Free talk: Mwanamke shtuka!

Wanawake walio wengi huolewa ili kupata sifa mtaani kuwa kaolewa pasipo kujua kuwa kuna mambo anatakiwa kuyazingatia na kuyafanya yeye kama mke...Neno msaidizi lina maana kubwa ambayo wanawake walio wengi wanafikiri ni kuingia katika ndoa kwa lengo la kuzaa na kulea watoto, kupika, kufua...Hapana!!!!

Yakiwemo yote hayo, mke anatakiwa asaidizane na mumewe kutimiza malengo yao, kwa ushauri na utendaji. Mwanamke aliye bora ni yule mwenye mawazo mazuri ya maendeleo, asiye na mtazamo wa kufanyiwa kila kitu na mumewe, msimamizi wa maendeleo, mtetezi wa haki ya familia yake na mwenye kiu ya kutimiza ndoto zake pamoja na ndoto za familia yake (mume na watoto).

Kama mwanamke umeingia ndoani bila kujua nini unakwenda kufanya tofauti na kuzaa basi daima utakuwa mzigo kwa mumeo... Tafsiri ya MSAIDIZI itageuka na kuwa jeraha kwa mumeo.. Hatakuwa na mshauri wa karibu, hatakuwa na msimamizi wa maendeleo ya familia yake na vilevile anaweza fikia hatua ya kujuta kwanini aliamua kukuweka ndani..
 
Ngoja nijifunze kitu leo, ila umejua kumisika agemate wangu. Mada nzuri sana ngoja nisubiri michango ya wadau

Mada nzuri sana! wanawake wengi wa hivyo bahati mbaya mume akitangulie mbele yahaki wanazirika.Kwa kweli kila mtu aishi akijua kuna leo na kesho tusiwe tegemezi kwa kila kitu tuweze kusimama hata kama mume hayupo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamani khaah
 
Na kuna wanaume nao wanapenda kutegemewa ili wamuendeshe mwanamke. Anajua hata akufanyie nini hutapata uwezo wa kuondoka. Nawaambiaga rafiki zangu hata kama unapewa mpaka hela ya pad jifunze kutafuta chako ili siku kupewa kukikata ujue kujisimamia.
 
Naomba uniruhusu nije nikupose.. maana nahisi Duniani umebaki wewe tu
 
Na kuna wanaume nao wanapenda kutegemewa ili wamuendeshe mwanamke. Anajua hata akufanyie nini hutapata uwezo wa kuondoka. Nawaambiaga rafiki zangu hata kama unapewa mpaka hela ya pad jifunze kutafuta chako ili siku kupewa kukikata ujue kujisimamia.
Ndio wapo, wanapenda kunyenyekewa, na wanafanya hivyo sio kama wanakupenda sana, la hasha! Hapo ni kukulemaza na kukufanya mtumwa siku zote ndoani, ataamua lolote kwako kwasababu anajua huna ujanja wa kujiendesha mwenyewe na kwa namna yoyote ile hutakuwa na jeuri ya kuishi nje ya yeye....

Just imagine wewe wamtegemea mwanaume kila kitu, kuanzia vocha mpaka kula yako, utakuwa na ujanja gani kwake??? Hata akutende vibaya mara kibao bado utaendelea kumvumilia kwasababu ya UOGA wa maisha aliokutengenezea mwenyewe..
 
Mimi ndo maana natafutaga changu maana akili yangu kubadilika ni dakika moja. Sijawahi kumnyenyekea mwanaume kisa naishi kwa hisani yake. Na nilijifunza ukitaka maisha ya tabu ishi kwa kutegemea kila kitu kwa bwana. Mwanaume anakwambia usisome usifanye kazi usifanye biashara na wewe unakaa unafurahia tu. Mwanaume anaweza akatoa kila kitu alicho nacho kwa mwanamke wake ila siku za kuishi kwa binadamu ni chache sana. Kesho mwanaume hayuko mwanamke wake aliemfanya kilema ataishije? Maana hata aache Mali atazitapanya ziishe zote
 
Mumu laiti wadada wote wangekusikia na kuku elewa. Basi kizazi hiki kinge change. Ila sasa shida ni kuwa wadada wengi kwa sasa wanambebesha kila kitu boy wake.

Yes kuhudumia ni kazi ya mwanaume lakin waangalie situation zenyewe. Unakuta dada kwao wana uwezo kabisa au ana kazi, lakin boi wake anabebeshwa majukumu mpaka ya baba mzazi.
Ndio hapa mtu anakimbia unaanza kuuliza umemkosea nn.
 
Ni hulka tuu mbaya,..ila kama mwanaume unacho pia na unawiwa kumpa mpenzio MPE,..sio basi na nyie ndio heee!!!!kisa tunaweza okoteza senti mbili tatu ndio hamtununlii hata pipi ivory sio Poa,...
 
Huo uchoyo sasa. Kwanza ili upate zaidi unatakiwa uonyeshe shukrani japo kwa zawadi ya boxer tuu.
Kuna watu ujue hawatoi zaka,fungu la 10 wala sadaka ya kuteketeza wala ya kawaida si kanisani wala msikitini...lakini kumpa hata mtu pipi tuu ya 150 anaona dhambi,.basi hata uonge napo 0 jomoniii....mfyuuuu[emoji57]
 
Tabia mbaya tu, hii kampeni ya kutunyima fursa kwanini lakini[emoji57] [emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…