Msema hovyo
Senior Member
- Jul 3, 2011
- 195
- 86
Msema hovyo, itakuwa ulizaliwa baada ya mapinduzi matikufu ya Januari 64 ndio maana inasema hovyo. Uhuru gani huo unaouulizia. Zanzibar si ilipata uhuru wake Desemba 1963?, sasa uhuru gani tena mnaoutaka.
Muungano wetu ni ndoa ya ukweli ya mkeka iliyoongiwa kwa convenience. Ndoa ni ndoa hata ikiingiwa kwa hiari ni binding na haiwezi kuvunjika kwa hiari hata kama mmoja wa wanandoa hakuingia kwa hiyari na kesha ichoka ndoa yanyewe, bado haiwezi kuvunjika.
Ukiona mke amekuchoka na kuanza kukufanyia visa, ujue kesha pata bwana mwingine hivyo anafanya visa ili apewe talaka akajinafasi. Bara tumeshalibaini hilo, tena bwana mwenyewe ni mafuta ambayo hayajai hata kwenye kinibu!. Visa fanyeni, talaka kamwe hatutoi na ndoa itadumu daima. Muungano Milele!
Mungu ibariki Tanzania.
Pasco.
Na wao walipeni pound 600,000 walizoanzishia benki kuu ya Tanzania 1960s na US dollar zao zilizotumika katika vita vya kagera kutoka kwenye mauzo ya karafuu yaliyopita.
Dharau mkuu hazitaleta mwafaka wala kuelewana hekima na demokrasia ndio solution ya muungano huu. Serikali 3 au muungano kuvunjika kabisa kwa ustaarabu.
MOVED TOSudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati
Sudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati
Duh, Zumbemkuu!!! nafikiri hapa hujaitendea haki thread yangu? Kwani ni mkoa gani mwingine ambao ulipigania uhuru wake binafsi, ukawa na bendera yake, na alama zote za taifa halafu ghafla huo uhuru ukanyang'anywa? Ukumbuke Zanzibar ni nchi ambayo ilipigania uhuru wake na ikajitawala kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kunyang'anywa huo uhuru na Nyerere.hivi mnaonaje ikiwa kila mkoa ikiwa ni nchi inayojitegemea halafu tuwe kwenye shirikisho? nadhani ufisadi utapungua.
inabidi muupiganie kwa vitendo sio kwa maneno!
Si na ndiyo maana tunasema tuachieni nchi yetu, maana tunachokizalisha Zanzibar kinatutosha kabisa, maana hatuhitaji vikubwa kama ninyi. Sasa kitendo cha kuwa kwenye muungano kila kitu mnatupangia, kiasi cha kwamba tunashindwa kufanya maendeleo yetu binafsi. Tunabaki tumeconcentrate kwenye issue za muungano ambazo hazitusaidii kwa lolote.jamani hizo paundi laki sita zinaweza kulipwa na chenge tu peke yake; hivi mnajua bajeti nzima ya Zanzibar ni sawa na bajeti ya Wizara moja tu ya Muungano!?
Duh, Zumbemkuu!!! nafikiri hapa hujaitendea haki thread yangu? Kwani ni mkoa gani mwingine ambao ulipigania uhuru wake binafsi, ukawa na bendera yake, na alama zote za taifa halafu ghafla huo uhuru ukanyang'anywa? Ukumbuke Zanzibar ni nchi ambayo ilipigania uhuru wake na ikajitawala kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kunyang'anywa huo uhuru na Nyerere.
Lipeni kwanza deni la Bilioni 50 kwa kuwapatieni umeme, halafu mnasepa tu.
Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure.
Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu.
Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.
Sudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati
Fine, lakini mkumbuke kwamba ni lazima iwe declared before international acts kwamba sasa imekuwa ni nchi halali. Ndiyo maana tunasema tunataka uhuru wetu. Mkubali kwamba mnatuacha tuishi na kujijenga kama nchi, mdeclare mbele ya sheria zote za kimataifa zitakazoitambua zanzibar kama nchi, na si kirahisi rahisi hivyo kusema eti tuachie madaraka tuende zetu! Halafu tukifanya hivyo? Nani atakayetutambua kwamba ni nchi?na wala haitakuwa kazi kubwa, ni kuchukua hatua ya kuachia madaraka yote yanayohusu muungano then warudi kwao.
Tunajua fika ukweli huo kwamba uhuru wa zanzibar ulipatikana mwaka 1963, hilo halina ubishi, lakini waarabu ndo waliokuwa wamekabidhiwa huo uhuru, na mapinduzi ya 1964, yalilenga kumpa utawala mzanzibari mzalendo. Bila shaka mwanakijiji una kumbukumbu nzuri ni mara ngapi ASP ilinyang'anywa ushindi wake na waarabu kiasi cha kuamua kuopt mapinduzi kama njia mbadala ya kurudisha utawala kwa wazalendo. Lakini hayo hayakufanyika ili kutoa mwanya kwa Tanganyika kututawala, bali wazanzibari wazalendo kujitawala wenyewe.sidhani kama unajua kilichotokea siku ya mapinduzi; mmeaminishwa soga mkaziamini. Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwa kuhusu Uhuru, Zanzibar ilikuwa tayari huru by the time mapinduzi yanafanyika.