Freeman Mbowe akutana na Raila Amolo Odinga

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe leo amekutana na Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, Mgombea Urais wa Muungano wa Azimio la Umoja na Mheshimiwa Martha Karua, Kiongozi wa Chama cha NARC Kenya Jijini Nairobi.

Kupitia kwao, Mheshimiwa Mbowe amewataka Wakenya wote kushikamana kuhakikisha kuwa uchaguzi wao unakuwa wa haki, huru na wazi.

Kipekee, amewasihi Viongozi na Wagombea hao kuhakikisha vurugu za uchaguzi zilizotokea nchini Kenya miaka ya nyuma na kusababisha vifo vya Wakenya kamwe havijirudii tena.

Aidha, amewataka kutambua nafasi ya Taifa la Kenya katika kuendeleza Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu katika Eneo la Jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba wanapaswa wakati wote kulinda na kuendeleza mafanikio hayo.

Mheshimiwa Mbowe amewatakia Wakenya wote mchakato mwema wa Uchaguzi wao wa August 2022.

IMG-20220330-WA0029.jpg
 
Mbowe ajifunze Siasa za Raila

Raia aliwahi kujiunga na Daniel Arap Moi, akawahi kujiunga na Mwai Kibaki na pia kajiunga na Uhuru Kenyata

Lakin kubwa zaid sometime inaruhusiwa kuwatosa Wahafidhina kama kina Miguna miguna waliokataa kuelegeza misimamo
 
Hivi Wachaga wamekosa kweli mtu wa kumuamini na kuwaongoza ? Mbona Wachaga wengi sana wapo ni wasomi wazuri wangeweza kuwawakilisha Wachaga kuliko huyu sellout.

Ni aibu kubwa sana kwa Wachaga kuongozwa na mtu kama Mbowe, aibu!
 
Hivi Wachaga wamekosa kweli mtu wa kumuamini na kuwaongoza ? Mbona Wachaga wengi sana wapo ni wasomi wazuri wangeweza kuwawakilisha Wachaga kuliko hiyu sellout.
Ni aibu kubwa sana kwa Wachaga kuongozwa na mtu kama Mbowe, aibu!
Ni maoni tu,yakwako na aliyekutuma,ila wenyewe wameridhia Kwa moyo na wapopamoja nae Kila hatua kwani imani yao ni kuwa Mwamba ataeafusha.🤔
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe leo amekutana na Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, Mgombea Urais wa Muungano wa Azimio la Umoja na Mheshimiwa Martha Karua, Kiongozi wa Chama cha NARC Kenya Jijini Nairobi.

Kupitia kwao, Mheshimiwa Mbowe amewataka Wakenya wote kushikamana kuhakikisha kuwa uchaguzi wao unakuwa wa haki, huru na wazi.

Kipekee, amewasihi Viongozi na Wagombea hao kuhakikisha vurugu za uchaguzi zilizotokea nchini Kenya miaka ya nyuma na kusababisha vifo vya Wakenya kamwe havijirudii tena.

Aidha, amewataka kutambua nafasi ya Taifa la Kenya katika kuendeleza Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu katika Eneo la Jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba wanapaswa wakati wote kulinda na kuendeleza mafanikio hayo.

Mheshimiwa Mbowe amewatakia Wakenya wote mchakato mwema wa Uchaguzi wao wa August 2022.View attachment 2169612View attachment 2169614View attachment 2169613
Ni jambo jema!
 
Back
Top Bottom