Naona humu zimeanza nyimbo za mapema za malalamiko kuwa Azam ni tawi la Yanga

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,358
2,497
Yaani mashabiki ni watu wa ajabu sana, yaani kisa Azam kufungwa na Yanga na wao kuwashindwa basi inachukuliwa kama Azam wanafungwa na Yangs kwa kupenda. Kwanza hakuns derby tamu inayokuwa na ushindani kama mechi ya Azam dhidi ya Yanga, haijawahi kuwa mechi nyepesi na pia ni mechi inayokuwa yenye kasi, ufundi na burudani haswa mtu una enjoy mpira wa kitabuni. Hakunaga papatu papatu wala mmoja kupaki bus.

Swala la Azam kufungwa na Yanga ni swala la kuzidiwa kimchezo, kama Yanga anafungika kirahisi basi nyie Simba ndio mngekuwa walimu wa kuwafundisha timu zingine jinsi ya kumfunga Yanga. Lakini nyie wenyewe mmekula goli tano je kwanini msianze kujinyoshea vidole nyie kwanza kuwa ni tawi la Yanga? Yanga alikuwa anafungwa ns Ihefu kulr Mbeya mfululizo lakini Simba ikienda Mbeya inashida tu kiulaini na Yanga hawakuwaza kuhusu tawi bali tunajua ni mpira ulivyo.

Timu fulani inaweza kuwa tishio kwa timu fulani lakini timu nyingine ikamtandika tu, mpira ni mchezo wa mbinu na ufundi na ni mchezo wa wazi. Hakuna mechi ambayo Yanga imfunga Azam kwa magoli ya kuachiwa bali magoli ya jitihada haswa.

Kwasasa tawi la Yanga ni Simba aliyeachia goli tano kwa Yanga
 
Back
Top Bottom