabiki mnakumbushwa kuwahi uwanjani na kwenye vibanda umiza.

Mchezo huu utakujia live kupitia Azam Sports 1HD na updates zote utazipata hapa usicheze mbali...
SIMBA 2 yanga 1
-679188381866516060.jpg
 
mechi ya Leo mayele Nampa nafasi kubwa ya kufunga hata kama yanga watapoteza mechi, kwa mechi mbili mfululizo mabeki wa Simba wametumia nguvu nyingi kumkaba Leo forward ya yanga itabadili mbinu ya ufungaji hakutakua na mipira mirefu ya mayele kukimbizana na inonga zitapigwa pasi za hatari mayele atakutana Nazo na kugusa kwene nyavu tu.
 
Hatafunga hata moja mark my words
 
Back
Top Bottom