Pamoja na kufungwa ila real madrid wamejitahidi sana, wameonesha ushindani mkubwa sana kwenye el classico ya leo kinyume na matarijio ya wengi, hasa walivyorudi second half.
Binafsi nilitegemea hii mechi barca angeimaliza mapema sana kama alivyofanya kwenye elclassicos mbili zilizopita.
Angalau kidogo leo tumeona hadhi ya el classico ambapo mzani ulibalance mpaka filimbi ya mwisho
Ila naona leo zile kelele za real madrid kuhusu marefa zimewasaidia kiasi fulani, refa kachezesha mechi kwa kuwaogopa real madrid kuna fouls nyingi sana kazipotezea upande wa real madrid hata ile handball ya Valverde ilistahili kuwa penalty maana ule mpira ulikuwa unafikia miguuni kwa Ferran, kiufupi pale Valverde alizuia move ya goli bila kukusudia.
Wachezaji wa real madrid hasa Rudger hawana class kabisa... siwatofautishi na wachezaji wa kwenye michuano ya ndondo cup.