FT: Yanga SC 4-1 Mtibwa Sugar | NBC Premier League | Azam Complex | 16.12.2023

Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
12,138
25,391
Naam majira ya saa 12:30 jioni ya Leo wananchi tutakuwa na jambo letu

20231215_222519.jpg
Magoli mawili yaliyofungwa na Stephane Aziz Ki na mengine ya Kennedy Musonda na Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ yameipa Yanga ishindi wa magoli 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam complex Jijini Dar es Salaam.

Yanga imeendelea kubaki nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikifikisha pointi 27 katika mechi 10, Azam FC ikiongoza kwa kuwa na pointi 28 ikicheza mechi 12, Simba ikiwa ya tatu kwa kuwa na pointi 22 kwenye michezo 9.

Mtibwa ambayo imepata goli lake kupitia kwa Seif Rashid, imeendelea kushika mkia, ikiwa nafasi ya 16 kwa kuwa na pointi 5 katika mechi 13.
 
Mwasibu ulipigaje hapa??🤭🤭
 
Mwasibu ulipigaje hapa??🤭🤭
🤣🤣🤣Hapa alizingua baadae akaja kula 5 akawa kimyaaa
 
Back
Top Bottom