FT: NBCPL, Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar | Uwanja wa Mkapa | 30/10/2022

Pettymagambo

JF-Expert Member
Aug 21, 2017
1,423
7,911
FULL TIME

90' Sakho anaipaia Simba goli la tano
GOOOOOOOOO
81 Mtibwa wamerudi nyuma na kuwapa Simba nafasi ya kumiliki mpira muda mwingi
77' Simba wanafanya mashambulizi mfululizo
Phiri anaipatia Simba goli la 4
73' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Beki wa Mtibwa anapata kadi ya njano ya pili na hivyo kuwa nyekundu
66' Ilanfya ana kazi nzito dhidi ya beki wa Simba, Inonga
Pasi ya kifua kutoka kwa Zimbwe Jr inatua mguuni kwa Okrah anafunga
64' GOOOOOOOOOOOOOO
55' Simba wanaendelea kumiliki mpira muda mwingi
Sakho anaipatia Simba goli la pili, anashangilia kwa staili kama anatambaa
48' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
47' Mchezo umeanza kwa kasi ya chini tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO'
45' Zinaongezwa dakika 3 za nyongeza
44' Sakho anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
40' Kitenge wa Mtibwa Sugar anapata kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Sakho, kisha kuonekana akimkanyaga mgongoni
40' Simba bado wanaendelea kucheza mpira kwa kasi
Mzamiru anaipatia Simba goli la kwanza akipata pasi kutoka kwa Okrah
38' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
33' Kipa wa Mtibwa, Tshikalo anatolewa baada ya kuumia wakati akiokoa
27' Simba wanacheza kwa kasi kutafuta goli
20' Simba wanalalamika mchezaji wa Mtibwa kuunawa mpira ndani ya 18 lakini refa kapeta
15' Mtibwa wanapata nafasi na kupiga shuti, Manula anadaka
10' Kasi ya mchezo inaendelea kuwa juu, Simba wakionekana kutafuta goli
5' Simba wameanza kwa presha kubwa ya kutafuta goli
Mchezo umeanza

Timu zinaingia uwanjani
FgU3XI5XEAEbGNg.jpg
========
Ni katika muendelezo wa Nbcpl leo katika Dimba la Mkapa! Wekundu wa msimbazi SIMBA katika kuzitafuta pointi 3 watawavaa wazee wa Manungu, MTIBWA SUGAR, mechi itaanza saa 1 kamili jioni hii na leo mnyama atapata nafasi ya kujiuliza alikosea wapi game iliyopita mpaka kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwa lambalamba, tuwe pamoja wanalunyasi kupeana updates mpaka mwisho, karibuni.
 
Nikatika muendelezo wa Nbcpl leo katika dimba la taifa! wekundu wa msimbazi SIMBA katika kuzitafta pointi 3 watawaalika wazee wa manungu tuliani MTIBWA SUGAR, mechi itaanza saa 1 kamili jioni hii na leo mnyama atapata nafasi ya kujiuliza alikosea wapi game iliyopita mpaka kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwa lambalamba, tuwe pamoja wanalunyasi kupeana updates mpaka mwisho, karibuni.
Mtibwa piga hao Mikia wamtimue Bonge arudi kwao Tanga
 
Back
Top Bottom