Mchambuzi wa soka Jemedari Saidi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika
KWA-MKAPA HATOKI MTU - Hii slogan iliyoanzishwa na Simba SC ndiyo hasa inawaumiza kichwa CAF, RS BERKANE na VIBARAKA wao. Wanahofia kombe litabakia Tanzania, kama hali hii ya kiwanja ipo hivi leo, WHY mechi isichezwe ikachezwe Zanzibar?
CAF waliwapa mashabiki wa Simba SC tunzo ya mashabiki bora Afrika wakiwa hata hawajacheza Nusu Fainali, lakini ile turn out yao kila game na namna wanavyohanikiza ushindi ilikuwa balaa, leo timu ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa. CAF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya CAF inatafuta ahueni ikacheze Zenji kwenye mashabiki 15,000 wanaogopa mashabiki 60,000/ watashusha gharika.
Nafahamu jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali, TFF na Simba SC juu ya kutumia uwanja wa Mkapa., nafahamu namna msimamizi/mkaguzi wa Viwanja wa CAF wa mwanza (Moustafa) ambaye alikuwa Mmorocco alivyokuwa anataka mechi ikachezwe Zanzbar akiogopa Kwa-Mkapa, nafahamu aliyeletwa pia anatoka Morocco 🇲🇦.
Hapa kuna vita ya Morocco 🇲🇦 Vs Tanzania 🇹🇿, kama una kichwa maji pekee ndio huwezi kujua hii kitu. Ila Morocco mpaka sasa wanasaidiwa na CAF kitu ambacho ni hatari sana.
Hata hivyo mara baada ya Jemedari kuchapisha ujumbe huo Mchambuzi nguli Edo Kumwembe akaweka comment yake kwenye post hiyo ya Jemedari ✍🏿
"Tumefungua uwanja mwaka 2007....mpaka leo mvua ikinyesha unatuama maji. Pambano la Simba na Al Masry liliharibika kwa sababu ya pitch kujaa maji. Tangu hapo hakuna mechi ya CAF iliyochezwa hapo. Wachina wametupiga tunasingizia Wamorocco wanatuogopa. Moja kati ya sifa kubwa ya uwanja wetu katika mafaili yao ni hiyo. Akina Morisson washapiga sana chenga katika madimbwi. Ebu tunyoooke kidogo na kuwanyoosha wahusika. Mvua kali sio sababu ya uwanja kutuama maji. Tusipige siasa nyingine.
".
Una mtazamo gani na hiki kilichoelezwa.