Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Chadema imeshakufa
Mkuu bado upo?

Habari za siku nyingi?

Umepotea, Umeibuka, Mbowe bado upo tu!

Kwa sasa hoja zinazoletwa ni kama vile bila uwepo Mbowe ni uwepo wa CHADEMA! Yaani Mbowe akitangulia mbele ya haki hata CHADEMA kinatangulia mbele ya haki!
 
Hakuna kiongozi anayekosa wapambe, lakini kiukweli Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm sio afya kwa cdm. Tunaosema hivi tuna mapenzi mazito na cdm kama taasisi, kuliko wapambe wake wachache wenye maslahi naye binafsi. Huu ni wakati sahihi wa mtu kama John Heche au Marcus Albanie kuwa mwenyekiti wa cdm, na Mbowe kubaki kama mjumbe maalum (VIP) wa cdm kwa afya ya chama.
Kapige kura mkuu porojo hatasaidia
 
#Mbowe Tano Tena#[/QUOTE]

Mkuu kwa akili km hz za kwako cdm haiwezi kwenda mbele. Ni hv acheni upuuzi, mbowe ameshafanya yake inatosha. Mwenyekiti na mgomnea uraisi wa Tz ajaye ni Tundu Lissu period.
 
Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
Leo hii Kigogo anapuuzwa!!!!
 
Hakuna kiongozi anayekosa wapambe, lakini kiukweli Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm sio afya kwa cdm. Tunaosema hivi tuna mapenzi mazito na cdm kama taasisi, kuliko wapambe wake wachache wenye maslahi naye binafsi. Huu ni wakati sahihi wa mtu kama John Heche au Marcus Albanie kuwa mwenyekiti wa cdm, na Mbowe kubaki kama mjumbe maalum (VIP) wa cdm kwa afya ya chama.
Marcus ndo nani, au anaibula km mashinji? Mwenyekiti this time ni Tundu Lissu
 
Hv mko serious mnamtaka mbowe? Yaani 15 years haitoshi siyo? Iko hv ikiwa Tundu hatakuwa Mwenyekiti wa cdm this time propaganda za ccm kuwa cdm ni ya wachaga itakuwa confirmed
Hata mkisema mara 10 000. Haitusaidii kitu yaani leo hii ndiyo mnamuna lissu ana nafasi kwenu wakati mmeshamfukuza kwenye ubunge?

Wacheni unafiki wenu huo
 
Wanashindwa kuelewa kuwa Baba Yake Mbowe alimfadhili Nyerere kwenda kwa malkia kudai uhuru.
TATIZO KUBWA MBOWE HAFIKI BEI NA SII MNAFIKI.
Anayetumia pesa za umma kujenga chato hasemwi
So kwa mfano mungu aepushe mbali akafa leo ndo mwisho wa cdm? This time Mwenyekiti ni Tundu Lissu
 
So kwa mfano mungu aepushe mbali akafa leo ndo mwisho wa cdm? This time Mwenyekiti ni Tundu Lissu
Hata ukitaka awe chakubanga mwambie aje agombee au mpandikizeni lipumba aje tu
 
Naona povu linakuvuja wakati hata access ya kupiga kura huna [emoji111]
#Mbowe Tano Tena#

Mkuu kwa akili km hz za kwako cdm haiwezi kwenda mbele. Ni hv acheni upuuzi, mbowe ameshafanya yake inatosha. Mwenyekiti na mgomnea uraisi wa Tz ajaye ni Tundu Lissu period.[/QUOTE]
 
Marcus ndo nani, au anaibula km mashinji? Mwenyekiti this time ni Tundu Lissu

Marcus alikuwa mgombea ukatibu mkuu wa cdm uchaguzi uliopita. Nilishangaa sana yeye kuachwa na cdm badala yake akawa Mashinji. Huyo Marcus alibanie ndie angefaa hasa kuvaa viatu vya Dr. Slaa kwani ana uelewa mpana wa mambo na ni mjenzi mzuri wa hoja zenye ushawishi. Pia alikuwa mgombea ubunge katika tiketi ya cdm, Morogoro mjini na alipata kura za kutosha japo hakuwa mbunge. Lakini ni mtu sahihi sana kwa sasa kwenye ngazi za juu za cdm.

Sipingi kabisa Lissu kuwa mwenyekiti, lakini naona Lissu anapenda zaidi kugombea urais. Ni vyema tukaepuka utamaduni wa ccm wa rais kuwa ndio mwenyekiti wa chama.
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa

Chama cha ukombozi kikipata kiongozi imara hakimbadilishi badilishi

Kwa nini sasa mnataka nchi inayopigana kujikomboa kiuchumi na iliyompata kiongoz imara My John pombe magufuli ibadilishe kiongozi

Magufuli had 2030
 
Mbowe asingekuwa ni mkwe wa Mzee Mtei, Founder wa CHADEMA

Hoja ya kuwa haaachii nafasi kwa kuwa ni kiongoz imara ingekuwa na mashiko

Otherwise mengine ya kuwa CDM ni taasisi ya familia, ukabila, ukanda lazima yawe na mashiko
 
Kapige kura mkuu porojo hatasaidia

Nakubaliana na wewe mkuu, japo ni vizuri zaidi wakati wa hizo kura Mbowe awe pembeni ya kinyang'anyiro. Hii ni kwa heshima ya taasisi kubwa kama cdm na demokrasia ya kupokezana vijiti.
 
Huyo kigogo wa Twitter sometimes anaweza akawa 'upgraded latest version' ya Msiba..

maana dola inashindwaje kudeal naye!

ikiwa wameweza kumwangushia kesi nzito kama ya Aquilina Aquilline tena kweupe hadharani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom