Freeman Mbowe: Kauli za Rais Magufuli Kagera hatari

Freeman Mbowe: Kauli za Rais Magufuli Kagera hatari

Mbowe sasa kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani TZ anafanya nn kusimamisha hotuba hizi za kipuuzi za Rais?
Mbona hachukua hatua yyt ile na yy analalamika kama sisi tu?
Magufuli anatakiwa ajutie kauli hizi lkn zinapita kimywa kimywa
CHADEMA imekufa aisee!
Nani mwenye ubavu, mzee wa ukuta wa biscuit ametekewa na kuchanganyikiwa, Maumvi na Zero hawampi nondo kama Dr Slaa alivyokuwa anafanya, Mashinji duu,yeye arudi tu kutibu siasa hawezi tena.
 
Sijui kama una habari ya kilichotokea Kagera. Rais na serikali yake waliweka msimamo kamili kuwa hakuna mtu "kujinufaisha kisiasa" na tetemeko la Kagera. Harakati za awali kabisa za CHADEMA kutoa misaada zilipigwa stop na mbunge Lwakatare alipata kashkash ya kutosha. Amri ikatoka misaada yote ipelekwe kwa RC. Hakuna mwenye ruksa ya kutembelea wahanga kuwafanyia chochote.

Mtu usipotaka kuelewa kwamba sasa tuna utawala wa kidikteta, ukajidai kuwalaumu wengine kwa matatizo ya uongozi mbovu ni ama huna habari na kinachoendelea nchini au wewe ni sehemu ya mashine ya propaganda ya CCM. Unatarajia kweli Magufuli asikie CHADEMA wanajengea watu nyumba na kuwapa chakula wakati yeye keshasema serikali haikuleta tetemeko mtu asisubiri msaada halafu mambo yaende kimya tu? Yaani CHADEMA waonekane bora huku rais na chama chake wakionekana wabaya kwa kuendeleza jeuri na kauli za maudhi? Yeye si mjinga kiasi hicho.

Wale wote wanaotaka kuwalaumu CHADEMA basi wa wawalaumu kwa kukosa ujasiri wa kupinga kwa nguvu jeuri inayoonyeshwa na serikali na kuwa tayari kupambana na vyombo vya dola hadi tone la mwisho la damu. Haya mambo si mchezo. Sijui ni nani asiyeona kwamba safari hii serikali imekaa kishari hasa? Watu wanalaumu tu vyama vya upinzani kwa kutochukua hatua stahiki bila kuiona hesabu kamili iliyo mbele yao. Mimi nataka kusikia watu watakaodai kuwa wameshajiandaa kufa katika mapambano lakini tatizo hawana uongozi makini wa upinzani wa kuwapeleka kwenye uwanja wa vita! Hata Dr. Slaa angekuwepo CHADEMA leo hii asingeweza kufanya kitu. Hizi si enzi za JK.
Hivi mabilioni ya michango yamehusika kwenye advance ya Dreamliner? (Swali,pamoja na alama ya swali mwisho wa swali)
 
yaani utawala huu unawapa wapinzani opportunity kibao za ku-capitalize lakini wao wamelala tu.

kufanyia kazi kauli na matamko yanayotolewa na utawala wa sasa ni mtaji mkubwa na tosha kuliko hata hiyo mikutano ya siasa wanayoililia!

sijui Watanzania tukimbilie kwa nani sasa???
Wanahorodhesha,hadi 2020 watahitaji kila swali,LISIKOSE JIBU.
 
Kwa hakika hiyo ilikuwa hotuba ya kipuuzi kuanza nayo mwaka

Mwaka wote huu utakuwa uchuro tu
 
Mbowe awaombe upya watanzania,wachangie bati hata katika hali hii ambayo jahazi la tanga haliwezi kwenda kwa kukosa upepo,maana tayari Bukoba ni kambi ya UKAWA.

Nadhani siyo wazo baya! Na kupitia Mbunge wanaweza kuanda taratibu inayokubalika kisheria. Kadhia ya namna hii na kauli isiyoyakiungwana kwenye masikio ya Binadamu anayejitambua siyo ya kuhangaika nayo bali kusonga mbelea. Haya ni sawa na kumkibiza kichaa aliyekukwapulia nguo ukiwa unaoga.

cc Tumaini Makene
 
Hivi mabilioni ya michango yamehusika kwenye advance ya Dreamliner? (Swali,pamoja na alama ya swali mwisho wa swali)
Inawezekana, manake hatujawekewa wazi matumizi yakoje. Wanajua wenyewe. Labda kama kuna taasisi rasmi za usimamizi wa fedha za umma zinahusishwa zituletee mrejesho baadaye.
 
Yeye na chama chake wamechukua hatua gani?Sukuwasikia hata michango ya chadema ikiwasilishwa.....this is bullshit.Kutafuta kiki kwenye hotuba ya Raisi hakuna maana yoyote.Yeye angechukua hatua ya kwenda kuwafariji na kuwajengea anachoweza ndio aje kupiga kelele....Mbowe hana nyimbo tena.Chama chake si kina ruzuku kubwa tu ....mbona hawajajenga hata nyumba moja....Je si wana mishahara wangejichanga tu kwa vile wana uchungu mkubwa zaidi kuliko Raisi.Otherwise pye pye pye hazina maana
Upoooo baba penielaa wa mathew
 
Mbowe sasa kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani TZ anafanya nn kusimamisha hotuba hizi za kipuuzi za Rais?
Mbona hachukua hatua yyt ile na yy analalamika kama sisi tu?
Magufuli anatakiwa ajutie kauli hizi lkn zinapita kimywa kimywa
CHADEMA imekufa aisee!
 
Kuna vilaza wa mwendo kasi hapa ! Hauungi mkono upizani ila unataka ukutetee et kama yy kiongozi wa upinzani amefanya maamuzi gani?

Afanye nn kama mtaji wake wa watu ni wengi lkn waoga sana akisema UKUTA Mnasema shika ww

na lile jamaa lina dola hata leo Mbowe akiweka mkuta wa hadhara wa harambee ya changia maafa atasambalatishwa tu et siasa hadi2020 unachekelea... Sasa wanasiasa watawezaje kukutetea bilaa majukwaa ya siasa?
 
ur smart broo
 
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani (CHADEMA), ameikosoa hotuba aloitoa Rais Magufuli Mkoani Kagera kwa kusema " Hivi mtu ambae amefiwa, nyumba imebomelewa, hana chakula, hana pesa unakwenda kutoa kauli za kibabe kwamba hutowapa chakula kwakuwa serikali haina shamba! hivyo sio sawasawa"

View attachment 454940
Kwa nchi zinazofuata misingi ya haki za binadamu , kauli zile ilikuwa ni UHALIFU DHIDI YA UBINADAMU , ni kinyume cha sheria za dunia hii .
 
Limeniacha hoi suala la katerero. Anatamka bila tone la aibu.Huyu si bure.
 
Mbowe sasa kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani TZ anafanya nn kusimamisha hotuba hizi za kipuuzi za Rais?
Mbona hachukua hatua yyt ile na yy analalamika kama sisi tu?
Magufuli anatakiwa ajutie kauli hizi lkn zinapita kimywa kimywa
CHADEMA imekufa aisee!
Kwa maana ya kiumakini na ushawishi hata mimi naona nayo imepwaya, huo ni ukweli. Pamoja sijafurahia alichokifanya mzee Slaa aka Mzee wa Mihogo bado ile ladha yake inakosekana.
 
Back
Top Bottom