From Madame B to Mung Chris...

From Madame B to Mung Chris...

Kwako Mung Chris kipenzi cha moyo wangu na tiba ya maradhi yangu sugu.
Ni siku, wiki, na hatimaye imetimu miezi mitatu tangu tuanze safari ya penzi letu tamu na lisilochuja hapa duniani tulilolianzisha hapa Jamii forums tarehe kama ya leo.
Na pia nakumbuka jinsi tulivyosumbuana hapa Jamii Forums kule Pm kila siku.
Usijali....(ile ilikuwa mitego yangu kukupima kiasi cha upendo wangu kwako).

Hakika sikutaraji kama nitaweza kupata mwenza wa kuweza kunituliza na kufanya niweze kuwa kiumbe kipya katika safari hii ya penzi tamu.

Sijutii kukupenda
Sijutii uamuzi wangu
Sijutii kuchaguliwa na wewe
Sijutii vile binadamu wanasema nini kunihusu mimi au wewe.
Ila kwangu utabaki kuwa mpenzi na baba bora wa mtoto wetu mtarajiwa.

Natamani nimalize hii ng'we salama ili niweze kupakata katoto kako kalikochanganya damu ya Kisambaa na Kichaga.
Nakupenda leo
Nitakupenda kesho na
Nitakupenda milele daima.
Labda mmoja wetu afariki.

Kila mmoja ana mapungufu yake, hakuna aliyekamilika kwa 100%
Kama kuna sehemu naendelea kukukosea naomba uwe muwazi na uniambie ukweli.
Hatuhitaji kuishia njiani.

Asante kaka mkuu Maxence Melo kwa kuanzisha mtandao huu kwani kwa namna moja ama nyingine imechangia mimi kumpata mwenza wangu Mung Chris.

Pia natoa rai kwa wale tuliokuwa tunasumbuana Pm,
Nimetwaliwa....natawaliwa.
Nagharamiwa sasa hv.

Ila baba Mung Chris punguza wivu, wabantu wa mizigo ndio asili yetu.
Utagombana na wangapi baba?
Cha muhimu ni kutunza heshima ya penzi na pendo letu.
Ila nami itabidi nipunguze manjonjo....kha!!!!

Nakupenda sana.
Can't wait kuvaa ring...
Soon najua inakuja.
I love you, no matter how and what!!!
Madame B.
2018
Umeamua kutumia shairi kufikisha ujumbe hongera
 
Nakutakia kila kheri mpwa na maisha mema wewe na chaguo la moyo wako......

Kumbuka nguzo kuu ya penzi imara ni kuvumiliana na kusameheana.....

Mungu awasimamie kwenye maisha yenu na uzao wenu
Asante sana mpwa wangu.
Tutayafuata yote na kuahidi kuyatimiza.

Wala hamtasikia tumeenda kinyume.
Asante sana nawe naomba uwe na amani, tuko salama na tunaheshimiana vilivyo.
Asante mpwa.
 
Kumbe ndugu yangu alishakukula?

Na hiyo RIP mbona sielewielewi?

Msalimie dadaako afu heshima ishike mkondo. Vinginevyo natoa siri zako kwa jamaa...

Mwambie dadaako aondoe sana nshanunua bastola
Hahahahha
We Asprin unaanza mbwembwe zako eeee.

Hayo yalishapita bhana, nitaanza kulia hapa.
Dada amesharudi kama shemeji, anaanza safari ya kulea kichanga.

Nenda Pm yake ila nakukumbusha tu, shem ile bastola yake kaenda kuikatia kibali tena, hivo kuwa makini.
Kipindi kile ulikoswa ila safari hii atapasua bichwa hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom