Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini

Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini

Hachelewi kubadilisha gia angani akawaletea janga maana hata mgombea urais aliwaahidi mtu makini nadhani matokeo yake ya kubadili gia angani mliyaona.
 
He is limited by the sample space available to choose from ... No miracle
 
Kwani mlimsafisha tayari lowasa mliomchafua miaka mingi? Nafikiri hajatakata bado tumieni JIKI
Chuki binafsi za ccm na kuhutaka uwaziri mkuu ndio uliaminisha umma wa watanzania kua Lowassa ni fisadi kumbe ni wongo na uzushi mkuu
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.

Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho.
“Sifa za Katibu Mkuu zinajulikana, nawaomba wanachama na wajumbe kutulia, jina watakutana nalo ukumbuni muda ukifika… nina imani litakuwa jina la mtu makini,” alisema.

Mbowe alisema chama hicho kinakutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka jana, hivyo wana mambo mengi ya kujadili, ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuwafikia wafuasi wao.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kitamtambulisha Katibu Mkuu mpya rasmi Jumapili wakati wa mkutano wa hadhara utakaofanyika viwanja wa Furahisha jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, alisema majina mawili yatawasilishwa katika Baraza Kuu litakalokaa usiku wa Jumamosi kwa ajili ya kupitisha jina moja.

Alisema majina yatakayowasilishwa hayatakuwa na uhusiano au urafiki wowote na Mwenyekiti Mbowe.

“Tayari viongozi wa kitaifa wamewasili Mwanza, Sekretarieti imekutana kwa ajili ya kuandaa ajenda ambazo zitajadiliwa na Kamati Kuu yenye wajumbe 36.

“Siku inayofuata Baraza Kuu litakaa usiku kwa ajili kumpata Katibu Mkuu, hii ni nafasi nyeti sana ndiyo maana hata wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafuatilia kwa ukaribu kujua nani atapewa mikoba ya Dr Slaa.
ccm haitamsahau Mbowe milele , yaliyotokea uchaguzi mkuu ni siri ya lubuva .
 
Ina maana huyu Supreme Leader ana jina la Katibu Mkuu tayari mfukoni!!???? WanaSiasa wanatupeleka Watanzania pabaya sana. Nina shemeji yangu mmoja wanagombana na MKE wake kila mara kwa kuwa Jamaa ni Ukawa na mama ni CCM.
Unajua kilichotokea Dodoma?
ccm haitamsahau Mbowe milele , yaliyotokea uchaguzi mkuu ni siri ya lubuva .
Nabaado watajuta sana maana ndio tumeanza
 
Mnaeleweka sana mbona ugaidi ndio sera zenu au mmesahau kuwavisha vijana wenu miwani na mapanga kuweni makini safari hii ni magufuli sio jk
Hapa kazi tu....
kujilinda ni haki ya kikatiba , halafu huu uzushi wa ugaidi unaouleta hapa utakuponza sana , muulize mwigulu .
 
Demokrasia iko wapi? Kwanini mbowe ndio ateue mtu, na kuna wa kumpinga kweli? Kwanini wasiachie wanachama wajitose kugombea na wapigiwe kura. Atachagua mchaga na wachaga wote cdm watamkubali bila tabu yeyote.
 
Huo huo ushaidi mnaosema Lowassa ni fisadi wakati hamna huo ushaidi
Mlikuwa mnaiga eeh mimi sio mfuasi wa siasa chafu nabishana kwa hoja hamuwezi kuwa mnafuata mkumbo wakisema mkeo mzinifu nawe unasema ndio! Wakisema tulikuwa tunatania nawe unakubali pia!!! Huo ni utoto
 
Kwa taarifa nilizonazo za uwakika ni kwamba aliyekuwa mbunge wa Kahama James Lembeli ndio katibu Mkuu mtarajiwa. Kwa hili naomba niwapongeze watani zangu kwa kupata jembe.

Kwa hakika James Lembeli ana uwezo kama Dr. Salaa na pengine ana uwezo mkubwa kuliko Dr. Slaa....
 
Back
Top Bottom