Freeman Mbowe na kupanda na kushuka kwa CHADEMA!

vladimir_lenin_about_the_oppress_by_vladimirseyer-d7c6j8z.jpg
 
Asante Wille kwa uchambuzi makini..

Wachangiaje wengi wa bavicha kama kawaida yao watakuja na matusi au hoja za kitoto kisa hawataki kuambiwa ukweli!
Hoja ya msingi ni mbowe kuachia ngazi maana chadema kwa sasa hakina mashiko kwa wananchi na upinzania hauna nguvu kama miaka kadhaa iliyopita..

Utawala mpya na aina za siasa kwa sasa inawataka wabadilike..Upinzania una nafasi kubwa sana kwa maendeleo ya nchi lakini unapokosa nguvu ni wazi ccm inaweza pia kukosea kwenye baadhi ya maeneo na tusipate mawazo mbadala wa kuwaweka sawa!

Zama za Mbowe zimefika tamati na kamali zake ni wazi ameliwa kekundu na akina lowasa..Kukosea sio kosa ila kosa ni kurudia kosa!Kuendelea kuwakumbatia akina lowasa, Sumaye et al ni kosa zaidi wanaloendelea kulifanya..

1.Kwanza wawaondoe akina Lowasa na genge lake na wakiri kuwa walikosea bila kumung'unya maneno ikiwezekana a list of shame irudi hewani kwenye media!
2. Pili Mbowe ajiuzuru na kusuka chama upya hasa safu ya uongozi..Mpaka kufikia 2020 (Miaka 4 iliyobaki) naamini muda unawatosha kukijenga chama kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa..
3. Wajikite kwenye masuala ya msingi hasa kiuchumi kuikosoa serikali ya sasa hasa kwa kufanya siasa kwenye majimbo yao kwa kutumia madiwani, mameya na wabunge na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo hasa kiuchumi..Waachane na siasa za mihemko au maandamano na kauli za viongozi kama ajenda zao kuu!
4. Warudi kwa Dr. Slaa na kumuomba radhi ili arudi kukinusuru na kukijenga chama upya..Bado naamini Slaa ni mpinzani bora, genuine kuwahi kutokea na mwenye mikakati mizito kwa upinzani..
mkuu swali langu linarudi palepale mnatumia takwimu gani kuback up ur claims kuwa chadema haina mashiko tena mbele ya wananchi?? maana kma ni uchaguzi last year chadema imekuwa compared to 2010.... naombeni mruhusu shughuli za kisisasa ndio tutapata majibu sio sahvi mmetufunga minyororo afu unasema TUMEISHIWA PUMZI.....
 
Mm namuhamini sana mbowe sana turimujuwa chacha bobu wangwe kupitia mbowe turimujuwa zito kabwe kupitia mbowe turimujuwa john munyika kupitia mbowe arima mdee kupitia mbowe turimujuwa tundu risu kupitia mbowe nashanga unatoa oja kwa kumpinga mbowe unatoka wapi
Wewe hivi umeandika nini hapa???????
 
Mkuu Wille Malecela

Hapa Umejenga hoja za msingi sana

Hongera sana kwa hilo

You have brains sometimes..Kudos

Nakubaliana na wewe kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa sana CHADEMA lakini hadi sasa amefika mwisho wa uwezo wake....Hawezi kufanya cha zaidi na tofauti

Wasiwasi wangu ni Je....Nani anapaswa kupewa hiyo kazi kubwa ya kukikarabati chama?

Na je Mbowe kutokana na sacrifice aliyoifanya hadi CHADEMA kufika hapo atakuwa tayari kukiacha chama ?

Na je ....Kuna Process zozote zinazoonesha kuna SUCCESSION PLAN ambayo iko Inaishi ndani ya CHADEMA

Again wille...Thanks kwa hoja nzuri

cc Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji
Kuntu...hapo kwenye 'sucession plan' ndio issue....kwani wameshajikwaa kwa katibu mkuu.
 
Asante Wille kwa uchambuzi makini..

Wachangiaje wengi wa bavicha kama kawaida yao watakuja na matusi au hoja za kitoto kisa hawataki kuambiwa ukweli!
Hoja ya msingi ni mbowe kuachia ngazi maana chadema kwa sasa hakina mashiko kwa wananchi na upinzania hauna nguvu kama miaka kadhaa iliyopita..

Utawala mpya na aina za siasa kwa sasa inawataka wabadilike..Upinzania una nafasi kubwa sana kwa maendeleo ya nchi lakini unapokosa nguvu ni wazi ccm inaweza pia kukosea kwenye baadhi ya maeneo na tusipate mawazo mbadala wa kuwaweka sawa!

Zama za Mbowe zimefika tamati na kamali zake ni wazi ameliwa kekundu na akina lowasa..Kukosea sio kosa ila kosa ni kurudia kosa!Kuendelea kuwakumbatia akina lowasa, Sumaye et al ni kosa zaidi wanaloendelea kulifanya..

1.Kwanza wawaondoe akina Lowasa na genge lake na wakiri kuwa walikosea bila kumung'unya maneno ikiwezekana a list of shame irudi hewani kwenye media!
2. Pili Mbowe ajiuzuru na kusuka chama upya hasa safu ya uongozi..Mpaka kufikia 2020 (Miaka 4 iliyobaki) naamini muda unawatosha kukijenga chama kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa..
3. Wajikite kwenye masuala ya msingi hasa kiuchumi kuikosoa serikali ya sasa hasa kwa kufanya siasa kwenye majimbo yao kwa kutumia madiwani, mameya na wabunge na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo hasa kiuchumi..Waachane na siasa za mihemko au maandamano na kauli za viongozi kama ajenda zao kuu!
4. Warudi kwa Dr. Slaa na kumuomba radhi ili arudi kukinusuru na kukijenga chama upya..Bado naamini Slaa ni mpinzani bora, genuine kuwahi kutokea na mwenye mikakati mizito kwa upinzani..
Inastaajabisha sana kwa wafuasi wa chama fulani kutamani chama kinachowatoa jasho na kuwanyima usingizi kifanye mabadiliko katika uongozi wake ili kiweze kujiimarisha. Hii ni ajabu sana kwani hata katika ulimwengu wa ngumi bondia huwa anapitia mikanda ya bondia atakaye kwenda kupambana nae ili apate kujua udhaifu wake mapema na apange namna ya kumkabili kabla ya siku ya pambano.Sasa ni maajabu kuona watu wa CCM wakifanya tathmini ya mapungufu ya kimkakati na kiuongozi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kushauri wapinzani wao watafute mbadala wa Mheshimiwa Mbowe ili kujiimarisha wapate kupigwa siku ya pambano
 
Acha kutetea mafisadi wewe
Hao GSM ni wakwapuaji wakubwa wa uchumi wa Taifa hili. Wamehujumu sana hii Nchi wakati wa utawala wa JK kwa Kampuni yao ya Home Shopping Centre..
Hapo ndio unapojidhalilishaga kwenye kutetea upuuzi.
Kama unavyomtetea Makonda kila siku..
Hopeless.

- Halafu GSM akijiunga na Chadema kama Lowassa mtasema nini au mmesahau Lowassa alipokuwa Fisadi mpaka alipojiunga na nyinyi mkasema hamna ushahidi hahahahahahaha

le Mutuz
 
- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
Inahitaji akili kubwa kuelewa andiko lako mkuu,lakin najua watakuja kukudhihaki na hoja zao dhaifu
 
Du! Kwa akili hii inaonyesha wazi ndo maana mkuru alimtumbua mama furani ktk ukuu wa mkoa ndani ya Siku 27 za uteuzi wake. Mwanzoni nilifikiri kaonewa lkn kwa mada kama hii kutoka kwako sasa sishangai tena. Kwani ni akili duni za ujengaji wa hoja.
Kama kweli chadema ni dhaifu kwann mnawaogopa? Kwann wasipewe nafasi ya kupanda mjukwaani kama mnavyofanya ninyi kupitia serikali ili wote tuone udhaifu huo? AKILI NI ZAO LA URITHI KUTOKA KWA WAZAZI WAWILI. Umethibitisha hilo

- Siku ukiona nimeingai hapa kwa majina ya bandia kama wewe ujue nitakuwa nimefilisika mawazo kama wewe so far bado, siku ukiweza kuwa na akili kubwa kama mimi utaingia kwa jina lako kama mimi, hahahahahahahaha pole sana

le Mutuz
 
Inahitaji akili kubwa kuelewa andiko lako mkuu,lakin najua watakuja kukudhihaki na hoja zao dhaifu

- Hapana huwa wanapoteza muda unashindana vipi na mtu anayetumia majina ya bandia? hahahahahaha nani anaweza kumsikiliza mtu anayetumia majina ya bandia kudai ukweli? hahahahahahha

le Mutuz
 
Okay, pale adui anapokuambia ukinipiga kwa silaha hii umeniua, wakati huo huo anakwambia hizo ulizonazo haziwezi kufanya kitu (huku amekuwekea zuio la kuzitumia hizo ulizo nazo).
 
- Siku ukiona nimeingai hapa kwa majina ya bandia kama wewe ujue nitakuwa nimefilisika mawazo kama wewe so far bado, siku ukiweza kuwa na akili kubwa kama mimi utaingia kwa jina lako kama mimi, hahahahahahahaha pole sana

le Mutuz
Swala si Nina LA bandia au la, hapa ni kujibu hoja.
Kama chadema ni dhaifu hivyo kwann msiruhusu ifanye siasa kama ninyi mnavyofanya kupitia serikali ili sisi wote tuone udhaifu huo.
Mara ngapi viongozi wa chadema wamezuiwa kufanya siasa na kutumia majukwaa kutoa hoja na kutafuta wanachama wapya?
Mbona hoja ni nyepesi, mwambieni mkuru awache milango wazi kwa siasa za usawa na ukweli utajidhiri.
 
Ni vigumu kumtathmini Mbowe kwa wakati huu kwani chuki za watawala zidi ya upinzani, katiba mbovu na ukweli kwamba bado tuna chamadola vimeathiri siasa za upinzani. Wapinzani wakiwa wamebanwa tunaona kuzuka kwa jamaa yule na wengine kama yeye ndani ya upinzani ili kudhoofisha upinzani. Swali langu lingekuwa "Je upinzani una viongozi wanao weza kupambana na hali hii?"
 
Bado mnaendelea na kampeni ya Mbowe kuwapisha vijana!!!
Yupo kijana ndani ya upinzani, alipigiwa debe ili akamate nafasi ya Mbowe ikashindikana, akapata nafasi kwenye chama kingine cha upinzani.
Vipi hali ya hicho chama kinachoongozwa na huyo kijana wetu? Kinapiga hatua ya kukua zaidi?
 
- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
Kama nimekuelewa, umejenga hoja yako kwa kutumia jambo moja tu-Chadema kuwakaribisha Lowasa na Sumaye. Sasa kama niko sahihi nasita kukubaliana na wewe kwa kuwa hujatuonyesha facts ambazo zinatengeneza msingi wa hitimisho lako. Kwamba umeshindwa kutuonyesha anguko la Chadema/Mbowe huko mbele kutokana na presence ya Lowasa na Sumaye ndani ya Chadema.

Lakini wenzako wengine hawaamini kama unavyoamini wewe, wanaamini kinyume chake. Ni hao ambao wanatumia rasilimali za nchi kuhakikisha kuwa Lowassa na Chadema yenyewe hawafanyi siasa hadi 2020. Sasa hili linatupeleka mahali pa kupima unabii wa nani uko sahihi; wako wewe au wa wale ambao wanaiona dhoruba inayoweza kusababishwa na Lowassa akiwa ndani ya Chadema na kuamua kumdhibiti mapema?

Mtazamo wangu ni kwamba bado Mbowe anafikiri sawa sawa, na pengine kwa mazingira ya siasa za kipindi hiki anahitajika zaidi Chadema. Jambo muhimu la kuzingatia hapa ni kwamba tumeondolewa, labda kwa muda, fursa ya kweli ya kufanya analysis ya siasa za vyama na viongozi wake. Hivyo, waathirika katika zuio la kufanya siasa hadi mwaka 2020 itakuwa ni pamoja na wewe, kwani andiko lako katika mazingira tuliyo nayo linakosa mashiko!
 
Uko ulingoni mpinzani wako umemfunga mikono na macho umemfunga kitambaa,na refa ni wewe utategemea matokeo gani?
 
Huwa nasikia sana watu wakikuponda.
Umejenga hoja nzito ambazo mwenye akili atakuelewa. Najua wengi watakuchukulia kuwa wewe ni ccm, ila wanakuelewa vzr.

Tatizo la chadema hawawezi simamia ajenda, hawabadiliki kulingana na wakati.Mbinu wanazotumia ni zilezile za kale, hawajui dunia imebadilika.

Gharama za kufanya mikutano nchi nzima zinatosha kuwa na media zenu mfano refio, magazeti na mitandao ya kijamii.

Lkn hilo hamliwazi kazi yenu kulalamika eti clouds media ni ccm, hamjui media ni biashara???

Niliwahi sema humu sana lkn mwisho wa siku unaonekana msaliti, au ccm.

Chadema inabidi ijitazame upya, ni wakati wa mbowe kuandaa vijana ambao watakuwa na good plan.
Tatizo la viongozi wetu wanang'ang'ania madaraka, mwisho wa siku wakiachia chama kinakuwa hakina nguzo imara zilizojengwa kusimamia ajenda za chama kushika dola.

Nafasi ya katibu mkuu imepwayaa.
Kinachoibeba chadema sasa ivi ni Lowassa.
Siku lowassa akipotea na chadema kwishaa.

Leo Lema anasimama na kuropoka kauli za kihuni, yani anafikiri nchi inaendeshwa kwa hisia zake.

Nimeamua kuachana na siasa za kushabikia chama, natamani siku itokee jeshi likamate nchi.

CCM ni mbovu, chadema ni dhaifu, sijui twende wapi??
Twende Wazalendo
 
Back
Top Bottom