Freeman Mbowe Award: From BAVICHA

This is a very logical but biased analysis. Hofu hii ya tuzo kuchafuka kutokana na jina la mwenye tuzo kuchafuka ipo; ndio maana taasisi nyingi huchagua majina ya hayati katika tuzo. Lakini tunaweza pia kumpima mtu kwa muda aliyoishi mpaka wakati huo maamuzi yanapofanyika.

Naamini vijana wa Mikoa mingine wanapaswa kuiga mfano huu wa Mkoa wa Kinondoni ambao Mwenyekiti Mbowe ni mmoja wa wakazi wake mathalani mkoa wa Mara unaweza kuanzisha Tuzo ya Ujasiri ya Chacha Wangwe.

JJ

JJ hapo nilipoweka redi ni statements mbili zinazokinzana. Mwanajamvi hapo juu alishauri ni bora tuzo ikapewa jina la almarhum kwa sababu ni mtu aliyemaliza kazi yake. Naamini hapo chadema mnao watu wengi wakiwemo waasisi wa chama waliofanya kazi kubwa kukifikisha chama hapo kilipo na wengine bado wapo wanafanya kazi nzuri(bado tunakumbuka vizuri namna wazee hao walivyotumia busara wakati wa uchaguzi wenu mwezi septemba) na wapo wengine wametangulia mbele ya haki. Kwahiyo mngeweza kumtumia mmoja wapo kwenye hiyo tuzo. Wasiwasi wa wadau ni kuonekana mnamtukuza sana mbowe, mnafanya yale mambo ya zidumu fikra za mwenyekiti.

Kwakuwa umemtaja almarhum kamanda Chacha Wangwe basi nadhani katika mtazamo huo huo mfikirie kubadilisha jina la hiyo tuzo, na mimi nadhani hakuna ubaya wowote mkiita kwa jina la Chacha Wangwe. Sio lazima ifanywe na watu wa mkoa wa mara, kwakuwa Chacha Wangwe alikuwa kiongozi wa kitaifa katika chama chenu na alichangia kwa kiasi kikubwa ustawi na kushamiri kwa chadema wilayani Tarime na mkoaa mara kwa ujumla.

Kama mkiendelea kusisitiza na kuhimiza utoaji wa tuzo kwa kuangalia mahali mtu alikozaliwa, jihadhari sana msije mkaonekana wakabila!!!
 
Ikiitwa Chacha Wangwe na kuitwa Freeman Mbowe tofauti ni moja kwamba mmoja katangulia mbele za haki na mwingine yuk lakini bado tuzo itatolewa iwe na Mbowe ana yeyote ndani ya Chadema . Hapa asiyetakiwa kwa uharaka wangu wa kuona mambo ni Mbowe maana hapa jamvini kuna watu siku hizi ni Mbowe , Zitto , Chadema na hata ustawi wa Chama hakuna tena .So JJ fikirieni tena bwana muone kipi bora mjiandae na kujibu hoja na sijaona la kutukuza . Mo ana tuzo yake hapa Africa wanapata ama wana kosekana je anatukuzwa MO ?
 
Bavicha kabla kuwa na uthubutu wa kutoa award za Uhuru na blah blah zingine waanze na kusafisha nyumba yao kwanza kwa kuheshimu matokeo ya uchaguzi wao wenyewe. Mnataka kufanya makubwa wakati demokrasia mnaibaki mchana kweupe.

Halafu huyo mwenye jina la hiyo award ndio ovyoo kabisa, hana cha kutoa mfano kwa so called vijana labda hilo jina lake tu. Mtu alieshindwa shule atapewaje jina la award yenye hadhi kama hiyo.

Na wewe Mnyika umekimbia shule huwezi kuwa mfano kwa hao vijana. Yaani hiyo Bavicha mambo ni shaghala baghala tu.
 
Masatu Chama Chetu kimesheheni wasomi haswa na wa kufinyangwa walio jaa vyeti vya kugushi lakin wote hawana toafuti na wale akina Mwakyembe wenye shule za kweli , unalisemeaje hilo ?

Demokrasia kwako means what kaka .
 
Bavicha kabla kuwa na uthubutu wa kutoa award za Uhuru na blah blah zingine waanze na kusafisha nyumba yao kwanza kwa kuheshimu matokeo ya uchaguzi wao wenyewe. Mnataka kufanya makubwa wakati demokrasia mnaibaki mchana kweupe.

Halafu huyo mwenye jina la hiyo award ndio ovyoo kabisa, hana cha kutoa mfano kwa so called vijana labda hilo jina lake tu. Mtu alieshindwa shule atapewaje jina la award yenye hadhi kama hiyo.

Na wewe Mnyika umekimbia shule huwezi kuwa mfano kwa hao vijana. Yaani hiyo Bavicha mambo ni shaghala baghala tu.
Masatu suala la shule halina wakati, labda huko kwenu mlipangiwa msome muda gani, nani amekwambia elimu ina mwisho? Huoni kwa wenzio wasomi wa hali ya juu na wale moderate walivyoshirikiana kuendeleza nchi zao. Huoni ile combination ya Lula kule Brazil, yule kondakta wa basi kule Uingereza alivyoumudu uwaziri Mkuu, kule China yule mzamiaji ufaransa (mbeba maboksi = Deng Xiaoping) alivyorudi kwao China na kuibadilisha China tunayoiona leo? Mifano ni mingi. Let them work. Upo right kwenye haya ya demokrasia na power grabbing labda haya inabidi watuambie.

They worked very hard and they want to destroy what they achieved in a decade of building their party!
 
Masatu umerudi tena na vita vyako kwa CHADEMA.He he heee.Utajuji uchaguzi wa BAVICHA ulishafutwa na aliyeuvuruga ameshahama chama unatak nini tena? Mbowe wala si hovyo kushinda wewe,wewe umezidi...kwa taarifa yako hakuna mtu asiyekuwa na mapungufu. Unafikiri kusoma ndo dili?si bora Mnyika hata kama amekimbia shule but he is very bright?we uko wapi na hako kaelimu kako?kuna wangapi wana prefix za Dr,Prof,je wanadeliver au kubehave kulingana na elimu zao?we mbona hufanani na unachokililia eti elimu?We want think tanks na sio mavyeti.
 
Masatu suala la shule halina wakati, labda huko kwenu mlipangiwa msome muda gani, nani amekwambia elimu ina mwisho? Huoni kwa wenzio wasomi wa hali ya juu na wale moderate walivyoshirikiana kuendeleza nchi zao. Huoni ile combination ya Lula kule Brazil, yule kondakta wa basi kule Uingereza alivyoumudu uwaziri Mkuu, kule China yule mzamiaji ufaransa (mbeba maboksi = Deng Xiaoping) alivyorudi kwao China na kuibadilisha China tunayoiona leo? Mifano ni mingi. Let them work. Upo right kwenye haya ya demokrasia na power grabbing labda haya inabidi watuambie.

They worked very hard and they want to destroy what they achieved in a decade of building their party!

Sawa sikatai elimu haina mwisho lakini M/kiti kaenda kusoma ukubwani na kafeli vibaya.

Hii inaonyesha upeo wake umefikia hapo kichwa chake hakiwezi tena kubeba mambo ya kitaaluma.

Sasa huyu huyu ndio anatoa award kwa jina lake. Tuna safari ndefu
 
Ikiitwa Chacha Wangwe na kuitwa Freeman Mbowe tofauti ni moja kwamba mmoja katangulia mbele za haki na mwingine yuk lakini bado tuzo itatolewa iwe na Mbowe ana yeyote ndani ya Chadema . Hapa asiyetakiwa kwa uharaka wangu wa kuona mambo ni Mbowe maana hapa jamvini kuna watu siku hizi ni Mbowe , Zitto , Chadema na hata ustawi wa Chama hakuna tena .So JJ fikirieni tena bwana muone kipi bora mjiandae na kujibu hoja na sijaona la kutukuza . Mo ana tuzo yake hapa Africa wanapata ama wana kosekana je anatukuzwa MO ?

Jamani ndugu yangu
sasa Mbowe kafanya nini hadi atunukiwe ? mambo mengine sisi watanzania tunafurahisha sana.
 
Wazo zuri but "short notice". Ni changamoto kubwa mtu kujipanga na kuandika hotuba nzuri ndani ya siku 5.
 
chadema kuna uhuru wa kweli?
hakuna uhuru wa kweli.kichekesho sana hilo baraza la vijana halina mwenyekiti wa taifa wa vijana.aliyebaka demokrasia ndiye anatengenezewa award. Ni kujikomba kwa mnyika na kumkosha mwenyekiti wao ambaye ni dikteta wa demokrasia.hivi sasa wamewafukuza watu wote wanaomsapoti zitto kabwe. Hii ni kama njia ya kumdhoofisha zitto.
 
jamani ndugu yangu
sasa mbowe kafanya nini hadi atunukiwe ? Mambo mengine sisi watanzania tunafurahisha sana.
kizuri zaidi mwenyekiti ana elimu ya kidato cha nne tunawapa ujumbe gani vijana?
 
This is a very logical but biased analysis. Hofu hii ya tuzo kuchafuka kutokana na jina la mwenye tuzo kuchafuka ipo; ndio maana taasisi nyingi huchagua majina ya hayati katika tuzo. Lakini tunaweza pia kumpima mtu kwa muda aliyoishi mpaka wakati huo maamuzi yanapofanyika.

Naamini vijana wa Mikoa mingine wanapaswa kuiga mfano huu wa Mkoa wa Kinondoni ambao Mwenyekiti Mbowe ni mmoja wa wakazi wake mathalani mkoa wa Mara unaweza kuanzisha Tuzo ya Ujasiri ya Chacha Wangwe.

JJ
Wewe kweli unapendekeza tuzo ya Chacha Wangwe? wewe mbona ni kijana lakini unajiingiza katika unafiki ukiwa mdogo? sio wewe na wenzako mliohujumu tamasha la kumbukumbu ya mwaka mmoja ya Chacha Wangwe, lakini tunamshukuru Mungu ilifanyika Tarime kwa ushindi.

Najua utakanusha hili lakini moyoni mwako wajua ukweli na Mungu anajua kuwa unachosema juu ya Wangwe kwa uzuri hayatoki moyoni na ndo maana ulimkana humjui Deus Malya na ilhali we ndo ulimteua na kumpeleka Libya kuwakilisha chama na kama mnaona kuna umuhimu wa kutoa award in the name of Wangwe na ni dhamira ya kweli kwenu na kwa kuwa Wangwe alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa kwanini Chadema Taifa msianzishe ikawa na ukubwa huo wa Taifa na unasema Mkoa wa Mara wafanye, kwa nini wewe uliyepata wazo hilo usimshirikishe Mwenyekiti wako na Katibu Mkuu na Sekretariet yenu ili mtoe tuzo hiyo?

Mkifanya hivyo tutaamini kweli ninyi si wanafiki ila nia yenu/yako dhidi ya kumuenzi Wangwe ni dhahiri la sivyo itakuwa ni porojo zenu za kila siku na unafiki uliotukuka.
 
Zidumu fikra za mwenyekiti wa CHADEMA..Zidumuuuuuuu
wanajamvi kwa anayejua naomba anisaidie kuniweka wazi kuhusu ni nani wanaokamata nafasi hizi na ni watu wa makabila gani katika CHADEMA!!
1.WABUNGE VITI MAALUM
2.WAKURUGENZI WA VITENGO VYA CHAMA(vijana,kina mama n.k)
3.WAFANYAKAZI KATIKA OFISI ZA CHAMA(wahasibu,makarani,makatibu muhtasi n.k)
4.VIONGOZI WA CHAMA WA MIKOA(wenyeviti,makatibu,waweka hazina n.k)
5.KITENGO CHA WAZEE WA CHAMA.
Yalimtokea CHACHA WANGWE tukaambiwa ni ajali,hatutakubali yamtokee ZITTO KABWE......
hii nchi ni yetu sote na wala sio ya wachaga tuuuu.Mtaniita m-baguzi lakini huo ndio ukweli.If we dont control them within our part CHADEMA,it will finally be the cancer of the whole Tanzania as a nation.
 
hakuna uhuru wa kweli.kichekesho sana hilo baraza la vijana halina mwenyekiti wa taifa wa vijana.aliyebaka demokrasia ndiye anatengenezewa award. Ni kujikomba kwa mnyika na kumkosha mwenyekiti wao ambaye ni dikteta wa demokrasia.hivi sasa wamewafukuza watu wote wanaomsapoti zitto kabwe. Hii ni kama njia ya kumdhoofisha zitto.

Wewe nawe ni mwanachama wa CHADEMA?
 
Why is this award even named after this man who is a non-starter. This is absurd.
 
Yani watanzania kweli tuna muda wakuchezea bora tukalime tuu. Yani hii kitu japokuwa its of no consequence in a direct way, imenichefua sana. Siasa za ndio mzee alafu mzee mwenyewe in mbumbumbu.
 
Back
Top Bottom