Fredrick Edward Lowassa aziwezesha Vifaa vya TEHAMA shule za msingi nne

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,940
951
MBUNGE MHE. FREDRICK LOWASSA AZIWEZESHA VIFAA VYA TEHAMA SHULE ZA MSINGI NNE

Mbunge wa Jimbo la Monduli Mkoa wa Arusha, Mhe. Fredrick Edward Lowassa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Joshua Nassari wamegawa vifaa vya TEHAMA kwa Shule za Msingi Nne, Shule ya Msingi Losimongori; Losingiria; Lolkisale; na Manyara Ranch.

Vifaa alivyokabidhi Mhe. Fredrick Edward Lowassa kwa hizo Shule za Msingi Nne ni pamoja na;
1. Projekta (Projector)
2. Kompyuta ya Mezani (Desktop)
3. Mashine ya Fotokopi (Photocopy Machine & Printer)

Mhe. Fredrick Edward Lowassa amesema kuwa amefanya hivyo kwa sababu ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa mashindano ya michezo mbalimbali iliyofanyika jimboni yaliyojulikana kwa jina la Fredrick Lowassa CUP.

Aidha, Mhe. Fredrick Edward Lowassa amewapatia watu wa Jeshi la Magereza Wilaya ya Monduli Kompyuta (Computer) moja itakayowasaidia katika kazi mbalimbali za kiofisi.

Mhe. Fredrick Edward Lowassa amesema lengo la kuanzishwa kwa mashindano ya Fredrick Lowassa CUP ni ili kutambua, kulea, kutunza na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia michezo kwani michezo ni fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji.

WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.32.45(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.32.46.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.32.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.32.44(1).jpeg
 
Mbona hatuambii Mzee anaendeleaje?
Mambo ya familia za watu ya nini ndugu? Huwa unaamka kila siku na kujulishwa kila mtu anaendeleaje?

Mjulie hali hata mjomba wako huko kijijini ( just jokes)
 
Hongera bwana lowassa jr.

Naona mnarudisha Mali mlizovuna Kwa watz

..ametoa computer 2 kwa shule moja.

..tujiulize hiyo shule ina waalimu na wanafunzi wangapi.

..pia tujiulize Fred Lowassa ana computer ngapi nyumbani kwake.

..Mwisho, tujiulize kama tuko makini na elimu na maarifa yanayotolewa ktk shule zetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom