FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

RS Berkane timu yangu ya utotoni mjue nimeacha Kazi ya ofisini mshahara milioni 4 kwa ajili ya kuja kuwapa support nyie

Msiniangushe, naombeni mmalize mechi hapa hapa Morocco, mtakuwa mmeokoa dunia kwa kelele nyingi sana
Utopolo ingine hii.
 
Hii ndiyo maana halisi sasa ndugu zangu ya Ubaya Ubwela! Kila la heri kwa RS Berkane. No way out. Mimi ni Mzalendo kwa nchi yangu tu ya Tanganyika. Sijawahi kuwa Mzalendo kwenye mambo ya hovyo hovyo.
Utopolo ingine hii.
 
Hii itakuwa ni mechi ya tatu kwao kukutana katika michuano ya Kombe la Shirikisho, kwani mwaka 2022 walikutana makundi na kila moja ilishinda mechi ya nyumbani, Wamorocco wakishinda 2-0 kabla Wekundu kulipa kisasi cha 1-0 Kwa Mkapa.

RS Berkane si timu kubeza; msimu huu pekee, wamefunga jumla ya mabao 18-0 katika mechi zao zote za nyumbani za mashindano haya. Huu ni ujumbe mzito kwa Simba kwamba inapaswa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa tahadhari kubwa, na kwa malengo yaliyowekwa wazi kuondoka Morocco wakiwa bado na nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo watakaporejea nyumbani.

Kwa upande Wao Simba nao sio Kinyonge katika mashindano ya msimu huu wameshinda mechi sita, wamesuluhu mbili na kufungwa mbili..

Rs Berkane walifuzu fainali ya 24/25 kwa kuwatoa CS Constantine kwa jumla ya magoli 4-1 huku Simba ikifuzu fainali kwa ushindi wa jumla goli 1-0 dhidi ya Stellenbosch




#TotalEnergiesCAFCC
Huu ndio ulitskiwa kuwa uzi
 
Dah... kumbe wamefunga jumla ya mabao 18-0 katika mechi zao zote za nyumbani za mashindano! Si timu ya kawaida hiii ... hata Raja, Wydad, Far Rabat na wengine hawakufaniniwa kufunga hata kagoli kamoja kwenye uwanja huo!

Simba ina nafasi ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga goli nyumbani kwao msimu huu.
 
Mpanzu na wahuni wenzake wedharaulika mno

1747456988413.png
 
Back
Top Bottom