mambo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 2,371
- 5,608
Ukiwa hujitambui unafikiri kila mtu ni kama wewe....Sio lazima kila mtu ajue kwamba hujitambui
Ukiwa hujitambui unafikiri kila mtu ni kama wewe....Sio lazima kila mtu ajue kwamba hujitambui
Hapepesi maneno anaongea kitu kama kilivyo na sio mnafiki.uchuje mwenyewe na kupambanuaSawa, twende kwenye hoja. Unasemaje kuhusu Kauli za John kwenye hotuba yake!?
Walifika kagera na wakaanza kutoa misaada ya maturubai,wakakamatwa na polisi na kufurumushwa kuwa kamati maalum ndio yenye jukumu!
Chadema hajafa na wala haitakufa unshisi Mbowe angemkosoa vipi, mikutano imezuiliwa unajua inabidi atumie gazetMbowe sasa kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani TZ anafanya nn kusimamisha hotuba hizi za kipuuzi za Rais?
Mbona hachukua hatua yyt ile na yy analalamika kama sisi tu?
Magufuli anatakiwa ajutie kauli hizi lkn zinapita kimywa kimywa
CHADEMA imekufa aisee!
Chadema itimize wajibu wake iache kelele tu .Ni mgonjwa wa utindio wa ubongo ndie anaewaza kuwa Cdm ifanye yale serikali iliyoyashindwa! Badala ya kulaum serkali kwa kushindwa kutimiza wajibu wake unaleta upuuzi hapa kwahiyo madawa hospitali yakipungua utaiomba cdm ipeleke dawa? Hivi upo lumumba au mahabusu
Una uhakika au mvivu wa kutafta habariYeye na chama chake wamechukua hatua gani?Sukuwasikia hata michango ya chadema ikiwasilishwa.....this is bullshit.Kutafuta kiki kwenye hotuba ya Raisi hakuna maana yoyote.Yeye angechukua hatua ya kwenda kuwafariji na kuwajengea anachoweza ndio aje kupiga kelele....Mbowe hana nyimbo tena.Chama chake si kina ruzuku kubwa tu ....mbona hawajajenga hata nyumba moja....Je si wana mishahara wangejichanga tu kwa vile wana uchungu mkubwa zaidi kuliko Raisi.Otherwise pye pye pye hazina maana
Mmoja wa rafiki yangu anayefanya kazi kagera alinieleza hayo pia!Mkuu story za kusadikika unaziamini?
Huyo rafiki yako amedanganywa.usiamini uzushi mtu smart kama wewe.Mmoja wa rafiki yangu anayefanya kazi kagera alinieleza hayo pia!
Habari mnazopenda kuzisikia ni za kizushiUna uhakika au mvivu wa kutafta habari
Hana sababu ya kudanganya!Labda na wewe unaweza nipa ushahidi kuwa si kweli?Huyo rafiki yako amedanganywa.usiamini uzushi mtu smart kama wewe.
Habari mnazopenda kuzisikia ni za kizushi
Unajitoa ufaham.mbowe alienda kagera na wakachangia mifuko 400 ya cement na lowasa ndie aliyeiwakilisha kwa niaba ya chama.unaropoka huku huna data.Yeye na chama chake wamechukua hatua gani?Sukuwasikia hata michango ya chadema ikiwasilishwa.....this is bullshit.Kutafuta kiki kwenye hotuba ya Raisi hakuna maana yoyote.Yeye angechukua hatua ya kwenda kuwafariji na kuwajengea anachoweza ndio aje kupiga kelele....Mbowe hana nyimbo tena.Chama chake si kina ruzuku kubwa tu ....mbona hawajajenga hata nyumba moja....Je si wana mishahara wangejichanga tu kwa vile wana uchungu mkubwa zaidi kuliko Raisi.Otherwise pye pye pye hazina maana
kweliHana sababu ya kudanganya!Labda na wewe unaweza nipa ushahidi kuwa si kweli?
Uzushi upiHabari mnazopenda kuzisikia ni za kizushi
Mifuko 400?watu wakubwa kama hao?wanatania wananchi wa KageraUnajitoa ufaham.mbowe alienda kagera na wakachangia mifuko 400 ya cement na lowasa ndie aliyeiwakilisha kwa niaba ya chama.unaropoka huku huna data.
WakwakoUzushi upi
Kwa hiyo huu ni uzushi?!Imechapishwa: Thu, Sep 15th, 2016
Bungeni / Kitaifa / Slideshow | Na Mtanzania Digital
Zungu amwomba radhi Mbowe
SHARE THIS
[http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania][http://mtanzania]
TAGS
[http://mtanzania]
MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu.
Na Maregesi Paul, Dodoma
MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu, amemwomba radhi Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kutomtaja
alipokuwa akiwashukuru viongozi walioshiriki kuwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu mkoani Kagera.
Zungu alimuomba radhi Mbowe jana baada ya wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara wa Ukonga na Paschal Haonga wa Mbozi, kusimama na kuomba mwongozo kwa nyakati tofauti.
Aliyeanzakumlalamikia Zungu ni Waitara ambaye katika maelezo yake, alisema anashangazwa na utaratibu uliotumiwa na mwenyekiti huyo wa Bunge kwa kushindwa kutambua mchango uliotolewa na Mbowe baada ya kutokea tetemeko hilo.
“Mheshimiwa mwenyekiti, hivi punde umewataja na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa Serikali walioshiriki kwa karibu kuwapa pole wananchi waliopatwa na matatizo kule Kagera kutokana na tetemeko la ardhi.
“Umewataja waziri mkuu na mawaziri wengine walioshiriki tukio hilo, lakini hukumtaja kabisa kiongozi wa upinzani bungeni wakati naye alikwenda Bukoba kutoa pole.
“Hata sisi wabunge wa Chadema kabla ya Bunge kukubali kukatwa posho ya siku moja ili kuwachangia waathirika, tulikuwa tumekwisha kuchangishana fedha na kumkabidhi mwenyekiti wetu azipeleke, lakini hukututaja.
“Kwa hiyo, mheshimiwa mwenyekiti, naomba mwongozo wako juu ya tukio hili kwa vile imekuwa ni kawaida kwa viongozi wa Serikali kutowatambua viongozi wa upinzani katika matukio mbalimbali,” alisema Waitara.
Hoja hiyo ya Waitara, iliungwa mkono na Haonga ambaye naye alionyesha kumshangaa Zungu kwa kutomtaja Mbowe.
“Mheshimiwa mwenyekiti, mwongozo wangu hautofautiani na mwongozo wa Mheshimiwa Waitara kwa sababu umewataja viongozi wengine na kushindwa kumtaja Mbowe wakati ni kiongozi mkubwa hapa bungeni.
“Kwa hiyo na mimi naomba mwongozo wako katika jambo hilo,” alisema Haonga baada ya kutumia kanuni ya 68 (7).
Akijibu miongozo hiyo, Zungu alikiri kosa kwa kutomtaja Mbowe kwa kuwa naye alishiriki kwa karibu kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo.
“Ni kweli sikumtaja Mbowe, namuomba radhi kwa kosa hilo. Hili suala lisitugawe, tuwe wamoja tuweze kuwasaidia ndugu zetu waliopata matatizo,” alisema Zungu.
Awali, mwenyekiti huyo wa Bunge aliishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoshiriki kwa karibu kukabiliana na madhara ya tukio hilo na kuitaka iendelee
na utaratibu huo kila majanga yanapotokea.
Septemba 10 mwaka huu, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 katika vipimo vya richter lilitokea mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 17 na kujeruhi wengine zaidi ya 200.
Pia, tetemeko hilo lilisababisha majengo na nyumba kadhaa kuharibiwa zikiwamo taasisi za umma na za binafsi.
Msaada ni msaada.haujarishi ni wa kiasi gan.kuna wa fisiem walipeleka mifuko 50 ya unga.je mifuko hiyo kwa thaman ni sawa na ukubwa wa chama?Mifuko 400?watu wakubwa kama hao?wanatania wananchi wa Kagera
Kwani chama cha upinzani ni chadema tu tanzania?Aisee naazisha chama, huu upuuzi wa upinzani hauvumiliki