Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,013
- 967
MBUNGE MHE. FREDRICK LOWASSA AZIWEZESHA VIFAA VYA TEHAMA SHULE ZA MSINGI NNE
Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoa wa Arusha, Mhe. Fredrick Edward Lowassa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Joshua Nassari wamegawa vifaa vya TEHAMA kwa Shule za Msingi Nne, Shule ya Msingi Losimongori; Losingiria; Lolkisale; na Manyara Ranch.
Vifaa alivyokabidhi Mhe. Fredrick Edward Lowassa kwa hizo Shule za Msingi Nne ni pamoja na;
1. Projekta (Projector)
2. Kompyuta ya Mezani (Desktop)
3. Mashine ya Fotokopi (Photocopy Machine & Printer)
Mhe. Fredrick Edward Lowassa amesema kuwa amefanya hivyo kwa sababu ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa mashindano ya michezo mbalimbali iliyofanyika jimboni yaliyojulikana kwa jina la Fredrick Lowassa CUP.
Aidha, Mhe. Fredrick Edward Lowassa amewapatia watu wa Jeshi la Magereza Wilaya ya Monduli Kompyuta (Computer) moja itakayowasaidia katika kazi mbalimbali za kiofisi.
Mhe. Fredrick Edward Lowassa amesema lengo la kuanzishwa kwa mashindano ya Fredrick Lowassa CUP ni ili kutambua, kulea, kutunza na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia michezo kwani michezo ni fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji.