Freeman Mbowe Award: From BAVICHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Freeman Mbowe Award: From BAVICHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, Dec 5, 2009.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,090
  Likes Received: 2,225
  Trophy Points: 280
  TAARIFA KWA UMMA

  Taarifa inatolewa kwa umma kwamba Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Kinondoni Kanda ya Dar es salaam kilikaa kikao chake tarehe 1 Disemba 2009 na kuazimia masuala mawili kama sehemu ya kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania: Mosi, Kutoa Tuzo ya Vijana ya Freeman Mbowe kuhusu Uhuru wa Kweli (Freeman Mbowe Real Freedom Youth Award 2009). Pili; kuitisha Kongamano la Vijana kuadhimisha siku ya Uhuru lenye mada/ujumbe: "Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli.

  Tuzo hiyo itatolewa kwa vijana watakaoandika hotuba ya kurasa kati ya mbili na kumi kuhusu mada/ujumbe "Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli" yenye mawazo ya vijana kuhusu hali ya Taifa miaka 48 baada ya uhuru na kupendekeza mwelekeo mbadala. Wanaoweza kushiriki katika shindano hilo ni vijana wa kitanzania wa kike na wa kiume wenye umri kati ya miaka 12 na 35 wanaoishi katika Halmashauri ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam.

  Washindi katika shindano hilo watapa fursa ya kualikwa kutoa hotuba zao kwenye Kongamano hilo la maadhimisho ya siku ya uhuru mbele ya viongozi, wanachama na wananchi kwa ujumla. Washindi katika shindano hilo atazawadiwa vyeti vilivyosainiwa na BAVICHA pamoja na John Mnyika; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni Kanda ya Dar es salaam. Pamoja na zawadi hizo; mshindi wa kwanza atapatiwa kifuta jasho cha shilingi laki moja wakati mshindi wa pili atapata shilingi elfu hamsini na washindi watakuwa katika uwiano wa kijinsia. Washiriki kumi bora wa shindano hilo watapatiwa Tshirt maalum za Vijana. Aidha uongozi wa vijana unaomba wapenda demokrasia na maendeleo ndani na nje ya Tanzania kuchangia tuzo hii.

  Vijana wameanza kutangaziwa shindano hilo toka tarehe 1 Disemba 2009 na mwisho wa kutuma hotuba kwa wanaohitaji kushiriki ni tarehe 8 Disemba 2009 saa 6 mchana. Washiriki wanaweza kutuma hotuba zao kwa barua pepe kwenda kinondoni@chadema.or.tz ama chademakinondoni@gmail.com ama kuandika kwa mkono na kupeleka katika ofisi za CHADEMA mkoa zilizopo Kinondoni Kata ya Hananasifu Mtaa wa Kisutu. BAVICHA kinondoni inahimiza vijana wote wazalendo bila kujali itikadi kuandika mawazo yao ili kufikisha ujumbe kwa watanzania wote kuhusu mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli.

  Uamuzi wa kuchagua kuiita Tuzo jina la Freeman Mbowe umetokana na mchango wake katika harakati za mabadiliko ya kweli uhuru wa kweli. Freeman Mbowe alizaliwa miezi michache kabla ya Tanganyika kupata uhuru lakini wazazi wake hawakumbatiza mpaka tarehe 9 Disemba 1961 siku ya uhuru ndipo alipobatizwa na kupewa jina la Freeman; maana yake "Mtu Huru". Aidha amekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Vijana wa CHADEMA katikati ya kundi la vijana wa zamani (Wazee) walioamini katika nafasi ya vijana katika kuleta mabadiliko ndio maana chama kiliposajiliwa mwaka 1992 kilianza na kauli mbiu ya: Vijana; Taifa la Leo. Kwa sasa BAVICHA imeongezea kauli mbiu ya: Vijana; Nguvu ya Mabadiliko. Freeman Mbowe ni mmoja wa wafanyabiashara waliofanya vizuri kuanzia katika ujana wake na kuwa mfano katika harakati za kuleta uhuru wa kweli wa kiuchumi. Freeman Mbowe alipata kuwa mbunge wa Hai na mafanikio yake katika jimbo lake katika sekta ya afya, elimu nk yalikuwa ya mfano wa kuigwa. Pamoja na mambo mengine aligawa kompyuta mashuleni na kuanzisha mafunzo ya aina hiyo mpaka vijijini ili kutoa uhuru kwa vijana kuweza kuendana na karne ya sayansi ya Teknolojia. Pia alianzisha programu ya chakula na maziwa mashuleni ili kuwafanya wasome na kuwa mfano katika harakati za kuleta uhuru wa kweli wa kijamii. Freeman Mbowe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa mwaka 2004; na katika kipindi chake cha uongozi amekuwa mstari wa mbele kuwapa kipaumbele vijana wasomi na hata vijana kwa kuwapa fursa za kuongoza nafasi za juu katika chama.

  Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika na wengineo na kuwa mfano katika harakati za kuleta uhuru wa kweli wa kisiasa. Freeman Mbowe ameendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA akiongoza kipindi chake cha pili na cha mwisho kinachomalizika mwaka 2014. Freeman Mbowe amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mabadiliko ya kweli kwa ajili ya kuleta uhuru wa kweli akiamini kwamba uhuru wa bendera pekee hautoshi kama taifa litaongozwa kwa ukoloni mamboleo unaopora rasilimali na kwamba uhuru wa kweli ni ule unaowezesha wananchi kuwa huru kiuchumi, kijamii na kisiasa.

  Aidha BAVICHA Kinondoni inatambua na kupongeza kufanyika kwa Kongamano la Kumbukumbu ya Miaka 10 ya Kifo cha Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere(MNF). Hivyo, pamoja na hotuba zitakazotolewa na washindi kuhusu mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli; Kongamano la Vijana Mkoa wa Kinondoni Kanda ya Dar es salaam katika kuadhimisha miaka 48 ya uhuru litatafakari namna ya kuhamasisha utekelezaji maazimio ya Kongamano la Kumbukumbu ya Nyerere lililomalizika hususani yale yanayolenga kulinusuru Taifa.

  Maazimio hayo saba ni pamoja na: Mosi; Kufanyika maamuzi magumu na hatua za kijasiri kwa lengo la kurejesha maadili aliyoacha Nyerere. Maadili hayo ni pamoja na kuheshimu na kuzingatia katiba, utawala wa sheria kwa mujibu wa katiba, na viapo vya uongozi/utumishi. Pili; kutambua kwamba cheo ni dhamana na kamwe kisitumike kwa faida binafsi. Tatu; Viongozi kusimamia matumizi bora ya rasilimali za Taifa. Nne; Wananchi kutambua kwamba wanajukumu la kwanza kuhakikisha wanapata viongozi wazuri. Tano; Viongozi nao kutambua na kuheshimu maamuzi ya wananchi waliowapa madaraka. Sita; viongozi wakishirikiana na wananchi wachukie rushwa na ufisadi na wapinge kwa kwa kauli na vitendo. Saba; Viongozi wajenge utamaduni wa kuwajibika pale wananchi wanapowahusisha na kashfa na makosa ya kimaadili ya uongozi.

  Imetolewa na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Kinondoni Kanda ya Dar es Salaam, Hemed Msabaha; kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0712222214 au 0653329668

  Disemba 5, 2009
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nadhani ni move nzuri. Kama vyama vingine (pinzani) wataandaa matukio na majukwaa mbalimbali kujadili uhuru wa Tanganyika na kutafakari mustakabali wa nchi yetu ni jambo la kupongezwa sana. Itasaidia kufanya upembuzi wa matunda ya uhuru kwa jicho la 3! Ilike it!
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  MMMM, more explanation please! "the poster" is Jamiiforums; on the behalf of--------?
  Again, are we starting "Zidumu Fikra za mwenyekiti" style or that is a consolidation of power!
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tanganyika bado ipo vile?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ndiyo.. Kikwete alisema ipo!
   
 6. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,090
  Likes Received: 2,225
  Trophy Points: 280
  Mkuu IO,

  Taarifa hii imetumwa asubuhi ya leo (5th Dec 2009) kwa vyombo vyote vya habari. Tumetumiwa nakala katika info@jamiiforums.com, sidhani kama tumekosea kuiweka JF.

  Ahsante
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakuna nchi inayoitwa Tanzania , ambayo ilipata uhuru mwaka1961.
  Tanganyika ndiyo iliyopata uhuru bana.

  Pia tusijidai mabingwa wa kupotosha historia. We Kibs kila siku unadai kujiondoa toka muungano, unadhani tukikuachilia uende jina letu litakuwa nani?

  Tanganyika ipo, japo kama dormant entity!
   
 8. C

  Chuma JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Chadema kuna Uhuru wa Kweli?
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mkuu Chuma, najua swali hilo lazima wanajiuliza wengi... Hapo ndo tunapomwitaji Mnyika kwa ufafanuzi wa mambo kadha wa kadha!
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hongereni BAVICHA kwa wazo zuri.Keep it up...mwnedo huo huo Hakuna Kulala mpaka Kieleweke
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  Mbona upo tu? Au mpaka Zitto agombee uenyekiti?

  Mkuu kwanini tusiendelee na mada husika?
   
 12. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  This is what I want to believe: Chadema imekua, na nguvu zake ni kubwa; mvuto umekuwa mkubwa kwa watu wengi maarufu ambao sasa hivi wako mguu upande kwenda Chadema au kubaki na vyama vyao.

  Vilevile mawazo ya wananchi wengi yalishaanza kuwa muelekeo wa Chadema. Hii pressure inamfanya Mwenyekiti kuwa katika kukalia kiti ambacho ni cha moto. Kwa hiyo anataka kwa mbinu yoyote ile ajijenge kichama, as mwenyekiti na itikadi ambayo itamfanya aweze ku-survive.

  This chronicle of stories from the Chadema General Meeting to this day is a spolight of events which makes Chadema a contraversal political party. We tried to fight CCM by using an emerging example of Chadema, now we are caught within.

  What is cooking??
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280
  You are truly interested observer!
   
 14. M

  MC JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45


  Mnyika sikuelewi unapoomba michango toka kwa wadau, siku za nyuma uliandika kuhusu Kongamano la nyerere (kama sijakosea) ukaomba mchango, ukatoa Email address, nikakuandikia imail, hata kujibu haukujibu....
  leo tena unakuja na hoja ileile 'Naomba wapenda Demokrasia wachangie' You are either not serious! or you don't mean what you say!
   
 15. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu ingekuwa vizuri ukaweka wazi uhuru katika nyanja zipi? Maana kama umeuliza inawezekana kuna kitu unadhani hakiko vizuri.
   
 16. m

  mwansanga New Member

  #16
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana BAVICHA,

  Wazo ni zuri ila jina la tuzo sikubariani nalo. Ningeshauri jina Mbowe liondolewe kwani linajenga ushawishi kwamba nia yenu ni kumtukuza mwenyekiti wa chama Bw. Freeman Mbowe ambaye siku ya uhuru ni birthday yake kama taarifa zangu nilizonazo ni sahihi. Kusherekea birthday za viongozi naona ni yaleyale ya zidumu fikra za mwenyekiti.

  Je, ikitokea bw. Freeman akaamua kuhama chadema na kuingia NCCR kama alivyofanya bw. Kafulia, hiyo tuzo itaendelea kuitwa hivyo hivyo? Najua baadhi ya wanachadema wanafyonya chinichini kwakuwa nimesema Freeman anaweza kuhama Chadema. Nasisitiza anaweza.

  Mmemsahau Dr. Kaborou ambaye binafsi alinishawishi kweli miaka ya tisini alipohojiwa kwenye the best kipindi cha wakati hii almaarufu KITIMOTO. yupo wapi leo? Kama wengine wanaweza Freeman Mbowe ashindwe ana nini?

  Kuenzi vitu vizuri ni jambo zuri sana kwani linatia moyo wahusika. Ila inapendeza kuanzisha tuzo la watu ambao hawana nafasi ya kufanya makosa tena yaani waliotangulia mbele za haki.

  Huu ni mtazamo wangu tu, ambao najua wanaforum hii mtausoma na kuukubali au kuukataa.

  I BELIEVE in MBADALA aka ALTERNATIVE
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Leo unamjua Kikwete sio?
   
 18. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #18
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mc

  Nashukuru wa ujumbe wako.

  Mosi, sio mimi ninayeomba mchango katika suala hili, ni BAVICHA Kinondoni na mwenyekiti wao ndiye aliyetoa taarifa hii kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, kama Mwenyekiti wa Mkoa husika nina interest katika suala hili; naomba muwasiliane nao kupitia anuani pepe waliyoitoa kama walivyoomba.

  Pili; sikumbuki kupokea ujumbe toka kwako baada ya kuandika mwito wa Maandamano wakati ule kwa ajili ya kutuma mchango. Ila nakumbuka kuna mtanzania mmoja tu anayeishi nje ya nchi ndiye aliyeandika ujumbe na kueleza kwamba angependa kuchangia lakini mpaka arudi Tanzania. Samahani kwa kutokuona ujumbe wako kama uliutuma, naomba unitumie tena kupitia mnyika@chadema.or.tz na nakala kwenda mnyika@yahoo.com.

  Jukumu tulilonalo ni kubwa sana ukilinganisha na kiasi cha ruzuku ya chama na michango yetu binafsi tunayoitoa. Tunalazimika kutembeza bakuli tukiamini kwamba wajibu wa kuleta mabadiliko ni wa pamoja. Ni kama katika vita, wako waliojitolea kwenda front line, lakini wapo ambao wako nyuma ya pazia wakisaidia kwa kutoa supplies kwa ajili ya combatants.

  JJ
   
 19. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #19
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  This is a very logical but biased analysis. Hofu hii ya tuzo kuchafuka kutokana na jina la mwenye tuzo kuchafuka ipo; ndio maana taasisi nyingi huchagua majina ya hayati katika tuzo. Lakini tunaweza pia kumpima mtu kwa muda aliyoishi mpaka wakati huo maamuzi yanapofanyika.

  Naamini vijana wa Mikoa mingine wanapaswa kuiga mfano huu wa Mkoa wa Kinondoni ambao Mwenyekiti Mbowe ni mmoja wa wakazi wake mathalani mkoa wa Mara unaweza kuanzisha Tuzo ya Ujasiri ya Chacha Wangwe.

  JJ
   
 20. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #20
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  CHADEMA daima inaongoza kwa watu wenye vision pana, na muelekeo sahihi huku nidhamu na utii kwa chama vikiwa nguzo.

  NAWAPONGEZA BAVICHA na wapongeza wale wote waliowahi kupitia umoja huu wa vijana ambao ni mfano wa kuigwa.

  Daima mbele Nyuma Mwiko, mpaka kieleweke
  .
   
Loading...