Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.

Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho.
“Sifa za Katibu Mkuu zinajulikana, nawaomba wanachama na wajumbe kutulia, jina watakutana nalo ukumbuni muda ukifika… nina imani litakuwa jina la mtu makini,” alisema.

Mbowe alisema chama hicho kinakutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka jana, hivyo wana mambo mengi ya kujadili, ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuwafikia wafuasi wao.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kitamtambulisha Katibu Mkuu mpya rasmi Jumapili wakati wa mkutano wa hadhara utakaofanyika viwanja wa Furahisha jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, alisema majina mawili yatawasilishwa katika Baraza Kuu litakalokaa usiku wa Jumamosi kwa ajili ya kupitisha jina moja.

Alisema majina yatakayowasilishwa hayatakuwa na uhusiano au urafiki wowote na Mwenyekiti Mbowe.

“Tayari viongozi wa kitaifa wamewasili Mwanza, Sekretarieti imekutana kwa ajili ya kuandaa ajenda ambazo zitajadiliwa na Kamati Kuu yenye wajumbe 36.

“Siku inayofuata Baraza Kuu litakaa usiku kwa ajili kumpata Katibu Mkuu, hii ni nafasi nyeti sana ndiyo maana hata wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafuatilia kwa ukaribu kujua nani atapewa mikoba ya Dr Slaa.
 
Aaah mbowe safari hii akichanga karata kinafiki atapinduliwa na katibu wake bora amweke mchaga mwenzie
 
Hamna kitu mwaka jana aliahidi kutuletea mgombea urais makini na wala sio kapi toka ccm...kufumba na kufumbua anatuletea lowassa huku sumaye na kingunge wakiwa wazungumzaji wakuu...afanye atakalo chama cha mkwewe.
 
Hata akiwa uozo, sikutegemea angesema naleta katibu uozo! Hata hivyo hii ni safu anaiandaa ya 2035, maana 2020 hawana chao na 2035 kama spidi itaendelea, mtu sahihi atakuwa Majaliwa.
 
Tunamsubiri huyo Katibu Mkuu makini.
Tafadhali usituletee mroho wa madaraka,mnafiki na kigeugeu kama aliyejiuzulu.
Chama kinahitaji mtu makini atakayekijenga chama kuelekea 2020.
Kila la kheyr.
Alete mpiga dili...akiambiwa tupige hela asilete kauzibe!
 
Kesho ndo siku pekee ya kukata ngebe na dhihaka za CCM kutupachika jina la "NYUMBU"

C'mon comrade MBOWE usitubadilishie gia angani tena this time.
 
Back
Top Bottom