Jana tumeshuhudia kuzaliwa kwa taifa jipya la Sudan kusini, baada ya harakati za muda mrefu za mapambano ya kutafuta kuwa huru dhidi ya Sudani ya kaskazini. Hili ni somo mhimu sana kwetu wazanzibari ambaye kwa muda mrefu tumeishi kwa kuamliwa mambo na watanganyika.
Umasikini wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa umesababishwa na wabara ambao wamekuwa na mipango mibovu na wala rushwa halafu wanahamishia mipango yao ya hovyohovyo kule kwetu zanzibar na kutusababishia umasikini mkubwa na hali ngumu ya maisha.
Wazanzibar tuko wachache, kipato chetu kinatosha kutulisha sisi wote na kutuhakikishia maisha yenye neema, lakini kutokana na Muungano, kipato chetu tunashare na wabara, halafu gawiwo tunalopata linakuwa dogo na kutufanya tuonekane na sisi ni maskini kama walivyo wa bara.
Sasa tunataka uhuru wetu, tunataka tujitawale, hatutaki kupangiwa mambo na wabara. Seriously we are going for it.