From Madame B to Mung Chris...

From Madame B to Mung Chris...

Madame B

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2012
Posts
31,841
Reaction score
37,579
Kwako Mung Chris kipenzi cha moyo wangu na tiba ya maradhi yangu sugu.
Ni siku, wiki, na hatimaye imetimu miezi mitatu tangu tuanze safari ya penzi letu tamu na lisilochuja hapa duniani tulilolianzisha hapa Jamii forums tarehe kama ya leo.
Na pia nakumbuka jinsi tulivyosumbuana hapa Jamii Forums kule Pm kila siku.
Usijali....(ile ilikuwa mitego yangu kukupima kiasi cha upendo wangu kwako).

Hakika sikutaraji kama nitaweza kupata mwenza wa kuweza kunituliza na kufanya niweze kuwa kiumbe kipya katika safari hii ya penzi tamu.

Sijutii kukupenda
Sijutii uamuzi wangu
Sijutii kuchaguliwa na wewe
Sijutii vile binadamu wanasema nini kunihusu mimi au wewe.
Ila kwangu utabaki kuwa mpenzi na baba bora wa mtoto wetu mtarajiwa.

Natamani nimalize hii ng'we salama ili niweze kupakata katoto kako kalikochanganya damu ya Kisambaa na Kichaga.
Nakupenda leo
Nitakupenda kesho na
Nitakupenda milele daima.
Labda mmoja wetu afariki.

Kila mmoja ana mapungufu yake, hakuna aliyekamilika kwa 100%
Kama kuna sehemu naendelea kukukosea naomba uwe muwazi na uniambie ukweli.
Hatuhitaji kuishia njiani.

Asante kaka mkuu Maxence Melo kwa kuanzisha mtandao huu kwani kwa namna moja ama nyingine imechangia mimi kumpata mwenza wangu Mung Chris.

Pia natoa rai kwa wale tuliokuwa tunasumbuana Pm,
Nimetwaliwa....natawaliwa.
Nagharamiwa sasa hv.

Ila baba Mung Chris punguza wivu, wabantu wa mizigo ndio asili yetu.
Utagombana na wangapi baba?
Cha muhimu ni kutunza heshima ya penzi na pendo letu.
Ila nami itabidi nipunguze manjonjo....kha!!!!

Nakupenda sana.
Can't wait kuvaa ring...
Soon najua inakuja.
I love you, no matter how and what!!!
Madame B.
2018
 
Ahsante Mama kijacho. I will always love you more than your expectation. May God bless our house.
Love you tooo baba mtarajiwa.
Upunguze utoto.
Unakuwa baba muda si mrefu
20180923_175809.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom