Free and Independent Zanzibar

jana samweli sitta kasema mnadaiwa hela kibao za umeme,tunaombeni hela zatu nyie waunguja!!mmeona vimafuta vitapatikana ndio mnaanza kelele zenu wala nguru wakubwa

hizo hela zikilipwa, mtaondoa wanajeshi wenu walioko zanzibar? Watu wanaelewa kanuni ya mtawala ni kumpandikizia deni anae mtawala... We shall overcome ...we shall overcome ... We shall overcome !!!
 
zanzibar's issue go way beyond muungano. Zanzibar seceding from the union will not change their economic situation contrary to what they want to believe. Wajitenge kwa sababu zingine ila si uchumi.

whatever the case, ...zanzibar nje ya muungano ina nafasi nzuri ya kimaendeleo...
 
POUND 600.000 YA MİAKA YA 60s , SIO SAWA NA POUND 600,000 YA MWAKA 2011... ACHENI UNAFIKI NA UPOTOSHAJI...

Takashi,

600,000 pounds. £1 pound ya miaka ya 1940-1960 ni sawa na £45-£40 ya sasa. Kwasababu hiyo :-
600,000 x 45 = £27,000,000

£27,000,000 ndio initial capital iliyotumbukizwa BOT.

Tukicompound for 50 years ya muungano (muungano sasa ni 47 years).

FV = 27,000, 0000 ((1 +0.071)(Tbills yields by January 2011))^50= £833,368,931.674 (Tuchukulie wazanzibar hawachangii BOT zaidi ya initial capital invested).

Tukiweka na michango yao BOT kila mwaka kutoka kwenye mauzo ya karafuu na utalii na kodi tunaweza kufikia kiwango cha £ Billion kadhaa.

Chenge hataweza kulipa na wala Serikali ya Tanzania haiwezi kulipa. Narudia tena Muungano ujadiliwe kwa busara na hekima wakuu na sio dharau na kebehi uchumi wa nchi hii unaweza kucollapse.
 
huko usa mnafanya nini???kubeba magunia??njooni msaidie ndugu zenu kuvua samaki!
labda hizo gunia anazobeba ndio zinafanya ndugu zake wapate pesa za kununua vyombo bora vya kuvua samaki na kuwapeleka ndugu zake shule. Si kweli kwamba ambae yupo nchini ndio anafanya more for his/her country kuliko aliye nje, huenda tena ambae yupo ndani ndio fisadi mkubwa kodi halipi na kila kukicha anauza nchi
 
Ni mtu mpumbavu tu anayeweza amini vitu kama hivi(note mpumbavu hafundishiki).
Na hizo hela zilikuwa zikitika Unguja , wakati waunguja wamelala usingizi au ilikuwaje?
Acheni uvivu wa kimwili na wa kufikiri.
Halafu kwa ujinga wenu hivi BOT ilikuwepo 1964?
OVYO!!!
 
Mh umekosea sana wanawake na analogy hii. Kumbuka wanawake ni mama zetu, dada zetu , wapenzi wetu. Si vizuri kuwa tusi hivi.
Bwana mukubwa fikiri kama thinker na si kuchukua mfano at face value.Read between the lines.
 
kuwa na adabu na heshima
kama zamani walikuwa taifa huru
wana haki ya kutaka kuwa huru tena

matusi yako yanaongeza hasira
nahisi umetumwa labda,kuwatukana na kuwachokoza wazanzibari
Same mistake buddy,
Kwanza,hivi unapoambiwa umewaibia wazenj wewe unachekelea tu.
Kama hilo si tusi la kuambiwa wewe ni mwizi basi sielewi maana ya neno tusi.
Pili, inaeleleka we ni kama wale watu wanaotumiwa as a face nappy au tissue.
Hawa haja yoa ilikuwa nini katika kuingia muungano in the first place, walichotaka wamepata? hilo nikuulize weye mkubwa
 
Majoja, huna sababu ya kuwashushia heshima kiasi hiki wenzako. Kwanza ukubali, Zanzibar ilikuwa ni nchi huru au la? Kama ilikuwa ni nchi huru na yenye rais wake, mnachoona shida kuturudishia tena ule uhuru wetu tuendelee na hamsini zetu wakati nyie mkiendelea na za kwenu ni nini? Tulumbane kwa hoja na si kwa kuwafananisha wengine na tissue. Hii ni dharau kubwa sana mkuu. Tambua kwamba wazanzibari ni watu kama wewe na katu hawapaswi kubezwa pale wanapoomba haki yao ya msingi ya kuwa huru.
 
imewakilisha
 
free zbr. Mimi ni mtanganyika na sipendezwi na serikal yangu kuendelea kunyima zbr uhuru. Wazanzibar fanyeni mapinduz mengine. Shamhuna awe kiongoz wa serikal maana yeye pekee sio mnafik ktk suala hilo. Ccm iache upumbavu wa kulazmisha watu limuungano ambalo hawalitaki. Sitaki muungano, nataka nchi yangu TANGANYIKA.
 
Wazanzibar kwa asilimia kubwa sana mlichagua serikali ya mseto na CCM, sasa hivi kelele za kutokuwa huru zinatoka wapi wakati hata mwaka hamjamaliza ktk ndoa yenu?
 
Msema hovyo, kusema ukweli, kutokushukuru kwa lolote kuhusu muungano, ni ukosefu wa shukrani.
Panapo majaaliwa 2015 nitapenyesha karata yangu pahali, nikifanikiwa nitakuwa miongoni mwa nitakao waunga mkono mpate mnachotaka. Tukiendelea hivi, sio tena kuhusu kero za muungano, sasa ni kero za wanaotaka kuuvunja muungano, ili isiwe kero, mtakipata tuu mnachokitafuta. Naamini, atufutae, hachoki, na akichoka, kesha pata.

Hii hoja yako ya "kwa taarifa yako millions of Arabs were already dead", haina mashiko, japo ni kweli maelfu walikufa, nilisoma mahali population ya Zanzibar ilikuwa around laki 6-8. Waliokufa ni 86,000, sasa hao millions walitoka wapi?.
 
Hakiii, Munanifurahisha sana kwa comments zenu. Nina washangaa watu wazima wanasema maneno ya kitoto sana. Hizo 50 billion ni pesa za tanzania. Hivo katika fikra zenu kuwa hiyo ndio itakayotuzuia kutetea UHURU wetu?. Fanyeni hesabu za haraka haraka.

Mid-market rates: 2011-07-11 00:07 UTC
50,000,000,000.00 TZS = 31,397,177.40 US

hizi ndio vijisenti wanavyotudai. hahahahahahahaha. Eti Zanzibar inadaiwa na tanesco yaguju. Chukueni mutuachie nchi yetu mumesahau mulioiba karafuu. Mumesahau kama BOT ni pesa za Zanzibar. Amir Jamal amekufa lakini wenzake wengi bado wapo hai. Ile Dhahabu tani 600 ya zanzibar muliipeleka wapi?. Nyinyi muna vichwa vibovu sana tukianza kuwadai, ziwa tanganyika litakauka. "Lake tanganyika will cease (dry up)"
 
sidhani after 50yrs kama muungano bado utakuwepo
 
Wazanzibar kwa asilimia kubwa sana mlichagua serikali ya mseto na CCM, sasa hivi kelele za kutokuwa huru zinatoka wapi wakati hata mwaka hamjamaliza ktk ndoa yenu?

Napenda nikujuze kuwa Mseto ule ni wa Znz kwa Znz na wala hauwezi kabisa kuhusisha wa Tanganyika. Mseto ule umewekwa kwa ajili ya maslahi ya Znz na kwa waZanzibar. na wala si kwa WaTanganyika.

Lakini hapa kinachoongelewa ni Muungano na uhuru wa Znz kujikomboa dhidi ya Tanzania.
 
Hivi nani anamuhitaji mwenzake?ZNZ or Danganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…