FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,022
Reaction score
6,858
RS Berkane VS Simba SC

| Fainali CAF Confederation Cup

| 17 Mei, 2025

IMG_20250516_203412.jpg
Mashabiki wa Mnyama tayari wameanza kufanya kazi yao

Timu imeondoka kambini kwenda uwanjani.


Kikosi cha Simba tayari kimewasili Uwanjani


​
Vikosi na mfumo kwa kila timu

RS Berkane are playing- 3-5-2 Simba are playing- 4-1-2-3 Tactical sheet here. #cafccwithmickuy.jpg
 
Hii itakuwa ni mechi ya tatu kwao kukutana katika michuano ya Kombe la Shirikisho, kwani mwaka 2022 walikutana makundi na kila moja ilishinda mechi ya nyumbani, Wamorocco wakishinda 2-0 kabla Wekundu kulipa kisasi cha 1-0 Kwa Mkapa.

RS Berkane si timu kubeza; msimu huu pekee, wamefunga jumla ya mabao 18-0 katika mechi zao zote za nyumbani za mashindano haya. Huu ni ujumbe mzito kwa Simba kwamba inapaswa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa tahadhari kubwa, na kwa malengo yaliyowekwa wazi kuondoka Morocco wakiwa bado na nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo watakaporejea nyumbani.

Kwa upande Wao Simba nao sio Kinyonge katika mashindano ya msimu huu wameshinda mechi sita, wamesuluhu mbili na kufungwa mbili..

Rs Berkane walifuzu fainali ya 24/25 kwa kuwatoa CS Constantine kwa jumla ya magoli 4-1 huku Simba ikifuzu fainali kwa ushindi wa jumla goli 1-0 dhidi ya Stellenbosch




#TotalEnergiesCAFCC
 
Duh hii NDO Tz
Mchana mpira
Asubuh mpira
Usku mpira
Hadi mida ya wanga mada ni mpira

Uskute hata wachaw wanaenda kuwanga na smartphone zao wanaperuz na kureply na mada huko vilingeni kwao NDO hvohvo mpira mpaka uchawi unakua Hauna faida kama wazungu vile
 
RS Berkane timu yangu ya utotoni mjue nimeacha Kazi ya ofisini mshahara milioni 4 kwa ajili ya kuja kuwapa support nyie

Msiniangushe, naombeni mmalize mechi hapa hapa Morocco, mtakuwa mmeokoa dunia kwa kelele nyingi sana
 
RS Berkane timu yangu ya utotoni mjue nimeacha Kazi ya ofisini mshahara milioni 4 kwa ajili ya kuja kuwapa support nyie

Msiniangushe, naombeni mmalize mechi hapa hapa Morocco, mtakuwa mmeokoa dunia kwa kelele nyingi sana
Acha ulozi
 
Back
Top Bottom