Freeman Mbowe na kupanda na kushuka kwa CHADEMA!

Mkuu Wille Malecela

Hapa Umejenga hoja za msingi sana

Hongera sana kwa hilo

You have brains sometimes..Kudos

Nakubaliana na wewe kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa sana CHADEMA lakini hadi sasa amefika mwisho wa uwezo wake....Hawezi kufanya cha zaidi na tofauti

Wasiwasi wangu ni Je....Nani anapaswa kupewa hiyo kazi kubwa ya kukikarabati chama?

Na je Mbowe kutokana na sacrifice aliyoifanya hadi CHADEMA kufika hapo atakuwa tayari kukiacha chama ?

Na je ....Kuna Process zozote zinazoonesha kuna SUCCESSION PLAN ambayo iko Inaishi ndani ya CHADEMA

Again wille...Thanks kwa hoja nzuri

cc Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji
Hakuna kitu alichojenga hapo huyu ccm mwenzenu nyote ni mashahidi jinsi ccm walivyofurushwa na mchaka mchaka wa uchaguzi mkuu mpaka wakafika mahali kwa kutumia Dola wakawakamata mawakala wa Lowassa pamoja na kituo cha haki za binadamu kilichopo Mbezi siku mbili au tatu kabla ya kutangaza matokeo bila hivyo ccm kwisha walishashindwa uchaguzi, kama hawakushindwa hayo yote ya nini? Je kama haki ingetendeka leo mgesema Chadema inaenda kufa? Mimi nasema hata ikifa chanzo ni serikari oga ya Ngosha anazuia wengine mechi yy anajitengenezea mechi kila siku hivi kweli mchezaji anayecheza kila siku atakuwa sawa na ambaye yako benchi kiuwezo hata kama wanacheza namba moja ya umwenyekiti au ujumbe ktk halimashauri kuu au kamati kuu?
 
- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
Hapa badala ya kuja kujikita kujibu hoja nzito Lemutuuz watakuja na matusi hapa
 
Kila uchaguzi unapofika CHADEMA wanazidi kujiongezea kura za urais,majimbo yanaongezeka na majimbo mengi yanayochukuliwa na CHADEMA ni yale yaliyokuwa yanaongozwa na CCM,uchaguzi uliopita ndiyo usiseme kabisa,CHADEMA chini ya Mbowe imeacha kilio kikubwa sana Lumumba kwa kuwa pongezi CCM ruzuku kiasi cha kuwafanya wafanyakazi wa vyombo vya uhuru suruali ziwadondoke hovyohovyo kwa kuwa mikanda haibani,kwenye kura za urais ndiyo basi,mzee wa nusu karne bila kutumia miundo mbinu mbadala alikuwa amegaragazwa.

Kwa mafanikio haya ya CHADEMA chini ya Mbowe sijui ni ya kushuka au kupanda?kati ya CCM chama ambacho kila uchaguzi unapofika ni lazima wabunge wake wapunguzwe,kura za urais zipunguzwe,ruzuku ipunguzwe na CHADEMA ambayo imeifanya CCM kuwa mtaji wake wa kujiongezea kura nina anaye poromoka hapo?.
 
Huwa nasikia sana watu wakikuponda.
Umejenga hoja nzito ambazo mwenye akili atakuelewa. Najua wengi watakuchukulia kuwa wewe ni ccm, ila wanakuelewa vzr.

Tatizo la chadema hawawezi simamia ajenda, hawabadiliki kulingana na wakati.Mbinu wanazotumia ni zilezile za kale, hawajui dunia imebadilika.

Gharama za kufanya mikutano nchi nzima zinatosha kuwa na media zenu mfano refio, magazeti na mitandao ya kijamii.

Lkn hilo hamliwazi kazi yenu kulalamika eti clouds media ni ccm, hamjui media ni biashara???

Niliwahi sema humu sana lkn mwisho wa siku unaonekana msaliti, au ccm.

Chadema inabidi ijitazame upya, ni wakati wa mbowe kuandaa vijana ambao watakuwa na good plan.
Tatizo la viongozi wetu wanang'ang'ania madaraka, mwisho wa siku wakiachia chama kinakuwa hakina nguzo imara zilizojengwa kusimamia ajenda za chama kushika dola.

Nafasi ya katibu mkuu imepwayaa.
Kinachoibeba chadema sasa ivi ni Lowassa.
Siku lowassa akipotea na chadema kwishaa.

Leo Lema anasimama na kuropoka kauli za kihuni, yani anafikiri nchi inaendeshwa kwa hisia zake.

Nimeamua kuachana na siasa za kushabikia chama, natamani siku itokee jeshi likamate nchi.

CCM ni mbovu, chadema ni dhaifu, sijui twende wapi??
Nimekuelewa mkuu ni ss wachache sana wanaweza kukubali
 
kwani lemututz nini kigezo cha kushuka CDM Chini ya Mbowe? ninavyo jua ...Kwa ujasiri mbowe amekiongoza chama kwa ujasiri mkubwa sana na mwaka jana wakati wa uchaguzi walifanya maamuzi mazuri kuunganisha nguvu kuunda ukawa. juu ya kuhujumiwa na ccm lakini ni ukweli usio pingika uongozi wake ulifanukisha cdm kupata wabunge wengi zaidi ya chaguzi zilizo pita . kura za mgombea wa ukawa ni zaidi ya 40% sawa na 6 m kura na huku ushindi wa ccm ukiwa ni 8m ...tofauti ya kura 2m tu ..na hizi ukijumlisha za wizi , na zile za vijijini ambako upinzani unashindwa kufikia kutokana na fedha na muda wa kufikia maeneo yote. pia hawa 2m ni wale ambao wako less informed kuhusu siasa za Tz wengi wao bado wanadhani chama ni cha nyerere tu..hata kama kinavurunda.

hivyo ushauri wako sio sawa kwa sababu cdm imepata mafanikio makubwa na imekubalika maeneo yote ya mijini ambako watu ni well informed.
Dar waliichukua chini ya mbowe
Iringa
Mbeya
Moshi
Arusha
Tanga
hata Mwanza juu ukabila ulitumika lakini jiji hilo ni moja katika ngome kubwa ya cdm.
amejitahi na bado ana uwezo mkubwa wa kuongoza, kinachotakiwa sana ni kuona UKAWA unaimarika zaidi , ccm kupigana nayo peke yake ni ngumu ni chama dola na inatumia kila silaha at their disposal hata haram
sasa ushauri kwa mbowe ni kuona ukawa inasimama kwa nguvu zaidi na kufanya tathmini ya uchaguzi kisayansi kuona nini kilipita hata wakakosa baadhi ya majimbo na wapi walikosea hadi kura 2m zikaenda kwa magufuli. huo ndio ushauri wakiufanya kazi na kuja na recomandations basi ni wazi mbowe ataona 2020 ukawa ukiingia madarakani juu ya vitisho watavo kabilina navyo
 
Una tatizo la kuwa incoherent kwenye analysis zako. You are all over the place, umeanza kama unataka kujadili uwezo wa Mbowe kama kiongozi, then unahitimisha kwamba hakuna upinzani serious dhidi ya Chama tawala. Hapohapo tena umefananisha kinachoendelea ndani ya Chadema kwa sasa na Chama cha Democrats cha Marekani. Seriously? Sasa kama unasema Chadema haiwezi kuwa upinzani thabiti dhidi ya CCM unawezaje kuifananisha Chadema na Democratic party ya USA. Hakuna mantiki hapo. Maana inafahamika kwamba, kwanza, Democrats wamepata popular votes almost milioni mbili zaidi ya Republicans walioshinda chaguzi karibu katika kila ngazi ya chaguzi za USA awamu hii.

Sure, Democrats walishindwa kwenye electoral votes, kwa ngazi ya urais, na uwezekano wao kurudi madarakani hivi karibuni bado mkubwa sana tu. Sasa huwezi kuwafananisha na Chadema ambao hawajawahi kushinda majority votes Tanzania kwa ngazi za chaguzi zote tangu wazaliwe kama Chama. Isitoshe, kupotea kimaono kama chama au mtu mmoja mmoja ni kitu cha kawaida sana, na haimaanishi kwamba chama ndo kimepotea forever. Hivi unajua hata CCM walipotea sana kimaono kwa muda mrefu sana tu, mpaka angalau sasa unaona vision ya CCM kupitia Magufuli, ambaye unaweza kumkosoa kwenye tactics anazotumia kufikia vision yake lakini vision yake ipo fairly clear: kusafisha uchafu ulioachwa na watangulizi wake wakiwemo wakina Malecela, Sumaye, Lowassa etc.
 
Hivi wewe na Shigongo ni nani mwenye media coverage kubwa ya kuchafuwa watu?

Kamuulize alipokwenda kudai madeni hewa Lumumba aliambulia mini kama si chupa ya maji ya Kilimanjaro?
Au bado unaota Anna Kilango atapangiwa kazi nyingine?
 
Kosa kubwa la Mbowe na Chadema ni kumkaribisha Lowassa. Wataumia sana na kujuta lakini hawatafanikiwa hadi waachane naye
 
Eti kashuka kiwango! Mbowe ni sawa na bondia maarufu ambaye akipanda jukwaani mnamfunga miguu kisha mnatangaza kashuka kiwango mbona anashindwa Ku dance wakati wa pambano.
Mnamzuia kufanya siasa majukwaani kisha mnamtungia kuwa kashuka kiwango? Aliyeshuka kiwango ni kama mzee Malecela ukimlinganisha na PMs waliopita kiasi cha kujipendekeza walao mama arudishwe kazini. Ramli hizi zinegonga ukuta
 
This kind of discourse would have had substance had we been living in a state with some good measure of rationality. But, then, we're in a totalitarian state where all systems are rigged against dissent and the rush to exceed in applauding the rulers while trashing the opposition is the norm for the self-made "analysts" who are just after the odd opportunity. Whatever the argument, opposition politics and politicians stand no chance in Tz as to allow credible analysis of the same.
 
Eti kashuka kiwango! Mbowe ni sawa na bondia maarufu ambaye akipanda jukwaani mnamfunga miguu kisha mnatangaza kashuka kiwango mbona anashindwa Ku dance wakati wa pambano.
Mnamzuia kufanya siasa majukwaani kisha mnamtungia kuwa kashuka kiwango? Aliyeshuka kiwango ni kama mzee Malecela ukimlinganisha na PMs waliopita kiasi cha kujipendekeza walao mama arudishwe kazini. Ramli hizi zinegonga ukuta
Hata bondia maarufu na tishio Mike Tyson alishuka kiwango na akapewa kichapo.....
 
- Halafu GSM akijiunga na Chadema kama Lowassa mtasema nini au mmesahau Lowassa alipokuwa Fisadi mpaka alipojiunga na nyinyi mkasema hamna ushahidi hahahahahahaha

le Mutuz
Mahakama ya mafisadi si imeshakamilika kama ni fisadi mpelekeni mahakani sio kusema fisadi halafu hamuchukui hatua yoyote, Na kama hamuwezi kumshtaki bora mkae kimya sio kumuita mtu fisadi halafu huna hata ushaidi.
 
Umejitahidi kuwa convince waliokutuma kwamba pesa waliyokupatia has been properly accounted for. One thing you have forgotten is to advise your don to obey the law and govern by using the constitution. Mwambie afanye hivyo muone moto wake. Kwa mfano kutumia bwana yule kujaribu kumdhoofisha maalim hakuwasaidii sana bali huwadhoofisha kwenye macho na ufahamu wa mwenye akili za kawaida tu
 
- Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa. Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama hicho kilipo sasa hoi bin taabani.

- Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM, kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.

- Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho wanashindwa kuielewa hiyo concept.

- Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika kukifanya yaani Upinzani.

- Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa au kuja kujutia baadaye.

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Le Mutuz Nation
Afadhali hilo umeliona. Bora yeye aliwekeza kwa social media na Chama kikakubalika.
Chama tawala chakubalika kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom