Nakubaliana na wewe kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa sana CHADEMA lakini hadi sasa amefika mwisho wa uwezo wake....Hawezi kufanya cha zaidi na tofauti
Wasiwasi wangu ni Je....Nani anapaswa kupewa hiyo kazi kubwa ya kukikarabati chama?
Na je Mbowe kutokana na sacrifice aliyoifanya hadi CHADEMA kufika hapo atakuwa tayari kukiacha chama ?
Na je ....Kuna Process zozote zinazoonesha kuna SUCCESSION PLAN ambayo iko Inaishi ndani ya CHADEMA
Again wille...Thanks kwa hoja nzuri
[/USER]
Mkuu nianze na hoja yako ya mwisho. Hili la succession plan
Baada ya uchaguzi tulisema,KUB awe mtu mwingine kama succession plan
Pili, vijana wapewe nafasi ya kutumia talent zao. Hiyo ni succession plan.
Muundo wa kupata viongozi ubadilike. K/mkuu iwe nafasi ya kuomba
Matokeo ya mapungufu haya ni kuwa na katibu mkuu aliyepwaya
Kuhusu sacrifice na kuacha chama, hili ni suala la Demokrasia.
Alikuwepo Mzee Mtei akampa Marehemu Makani na Mbowe hana choice
Anachotakiwa ni kulea viongozi wajao ambalo ni jukumu lake kwa sasa
Kuhusu kukarabati chama, nalo si suala la mtu ni suala la chama kama taasisi
Anapaswa kuongoza ukarabati na siye yeye kuwa mkarabati
Kuhusu kutokuwa na impact, nalo tuliwahi kusema.
Kwamba amefanya mengi na sacrifice hilo halina ubishi.
Na kwamba ni wakati wa kutoa kijiti. Ameongoza kwa muda wa kutosha
Naliona tatizo kwa CDM katika mambo yafuatayo
1. Lazima safu ya uongozi na hasa katibu mkuu isukwe upya
2. Hakuna sababu za uchaguzi mkuu tofauti na uchaguzi wa Mwenyekiti
Hivi unawezaje kutenga safu za uongozi kwa nyakati?
Yaani uongozi mpya na sekretariati iliyochaguliwa wakati tofauti. Haileti maana
3. Hakuna jitihada za 'amalgamation' kati ya waliohamia na zamani.
Hili lina highlight tatizo la ukarabati na linaashiria mzozo muda si mrefu
Ili kuleta harmony lazima kuwe na new leadership.
CDM wana pool of talents kinachokosekana ni leadership
Mwenyekiti kama tulivyosema ametumika and he has nothing new to offer