Freeman Mbowe na kupanda na kushuka kwa CHADEMA!

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,216
2,000
- Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Hii ndiyo aya niliyoikubali kabisa, hata hivyo si tayari Mbowe ameshamuachia Lowasa chama?
 
General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,699
2,000
Huwa nasikia sana watu wakikuponda.
Umejenga hoja nzito ambazo mwenye akili atakuelewa. Najua wengi watakuchukulia kuwa wewe ni ccm, ila wanakuelewa vzr.

Tatizo la chadema hawawezi simamia ajenda, hawabadiliki kulingana na wakati.Mbinu wanazotumia ni zilezile za kale, hawajui dunia imebadilika.

Gharama za kufanya mikutano nchi nzima zinatosha kuwa na media zenu mfano refio, magazeti na mitandao ya kijamii.

Lkn hilo hamliwazi kazi yenu kulalamika eti clouds media ni ccm, hamjui media ni biashara???

Niliwahi sema humu sana lkn mwisho wa siku unaonekana msaliti, au ccm.

Chadema inabidi ijitazame upya, ni wakati wa mbowe kuandaa vijana ambao watakuwa na good plan.
Tatizo la viongozi wetu wanang'ang'ania madaraka, mwisho wa siku wakiachia chama kinakuwa hakina nguzo imara zilizojengwa kusimamia ajenda za chama kushika dola.

Nafasi ya katibu mkuu imepwayaa.
Kinachoibeba chadema sasa ivi ni Lowassa.
Siku lowassa akipotea na chadema kwishaa.

Leo Lema anasimama na kuropoka kauli za kihuni, yani anafikiri nchi inaendeshwa kwa hisia zake.

Nimeamua kuachana na siasa za kushabikia chama, natamani siku itokee jeshi likamate nchi.

CCM ni mbovu, chadema ni dhaifu, sijui twende wapi??
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
8,911
2,000
Hizi tabiri zimeshazoeleka. Kabla ya 2015 kuna waliosema ni chama cha msimu na wengine wakasema kingekufa....lakini sote tulishuhudia chama tawala kilivyotolewa "kamasi" kwenye uchaguzi wa 2015! Tumeona ya Jecha kule visiwani (dhidi ya CUF).

Kusema CDM/upinzani unaenda kufa au unafifia ni matusi kwa kiongozi anayezuia vyama vya siasa kufanya siasa kwa uhuru maana ni sawa na kumwambia anaogopa kitu kisichokuwepo. Sote tulishuhudia operesheni UKUTA ilivyowatia kiwewe watawala mpaka wakafikia kubuni maadhimisho ambayo hayana hata mantiki. Askari wetu walifanyishwa mazoezi ya 'kawaida' ambayo inashangaza nayo yamepotea baada ya UKUTA kuahirishwa.

Nimeona "mamvi" ameanza ziara, soon watawala wataanza kuogopa!
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
Mkuu Wille Malecela

Hapa Umejenga hoja za msingi sana

Hongera sana kwa hilo

You have brains sometimes..Kudos

Nakubaliana na wewe kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa sana CHADEMA lakini hadi sasa amefika mwisho wa uwezo wake....Hawezi kufanya cha zaidi na tofauti

Wasiwasi wangu ni Je....Nani anapaswa kupewa hiyo kazi kubwa ya kukikarabati chama?

Na je Mbowe kutokana na sacrifice aliyoifanya hadi CHADEMA kufika hapo atakuwa tayari kukiacha chama ?

Na je ....Kuna Process zozote zinazoonesha kuna SUCCESSION PLAN ambayo iko Inaishi ndani ya CHADEMA

Again wille...Thanks kwa hoja nzuri

cc Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji
 
Aug 31, 2016
43
95
Mm namuhamini sana mbowe sana turimujuwa chacha bobu wangwe kupitia mbowe turimujuwa zito kabwe kupitia mbowe turimujuwa john munyika kupitia mbowe arima mdee kupitia mbowe turimujuwa tundu risu kupitia mbowe nashanga unatoa oja kwa kumpinga mbowe unatoka wapi
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,605
2,000
- GSM na Clouds ni wafanya biashara, GSM wanakodisha Malori yao na Clouds unalipia matangazo kurushwa live, so rekebisha kauli yako mkuu.

le Mutuz
Kwa kutumia jina la rais matapeli wamiliki Wa Home shopping centre walifilisika na kuja na njia mpya ya kukwapua Mali za watanzania .

Wasitumie jina la Rais Wa nchi tafadhari wezi wakubwa hao..
 
dikembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,646
2,000
Siku zote mpiga filimbo haisikii kelele ya filimbi. mwache aendelee kuwa kocha wa upinzani wakati yeye yalimkuta miezi michache iliyopita. sipendi kuzungumzia kifo cha kisiasa cha jina lake la pili, napenda kusoma tabiri zake za kifo cha chama baki.
 
valuablecock

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
782
1,000
- GSM na Clouds ni wafanya biashara, GSM wanakodisha Malori yao na Clouds unalipia matangazo kurushwa live, so rekebisha kauli yako mkuu.

le Mutuz
Nani asiejua kuhusu uchafu wa GSM? Au kwasababu waliwasaidia katika campaigns na sasa wanatakasa pesa katika CSR? Watumbueni basi tuone kama mnamaanisha mnayo hubiri.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
681
500
Le Mutuz
You might be right or wrong according to what you see, say, and write depending on the school of thought which you belong. Ili tumpime Mbowe vizuri na either tukubaliane au kupingana na hoja zako kuna mambo ya msing ya kuangalia. Tangu JPM ameingia madarakani ameminya kwa makusudi uhuru wa habari na uhuru wa shugguli za kisiasa kwa wapinzani wake huku ccm ikipokea wanachama wapya kila uchao. Ni muhimu basi kumshauri kwanza JMP aendelee kupambana na ufisadi bila kuingilia uhuru wa wengine hiyo itatupa nafasi ya kupima shuguli za Mbowe na kuridhika pasipo shaka kama bado anafaa au aende mgombani. Wengine tunaona kama vile chadema haina katibu mwenye uwezo kama wa mzee wetu yule aliyelala mbelezeeee, lakini pia kama mkuu wa nchi amezuia shuguli za kisiasa kinyume na katiba unawezaje ku-conclude kwamba Mbowe hana jipya tena?? Mwambie Magu jamaa yule muungwana na mfanyakazi wa Nyanza wa zamani arudishe uhuru wa watu kisha tupime siasa za nchi yetu mind you sijawahi kuwa mwanachama wa upinzani

- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom